Neno linasema Suleimani alikua na wake 700 na masuria 300 lakini wake hao walimfanya amuache Mungu wa baba yake Daudi Mungu aishiye milele na kufwata miungu ya kigeni.Neno hili halimaanishi kama linavyosomeka huu ni ufunuo unaposikia neno mwanamke kwenye biblia linatumika kumaanisha Kanisa.Baada ya Mfalme Suleimani kushika nchi alijenga madhabahu nyingi sana yani makanisa mengi sana kwenye kila ufalme watu walitoka mbali kuja kusikiliza hekima aliyo pewa na Mungu baada ya kumsikia waliondoka na kwenda kufungua makanisa ambayo yalianzishwa kupitia yeye na ndio maana yanaitwa wake zake.Baadae ikatokea makanisa hayo yakaanza kuabudu tofauti ikatokea imani mpya iliyo letwa na watu fulani mwisho wakamshawishi mpaka Suleimani kubadili msimamo wake akajisahau akajikuta anafanya yasiyo mpendeza Mungu.Ni lazima umfahamu Mungu kabla hujaanza kumuabudu kama humjui Mungu hata nikikuombea leo kesho kutwa utarudia mambo uliyokuwa unayafanya,kama ulikuwa una muamini mganga leo ukapata shida ambayo mganga ameshindwa kukusaidia ukaja kwa Mungu akusaidie kama humjui Mungu (Yehova) ni nani hata ukipokea ufumbuzi ukipata shida utakimbia kwa mganga tena sio kwa Mungu,Mungu anachukia sana kwa wanao abudu miungu wengine na ndio sheria yake kuu Usiabudu Miungu Mingine.Imani chanzo chake kusikia soma neno la Mungu na hakikisha unasikia maneno yaliyo sahihi kuhusu Mungu ili kumjua si kila neno linafaa kusikia.Mtu anaposema suleimani alikua na wake 700 na anasisitiza kwamba alikua na mahawara wengine 300 huo ni uchanga wa akili Mungu hawezi kumbariki na kumpa mali na hekima muwasherati mwenye wanawake kila kona na wala si sheria ya Mungu kuwa na wake wengi namna hiyo.
Iposiku #Getinspired #CantonaJosephMotivates All rights reserved©2019

Discover more from cantonadigital
Subscribe to get the latest posts sent to your email.