Wakati wa crisis ndoto nyingi hufa.

Usisahau kuwa ndoto nyingi sana huwa ZINAKUFA watu wanapopitia “CRISIS” za maisha.

Pale mtu anapokuwa amepoteza PESA nyingi sana kwa hasara kubwa au kutapeliwa. Mwingine ni MADENI makubwa yaliyo Juu ya uwezo wake.Anaweza kuua kabisa ndoto Yake ya kuja kufanikiwa tena kifedha/Kibiashara.

Wengine baada ya kupitia Hali ya mahusiano KUVUNJIKA,huwa MAONO Yao yanasambaratika kabisa.

WAPO ambao walipoteza kabisa ndoto zao baada ya KUPOTEZA KAZI ambayo waliamini ndio itawapa maisha kwa muda mrefu.

Kipindi Cha “Crisis” kina tabia ya kukufanya ujione HAUWEZI, HAUNA THAMANI na HAUTAINUKA TENA.

Kutakuwa kuna sauti ya Kukuambia hakuna mtu alipitia Kama unachopitia akainuka tena.

Sio kweli, yeyote UNAYEMUONA AMEFIKA JUU kwenye maisha yake, kuna siku alikutana na “CRISIS”.

Kumbuka kuwa ni “Phase” tu ya maisha, ITAPITA. Ili uwe Salama, USIKUBALI kuamini kuwa UMEKWISHA, bado UNAYO NAFASI.

All Rights Reserved|© Cantona Group Ltd


Discover more from cantonadigital

Subscribe to get the latest posts sent to your email.

Leave a Reply