Radio Fortune Africa -Na Cantona Joseph
https://zeno.fm/radio/radio-fortune-africa
Alejandro Arcos Catalan, meya wa Chilpancingo, mji mkuu wa jimbo la Guerrero kusini mwa Mexico, ameuawa siku sita baada ya kuchukua wadhifa huo, mamlaka ya ndani imetangaza.

Afisa huyo aliyechaguliwa mwenye umri wa miaka 43 alikatwa kichwa na kichwa chake kuachwa juu ya gari, kulingana na vyombo vya habari vya ndani. Picha ya kusikitisha ilishirikiwa kwenye mitandao ya kijamii, kisha ikafutwa.
“Ninalaani vikali mauaji ya rais wa baraza la manispaa ya Chilpancingo, Alejandro Arcos Catalan, taarifa ambayo Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali imethibitisha,” amebainisha kwenye mtandao wa X gavana wa Jimbo la Guerrero Evelyn Salgado, aliyechaguliwa kutoka chama cha Movement for National Regeneration ( Morena, mrengo wa kushoto) madarakani.
Ofisi ya Mwendesha Mashtaka wa Serikali imetangaza katika taarifa kwa vyombo vya habari kufunguliwa kwa “faili la uchunguzi wa uhalifu wa mauaji uliofanywa dhidi ya Alejandro +N+ kwa matukio yaliyotokea Chilpancingo”.
Ofisi ya mwendesha mashtaka wa umma imerejelea ahadi yake ya “upatikanaji wa haki na dhidi ya kutokujali”, katika nchi ambayo uhalifu mwingi haujaadhibiwa.
Meya huyo aliuawa “siku tatu tu baada ya katibu wa Halmashauri ya manispaa ya mji huo, Francisco Tapia kuuawa”, amesema mkuu wa chama cha upinzani cha PRI, Alejandro Moreno. “Walikuwa na chini ya wiki baada ya kuanza kazi.”
Makumi ya wagombea waliuawa wakati wa mchakato wa uchaguzi kabla ya uchaguzi wa Juni 2 (34, kulingana na shirika lisilo la kiserikali la DataCivica).
Chilpancingo iko kilomita 16 kutoka Chuo Kikuu cha Ayotzinapa, ambapo wanafunzi 43 walitoweka miaka kumi iliyopita baada ya usiku wa vurugu, kisa mfano wa takriban watu 100,0000 waliotoweka nchini Mexico.
Mauaji hayo yametokea siku tano baada ya kuapishwa kwa Rais Claudia Sheinbaum, ambaye anatarajiwa kuwasilisha mpango wake wa usalama wa taifa siku ya Jumanne.
All Rights Reserved © Cantona Group PLC||2024
Discover more from cantonadigital
Subscribe to get the latest posts sent to your email.