Afrika Kusini: Mahakama yaagiza mwili wa Edgar Lungu kurejeshwa Zambia

Radio Fortune Africa -Na Cantona Joseph

https://zeno.fm/radio/radio-fortune-africa

Mahakama nchini Afrika Kusini imeipa ruhusa serikali ya Zambia kuurejesha mwili wa Rais wa zamani Edgar Lungu nchini Zambia licha ya familia yake kupinga hatua ya serikali kutaka mwili wake uzikwe Lusaka.

Rais wa zamani wa Zambia
Rais wa zamani wa Zambia REUTERS – Lucas Jackson

Katika uamuzi wa mahakama, serikali inatakiwa kuandaa mazishi ya kitaifa kwa ajili ya kiongozi huyo wa zamani.

Serikali ya Zambia ilikuwa imekata rufaa kupinga mipango ya familia ya Lungu kuuzika mwili wake katika hafla ya kisiri nchini Afrika Kusini kufuatia kifo chake mwezi Juni.

Kulingana na mawakili wa serikali ya Zambia, uamuzi wa mtu binafsi hauwezi kupita masilahi ya nchi.

Mzozo huo unatokana na uhasama wa muda mrefu kati ya Lungu na mrithi wake Rais Hakainde Hichilema, familia ya Lungu ikisema kwamba mpendwa wao hakuwa akitaka Hichilema kuhudhuria mazishi yake.

Kufuatia kifo cha Lungu akiwa na umri wa miaka 68, familia yake ilitaka kuongoza mipango ya mazishi yake ikiwemo kuurejesha mwili wake nchini Zambia, serikali nayo ikitaka kupanga mazishi yake.

Serikali na familia yake baadaye walikubaliana kuandaa mazishi ya kitaifa kwa ajili ya Lungu kabla ya mzozo kuibuka kati ya pande hizo mbili, familia yake ikiamua kuuzika mwili wa Lungu nchini Afrika Kusini.

All Rights Reserved © The Cantona Group PLC||2025


Discover more from cantonadigital

Subscribe to get the latest posts sent to your email.

Leave a Reply