Radio Fortune Africa -Na Cantona Joseph
https://zeno.fm/radio/radio-fortune-africa
Nchini Kenya, wasiwasi unaongezeka kuhusu msururu wa utekaji nyara na visa vya watu kutoweka unaodaiwa kutekelezwa na polisi katika wiki za hivi karibuni. IPOA, Halmashauri ya utendakazi wa polisi, imepaza sauti katika taarifa kwa vyombo vya habari iliyochapishwa siku ya Jumatano, Desemba 25. Taasisi hiyo inatangaza kuwa imeanzisha uchunguzi.
Kutoweka kwa watu wawili kumewakasirisha Wakenya kwenye mitandao ya kijamii katika siku za hivi majuzi. Peter Muteti na Billy Mwangi, vijana wawili maarufu kwenye mtandao wa kijamii wa X, walitekwa nyara mwisoni mwa juma lililopita, na kuingizwa kwa nguvu ndani ya gari na watu wasiojulikana.
Walikuwa wamechapisha picha zilizotengenezwa na akili bandia siku chache zilizopita, zikimuonyesha Rais wa Kenya William Ruto kwenye jeneza. Hadi Jumatano Desemba 25 jioni walikuwa bado hawajapatikana. Sawa na Wakenya wengine watatu, pia waliotekwa nyara katika siku za hivi majuzi, kulingana na vyombo vya habari nchini humo.
“Maafisa wetu wamefika maeneo ambako matukio haya yalitokea kutafuta taarifa kuhusiaa na visa hivi na kujua iwapo polisu walihusika” , amesema Issack Hassan Mwenyekiti wa IPOA.
“Iwapo makosa yatapatikana, tutatuma mapendekezo kwa hatua kuchukuliwa” , Issack Hassan ameongeza.
Katika taarifa yake kwa vyombo vya habari, IPOA inataja visa vya watu wanne waliotoweka kwa mwezi wa Desemba, ikiwa ni pamoja na Peter Muteti na Billy Mwangi. Halmashauri ya utendakazi wa polisi inasema “ina wasiwasi na ongezeko la utekaji nyara, unaodhaniwa kutekelezwa na maafisa wa polisi ya taifa” na inamtaka mkuu wa polisi kuchukua hatua.
All Rights Reserved © Cantona Group PLC||2024
Discover more from cantonadigital
Subscribe to get the latest posts sent to your email.