Afrika Leo Asubui-Bao La Asubui.

https://zeno.fm/radio/radio-fortune-africa

Na Cantona Joseph -Radio Fortune Africa.

Unashindwa kuongeza mauzo ya biashara yako? Njia rahisi zaidi ya kuongeza mauzo yako, huku ukiwa unagusa jamii yako… …“Cause Marketing”.

Kwa mujibu wa utafiti wa MailChimp, imeonekana kuwa takribani 70% ya wanunuzi huwa wanapenda…

…kujua mchango wa kampuni wanazonunua katika jamii husika.

https://zeno.fm/radio/radio-fortune-africa

Unachofanya hapa, ni kuunganisha mauzo yako na kuchangia/kusaidia jambo fulani katika jamii.

Ili kujua usaidie kitu gani unapaswa kuangalia vifuatavyo:

Angalia kitu kinachoendana na Brand yako.

Ni vizuri kuoanisha unachokifanya na unachosapoti.

Mfano, kama wewe unauza bidhaa za watoto, ukisema kuna pesa ya mauzo utapeleka kwenye matibabu ya…

…watoto wenye ugonjwa wa moyo inaeleweka kwa haraka zaidi KULIKO ukisema utaenda kupanda miti.

Pili, jaribu kuchunguza wateja wako wanathamini mambo gani zaidi ndio uyatumie kama mchango wako kwa jamii.

Usijiingize katika kampeni ambazo wateja wako hawatona thamani…

…au umuhimu wake kwa haraka.

Ukisikia mtu anasema “Kwa kila bidhaa/ticket utakayonunua asilimia 10% inaenda kuchangia jambo fulani”…

…ujue hapa inatumika mbinu ya “Cause Marketing”.

Je, ulishawahi kuona mtu/taasisi inatumia mbinu hii?

Tushirikishe kwenye comments tujifunze kwa pamoja.

All Rights Reserved © Cantona Group Ltd||2024


Discover more from cantonadigital

Subscribe to get the latest posts sent to your email.

Leave a Reply