Usiogope KUTOKUELEWEKA kwa kufanya JAMBO sahihi Bali…
…OGOPA kueleweka huku ukijua UNAPOTEA.
Huu ni MTEGO hatari ila lazima UUVUKE.
Watu wengi WAMEKWAMA HAPA.
Kuna wakati DUNIA inaweza kukufikisha hapa.
Yaani, inakulazimisha UCHAGUE…
…kati ya KUSIMAMIA unachokiamini…
…ukiwa umebakia PEKE YAKO.
Au UPOTEZE mwelekeo…
…ukiwa UNASHANGILIWA na wengi.
Kuna ambao inawatokea kwenye KAZI wanazofanya…
…wanajua wanachopaswa KUSIMAMIA…
…ila Hofu ya kubakia PEKE yao inawasumbua.
Hii inaweza kukutokea kwenye MAHUSIANO…
…unajua uamuzi sahihi wa kufanya…
…ila mtego wa kubakia peke yako unakusumbua.
Hata ukiwa KIONGOZI, huu ni mtego mgumu pia.
Kusimamia unachokiamini ambacho ni…
…SAHIHI huku ukiwa na wengi wanaokupinga.
Kutoeleweka kwa MUDA MFUPI kwa jambo lililo sahihi ni…
…bora zaidi kuliko kupoteza mwelekeo…
…kwa sababu ya kutaka kuwaridhisha wengi.
Nakuombea UJASIRI wa KUFANYA kilicho SAHIHI.
HakiMiliki © Cantona Group Ltd|2024
Discover more from cantonadigital
Subscribe to get the latest posts sent to your email.