Mungu akukutanishe na mtu aliyebeba majibu yako.

Nakuombea Mungu akukutanishe na mtu aliyebeba majibu yako ambaye

Wakati wengine wote wamekukata yeye atakupokea, wakati wengine wote wanapokuona huna maana yeye ataiona maana ya uwepo wako

Haya ni maombi yangu kwako leo, kumbuka wapelelezi kwasababu walikuwa wamebeba majibu ya Rahabu walilazimika kulala kwenye nyumba ya kahaba

Tena kahaba ambaye alikuwa ametengwa na wazazi wake, ndugu zake.Na fahamu kuwa wale wapelelezi wangeweza kufikia kwa mtu mwingine

Au wangeweza kukata kufikia kwa kahaba,lakini kwasababu walikuwa wamebeba majibu ya Rahabu walilazimika kumsaidia rahabu na madhaifu yake.

Mungu akuinulie huyo mtu iwe ni ofisini kwako, kwenye biashara,nimekuombea na huyo mtu atakupenda, atakutambulisha,atakubeba pamoja na madhaifu yako

Kama unaamini kwamba ujumbe huu nj kwa ajili yako comment “Bwana niinulie mtu aliyebeba majibu yangu na kwa neema yako nikutanishe nae” na itakuwa


Discover more from cantonadigital

Subscribe to get the latest posts sent to your email.

2 thoughts on “Mungu akukutanishe na mtu aliyebeba majibu yako.

Leave a reply to Stella Masasi Cancel reply