Radio Fortune Africa -Na Cantona Joseph
https://zeno.fm/radio/radio-fortune-africa
Mashirika ya chakula ya Umoja wa Mataifa yameonya siku ya Alhamisi Oktoba 31, 2024 kuhusu kuongezeka kwa viwango vya njaa katika muda wa miezi saba ijayo katika maeneo mengi ya dunia, huku Gaza, Sudani, Sudani Kusini, Mali na Haiti zikiwa na wasiwasi mkubwa.

Migogoro na vurugu za kutumia silaha husababisha sehemu kubwa ya uhaba mkubwa wa chakula katika maeneo yote yaliyotathminiwa katika ripoti ya kila mwaka ya Shirika la Chakula na Kilimo la Umoja wa Mataifa (FAO) na Shirika la Mpango wa Chakula Duniani (WFP).
Hali ya hewa kali ni jambo muhimu katika maeneo mengine, wakati ukosefu wa usawa wa kiuchumi na viwango vya juu vya madeni katika nchi nyingi zinazoendelea vinadhoofisha uwezo wa serikali wa kukabiliana na hali hiyo, kulingana na ripoti ya pamoja iliyohusu kipindi cha kuanzia Novemba 2024 hadi mwezi Mei 2025.
Hatua za kibinadamu zinahitajika haraka ili kuzuia njaa na vifo katika Ukanda wa Gaza, Sudani, Sudani Kusini, Haiti na Mali, inasema ripoti hiyo, ambayo inategemea utafiti kutoka kwa wataalam katika mashirika mawili ya Umoja wa Mataifa yenye makao yake makuu mjini Roma.
“Kwa kukosekana kwa juhudi za haraka za kibinadamu na hatua za pamoja za kimataifa za kushughulikia vikwazo vikubwa vya ufikiaji na kwa lengo la kupunguza migogoro na ukosefu wa usalama, njaa na kupoteza maisha kunaweza kutokea” katika maeneo haya, ripoti hiyo inaonya.
Nigeria, Chad, Yemen, Msumbiji, Burma, Syria na Lebanoni pia ziko katika hali ya wasiwasi mkubwa.
Ripoti inaangazia “hali mbaya zaidi” na kwa hivyo haiwakilishi “nchi/maeneo yote yanayokumbwa na viwango vya juu vya uhaba wa chakula”, wanakumbusha waandishi wa ripoti hiyo.
Mwaka wa 2024 ni mwaka wa pili mfululizo wa kupungua kwa ufadhili wa misaada ya kibinadamu na mipango kumi na mbili katika sekta ya usalama wa chakula ambao ilikabiliwa na mapungufu ya ufadhili wa zaidi ya 75% katika nchi kama Ethiopia, Yemeni, Syria na Burma.
– Matukio mabaya zaidi bado yanakuja –
Viwango vya ukosefu wa usalama wa chakula hupimwa kwa kiwango cha 1 hadi 5, na kiwango cha mwisho kinalingana na hali ya “janga”.
Katika Ukanda wa Gaza, kuongezeka kwa uhasama hivi karibuni kumezusha hofu kwamba hali ya “janga” la njaa inaweza kutokea, kulingana na ripoti hiyo.
Takriban 41% ya watu, au watu 876,000, watakabiliwa na viwango vya “dharura” vya njaa, kiwango cha 4, kuanzia mwezi wa Novemba hadi mwisho wa mwezi wa Aprili, wakati karibu 16%, au watu 345,000, watapata viwango vya “janga”, kulingana na ripoti.
Kufikia katikati ya mwezi wa Oktoba, watu milioni 1.9, au 91% ya wakazi wa Gaza, walikimbia makazi yao.
Nchini Sudani, mamia ya maelfu ya watu waliokimbia makazi yao kutokana na mzozo wataendelea kukabiliwa na njaa, kulingana na chanzo hicho.
Nchini Sudani Kusini, idadi ya watu wanaokabiliwa na njaa na vifo tayari inatarajiwa kuongezeka maradufu katika muda wa miezi minne kati ya mwezi Aprili na mwezi Julai 2024 ikilinganishwa na kipindi kama hicho mwaka 2023.
Lakini takwimu hizi zinaweza kuwa mbaya zaidi kuanzia mwezi wa Mei 2025 kwa kipindi kinachofuata na kutangulia mavuno mawili.
Kwa mujibu wa ripoti hiyo, zaidi ya watu milioni moja wameathiriwa na mafuriko makubwa mwezi huu nchini Sudani Kusini, nchi ambayo imekumbwa na machafuko na mdororo wa kiuchumi.
Vile vile, vurugu za kutumia silaha nchini Haiti, pamoja na mgogoro wa kiuchumi na vimbunga, vinaweza kuwa hatari ya kuongezeka kwa viwango muhimu vya njaa.
Kuongezeka kwa mzozo nchini Mali, ambapo Umoja wa Mataifa uliondoa ujumbe wake wa kulinda amani mwaka 2023, kuna hatari ya kuongezeka kwa viwango muhimu tayari kwa makundi yenye silaha kuweka vizuizi barabarani na kuzuia utoaji wa misaada ya kibinadamu.
Athari za moja kwa moja na zisizo za moja kwa moja za migogoro katika ukosefu wa chakula ni kubwa, kulingana na ripoti hiyo, na huenda zaidi ya uharibifu wa mifugo na mazao.
Migogoro inawalazimu watu kukimbia makazi yao, “kuvuruga maisha na mapato, kuzuia upatikanaji wa masoko na kusababisha kushuka kwa bei na uzalishaji na matumizi ya chakula kisicho kawaida.”
Katika baadhi ya maeneo yanayofikiriwa kuwa ya wasiwasi, hali mbaya ya hewa inayosababishwa na uwezekano wa kutokea tena msimu huu wa baridi wa La Niña, hali ya asili ya hali ya hewa ambayo inaweza ama kusababisha mvua kubwa au kuzidisha ukame na mawimbi ya joto, inaweza kuzidisha majanga ya chakula, kulingana na ripoti hiyo.
Kusambaza :
All Rights Reserved © Cantona Group PLC||2024
Discover more from cantonadigital
Subscribe to get the latest posts sent to your email.