Radio Fortune Africa-Habari Na Cantona Joseph
https://zeno.fm/radio/radio-fortune-africa

Muhtasari
- Makubaliano ya kukiri mashtaka ya watuhumiwa wa shambulio la 9/11 yabatilishwa
- Mashindano ya Olimpiki 2024: Joshua Cheptegei wa Uganda ajishindia medali ya dhahabu
- Kamala Harris achaguliwa rasmi kuwa mteule wa chama cha Democratic
Hujambo na karibu katika matangazo yetu ya moja kwa moja AFRIKA MWISHO JUMA, ikiwa ni tarehe 03/08/2024 Jina Langu Cantona Joseph

MWANAMUZIKI maarufu nchini Kenya wa nyimbo za injili Linet Munyali, almaarufu Size 8, ametangaza mwisho wa ndoa yake na mumewe DJ Mo, jambo lililoibua hisia kali miongoni mwa watumiaji wa mitandao ya kijamii.
Size 8 kwenye posti yake kwenye mtandao wa Instagram Alhamisi aliandika kwamba anaanza ukurasa mpya wa maisha kama mwanamke asiye na mahusiano na wanaume.
“Wakati mwingine ndoa huwa imara katika neema ya Mwenyezi Mungu na wakati mwingine pia ndoa husambaratika, hata hivyo Mungu ndiye Mkuu,” akaandika.
Aliandika kwamba ameolewa kwa miaka 11 lakini kuanzia sasa yeye hana mume.
“Nilikuwa kwenye ndoa kwa miaka 11 lakini kuanzia sasa mimi ni mwanamke hana mume,” akaandika.
Aliendelea kusema katika ukurasa wake kwamba ana imani na matumaini kwamba Mungu ndiye anayeongoza maisha yake na licha ya hayo, anamtukuza Maulana.
Mashabiki na wafuasi wa mitandao ya jamii wameachwa vinywa wazi kufuatia tukio hilo kwa sababu siku nne zilizopita Size 8 alikuwa ameweka picha kwenye Instagram akiwa na Dj Mo.
Katika picha hiyo mtandaoni, Size 8 aliandika, “Mtu anaweza kufuata au kukimbiza elfu moja lakini wawili wanaweza kufukuza au kukimbiza elfu kumi katika jina la Yesu.”
Wakenya walipokea habari hizo kwa hisia tofauti huku baadhi yao wakihoji kwamba hizi ni sarakasi za wasanii na kufananisha tukio hilo sawa na lingine lililokuwa la msanii Bahati na mkewe Diana Marua.
Vilevile, wafuasi wa wasanii hao wanahisi hizi ni mbwembwe za wawili hao na kwamba huenda wamewafichia kadi na kusema huenda wawili hao wako karibuni kuchomoa kibao cha muziki

MWANAMUZIKI staa wa nyimbo za injili kutoka Tanzania, Christina Shusho, amekiri kuwa anafurahia kuwa mama mkwe katika umri wake mdogo.
Akizungumza jana baada ya kuwasili nchini Kenya, mwimbaji huyo alisema kuwa japo alijuta hapo awali kuolewa akiwa na umri mdogo, sasa anajivunia kuwa mama mkwe.
“Najihisi vizuri kuwa mama mkwe katika umri mdogo sana. Niliomba harusi ya faragha, jambo ambalo binti yangu ataishi kukumbuka,” akasema nyota huyo wa nyimbo za injili kwa kukiri anatazamia sasa kuanza kuitwa nyanya.
“Nahisi kwamba nitakuwa na nguvu ya kucheza na wajukuu wangu sasa,” akaongeza.
Hii ni baada ya Bi Shusho kutangaza kwenye mtandao wake wa kijamii kuwa binti yake amefanya harusi ya faragha.
“Dada Ode Mrs Willy. Maneno kwishaaaaa. My firstborn got married in an exclusive private ceremony. From today, call me mama mkwe. I Thank God for His faithfulness,” akaandika.
Harusi hiyo kulingana na Bi Shusho ilihudhuriwa na watu wachache mno.
“Tulifanya hivyo mradi tu kuwapa hao wawili (binti yangu na mumewe) kuwa na picha za kumbukumbu. Ilikuwa pia namna ya kuwapongeza na kuwaambia wamefanya jambo la maana sana,” akaongeza.
Bi Shusho ni mama wa watoto watatu na mara nyingi hapendi kuyaanika mambo yake ya kibinafsi mitandaoni.
Alivuma sana nchini Kenya baada ya kufyatua vibao vyake vya ‘Shusha Nyavu’ na ‘Zakayo’.
KANISA la Kikatoliki eneo la Mai Mahiu, limeorodheshwa kuwa ndogo zaidi Barani Afrika kutokana na viti vya mbao vilivyotengwa ambavyo huchukua idadi ya watu 12 pekee.
Kanisa hilo lililojengwa kando ya barabara ya Mai Mahiu-Naivasha, pia linafahamika kama Travelers Chapel, kwa kuwa kivutio kwa watalii.
Bw James Kuria, 68, mwenyeji wa eneo hilo, alisema wasafiri wanaotoka au kuingia mjini Nairobi wanaotumia barabara kuu ya Mai Mahiu-Naivasha, hupitia humo.
“Ni kivutio kwa wasafiri. Wengi hutumia sehemu hii kupiga picha za kibiashara na pia kufanya sherehe za harusi,” akasema Bw Kuria.
Watalii hao wakiwapa ufahamu ukubwa wa kanisa hilo.
“Tulijua ukubwa kutokana na viti tu, hadi pale mmoja wa wajenzi kutoka Nairobi alipima na kutueleza ukubwa wa kanisa hili ni futi 15 kwa 8,” akafafanua.
Kulingana naye, kanisa hilo lilijengwa wakati wa Vita vya Pili vya Dunia mwaka wa 1942 na Waitaliano waliokuwa chini ya ukoloni wa Uingereza.
“Kuna mwanamke mmoja wa Kiitaliano ambaye alichangia pakubwa kuchora hii barabara kuu ya Mai Mahui-Naivasha. Alipigwa risasi hadi kufa. Waitaliano hao walitaka sehemu hii kutambuliwa kwa kujenga kanisa hili,” akasema Bw Kuria.
“Vifaa ambavyo vilitumiwa vilikuwa vyenye ubora mzuri. Ndio sababu jengo hili lipo imara na litazidi kuwa vivyo hivyo,” akaongeza Bw Kuria.

Kuria alisema michoro ya kidini nje ya kanisa hilo iliashiria Baba katika Utatu, kando na waumini wengine, Wakatoliki wakimiminika zaidi.
“Utatu huo ni Baba, Mwana na Roho Mtakatifu. Wakati mwingine utapata wale Wakatoliki wenyewe wakiingia hapa na kufanya maombi.”
Hata hivyo, Waitaliano hufanya mkutano wao mara moja kwa mwaka. Hii ni baada ya waliojenga kurejea sehemu hiyo mwaka 1985 na kuweka viti vya idadi ya watu 12 ambavyo pia huashiria wanafunzi wa Yesu.
“Kabla ya miaka ya 1985 hakukuwa na viti. Wale ambao walifika sehemu hii, walilazimika kubeba viti vyao. Lakini baada ya Waitaliano hao kurudi 1985, waliweka viti hivyo,” akakamilisha.
Kando na Wakatoliki, sehemu hiyo ambayo ni ya kuabudiwa inaruhusu waumini wengine kuitumia.

WAZIRI mteule wa Hazina ya Kitaifa, John Mbadi, amekiri kuwa chama tawala cha United Democratic Alliance (UDA) na kile cha upinzani Orange Democratic Movement (ODM) havina tofauti kifalsafa.
Bw Mbadi alisema haya Jumamosi alipokuwa akihojiwa na Kamati ya Bunge kuhusu Uteuzi katika Bunge la Kitaifa baada ya kuteuliwa Waziri wa Fedha.
“Falsafa za vyama vya UDA na ODM hazina tofauti sababu zinaangazia demokrasia ya kijamii. Vyama hivi vinashughulikia ajira, gharama ya maisha, kilimo na uchumi wa majini,” alisema Bw Mbadi akijibu swali la mwanakamati Junet Mohamed, Mbunge wa Suna Mashariki.
Alifunguka kuwa alitarajiwa kuulizwa swali hili lakini hakutarajia litoke kwa mbunge wa upande wa Upinzani (ODM).
“Nilijua swali hili litaulizwa lakini si na Junet,” alikiri na kuzua kicheko ukumbini.
Kabka ya kuteuliwa kwake, Bw Mbadi alikuwa mkosoaji mkali wa Serikali ya Kenya Kwanza hasa kuhusu jinsi ilivyokuwa ikishughulikia suala la msukosuko wa uchumi nchini.

WAZIRI mteule wa Maji, Usafi na Unyunyiziaji Eric Muriithi Muuga amefichua kuwa thamani ya mali yake ni Sh31 milioni japo hamiliki gari.
Mhandisi Muuga jana alielezea wanachama wa Kamati ya Bunge kuhusu Uteuzi kuwa, mali yake inayotokana na kilimo cha majani chai, kahawa, ndizi na miraa, eneo bunge la Igembe Kusini, kaunti ya Meru alikozaliwa.
Mwenyekiti wa kamati hiyo Spika Moses Wetang’ula alipotaka kufahamu sababu ya yeye kutomiliki gari ilhali thamani ya mali yake ni Sh31 milioni, Muuga alijibu hivi: “Niliamua kuwekeza katika kilimo badala ya gari.”
Kufikia sasa, Waziri mteule ndiye mwenye kiwango cha chini zaidi cha utajiri miongoni mwa wanane ambao wamepigwa msasa na kamati hiyo kufikia sasa.
Muuga, 32, ndiye waziri mteule mwenye umri mdogo zaidi miongoni mwa wenzake watu 21 waliopendekezwa na Rais William Ruto kushikilia nyadhifa mbalimbali.

AFISI ya kiongozi wa ODM Raila Odinga iliyoko Capitol Hill Square, imegeuka kuwa ikulu ndogo ya aina yake huku ikitembelewa na watu mashuhuri wakiwemo maafisa wa serikali, wiki moja baada ya washirika wake kuteuliwa mawaziri.
Sawa na ilivyokuwa alipozika tofauti zake na Rais Uhuru Kenyatta 2018, Bw Odinga amekuwa akipokea watu mashuhuri baada ya ukuruba wake wa kisiasa na Rais William Ruto.
Jana, alitembelewa na Katibu wa Wizara ya Fedha Chris Kiptoo katika Capitol Hill, jambo ambalo lilikuwa mwiko kabla ya ukuruba wake na Rais Ruto.
Picha zake na Bw Kiptoo zilisambazwa mtandaoni na kuashiria mwamko mpya kati yake na serikali. Isitoshe, naibu wa balozi wa Kenya Ujerumani Valerie Rugene pia alimtembelea afisini mwake.
“Waziri wa Fedha Chris Kiptoo alinitembelea katika Capitol Hill Square. Tulijadili masuala makuu yanayoathiri uchumi,” Bw Odinga alichapisha katika mitandao yake ya kijamii jana.
Taifa Leo imefahamu kuwa, Bw Odinga, baada ya washirika wake kuteuliwa Mawaziri, anaweza pia kutengewa nafasi kadhaa za makatibu na tayari washirika wake wameanza kung’ang’ania nyadhifa hizo.
Mbali na Capitol Hill Square, nyumbani kwake Karen kumekuwa na shughuli nyingi kuliko kawaida huku watu wakijipanga na hali yake mpya.

Wasaidizi wake walitueleza kwamba, yanayoendelea ofisini na nyumbani kwake ni sawa na alipokuwa Waziri Mkuu.
Bw Odinga anashikilia kuwa hayumo serikalini. Hata wakati wa Handisheki 2018 hadi 2022, alisisitiza hakuwa sehemu ya serikali ya Rais Uhuru Kenyatta. Hata hivyo, yanayoshuhudiwa ni tofauti. Kupitia yanayonaswa kwenye kamera ndani ya ofisi yake, ni wazi kuwa ana ushawishi mkubwa.
Huku kukiwa na mzozo kati ya Dkt Ruto na naibu wake, Rigathi Gachagua, inachukuliwa kwamba mtu yeyote sasa yuko salama zaidi anapoonekana kujitambulisha na Bw Odinga.
Kwa hivyo, ni dhahiri kwamba ikiwa Ikulu ni jengo lililo Mlimani, basi Capitol Hill ndio njia ya kuekelea Ikulu, ikiwa sio ikulu mbadala.
Ni kisa cha historia kujirudia. Baadhi ya picha za Bw Odinga akiwa ndani ya Capitol Hill wakati wa handisheki ni pamoja na akiwa na Alfred Mutua (Julai 2019), Mike Sonko (Aprili 2018), Anne Waiguru (Desemba 2019), Joshua Kutuny na Zedekiah Kiprop (Septemba 2020), Peter Munya na Anyang’ Nyong’o (Agosti 2019), Charity Ngilu (Aprili 2019), Alex Tolgos (Agosti 2020), Nancy Macharia (Januari 2019), Robert Godec (Juni 2018), Joe Nyagah (Novemba 2018), Hassan Joho na Amason Kingi (Machi 2019), miongoni mwa wengine.
Kutokana na maoni yaliyotolewa kwenye mitandao ya kijamii, Capitol Hill Square inaweza pia kuwa mashine ya kutakasa walio na doa, ambapo watu wanaoandamwa na ufisadi hujitokeza na ghafla wanaacha kukashifiwa na upinzani.

Maoni ya Wakenya kwenye X, kwa picha ya Bw Odinga akitangaza ziara ya Dkt Kiptoo yanaonyesha jinsi Wakenya wanavyochukulia ziara kama hizo.
“Sanitaiza!” aliandika Cornelius Ronoh.
Kelvin Kiptoo aliuliza: “Je, serikali ya upinzani au upinzani uko serikalini?”
“Maafisa wa serikali sasa wanaripoti Capitol Hill kwa kushauriwa na Raila kuhusu jinsi ya kusimamia uchumi,” aliandika Mallo Fredrick.
- gachagua
- Maandamano ya Gen Z
- raila
- ruto
- uteuzi
- Makubaliano ya kukiri mashtaka ya watuhumiwa wa shambulio la 9/11 yabatilishwa
CHANZO CHA PICHA,GETTY IMAGES
- Waziri wa Ulinzi wa Marekani, Lloyd Austin amebatilisha makubaliano ya kukiri mashtaka nje ya mahakama yaliyofikiwa na maofisa wa wizara hiyo pamoja na watuhumiwa wa shambulio la kigaidi la Septemba 11, 2001.Kupitia taarifa aliyoitoa jana Ijumaa, Bw Austin amesema pia kuwa ametengua mamlaka ya ofisa anayesimamia mahakama za kijeshi ambaye alisaini makubaliano hayo siku ya Jumatano.Makubaliano hayo, ambayo yanaripotiwa kuwa yalikuwa yanawakinga watuhumiwa hao na adhabu ya kifo, yalipingwa vikali na baadhi ya familia za waathirika wa shambulio hilo.Taarifa ya Waziri huyo imewataja washtakiwa watano ambao wote wanashikiliwa kwenye jela ya kijeshi ya Guantanamo, ikiwemo anayetuhumiwa kusuka mpango wa mashambulizi, Khalid Sheikh Mohammed. Makubaliano yenyewe yalihusisha watuhumiwa watatu tu.“Nimeamua kwamba, kwa kuzingatia uzito wa kuingia kwenye makubaliano ya nje ya mahakama na washtakiwa…Wajibu wa kufanya jambo hilo inabidi uwe wangu kama mtu mwenye mamlaka ya juu (katika wizara ya ulinzi),” Bw Lloyd alimuandikia Brigedia Jenerali Susan Escallier, ambaye ni kiongozi wa kamisheni inayosimamia mahakama za kijeshi huko Guantanamo.”Hivyo basi, natengua mamalaka yako. Na kuanzia sasa, kama sehemu ya kutekeleza mamlaka niliyonayo, ninafuta makubaliano yote matatu ya nje ya mahakama.”Ikulu ya White House ilijitenga na kuhusika kwa namna yeyote katika kufikiwa kwa makubaliano hayo siku ya Jumatano.Watuhumiwa hao watano waliotajwa kwenye taarifa ya Bw Austin ni: Khalid Sheikh Mohammed, Walid Muhammad Salih Mubarak bin Attash, Mustafa Ahmed Adam al-Hawsawi; na wawili ambao hawakutajwa kwenye makubaliano ya Jumatano ni: Ramzi bin al-Shibh na Ali Abdul Aziz Ali.Wanaume hao wamekuwa kizuizini bila kufunguliwa mashtaka kwa zaidi ya miongo miwili sasa. Moja ya sababu zinazotia ugumu wa kufunguliwa mashtaka rasmi ni tuhuma za matumizi ya mateso makali katika kuwahoji na kusaka ushahidi.Kwa pamoja wanatuhumiwa kukeleza msururu wa makosa ya jinai, ikiwemo kushambulia raia, mauji ya kinyume cha sheria za vita, utekaji nyara na ugaidi.Wanasiasa kadhaa kutoka chama cha Republican ambao walipinga makubaliano ya Jumatano wamempongeza Waziri Austin kwa kuyabatilisha.Soma zaidi:Watatu wanaotuhumiwa kupanga njama ya 9/11 wafikia makubaliano ya kukiri mashtaka – PentagonShambulio la Septemba 11:Fahamu sababu za kisayansi zilizosababisha kuanguka kwa ‘Twin Towers’Shambulio la Septemba 11: Yafahamu Matukio matano yaliyoitikisa MarekaniMashambulio ya Septemba 11: Hiki ndicho kilichotokea dakika baada ya nyingine siku hiyoShambulio la Septemba 11: Milima ya ajabu iliyomficha Osama Bin Laden dhidi ya Marekani
- 2024Vita vya Ukraine: Mashambulizi ya Urusi yakaribia kilele chake mashariki mwa Ukraine
CHANZO CHA PICHA,REUTERS. Maelezo ya picha,Mwanajeshi wa Ukraine akiwa katika eneo la mapigano karibu na Chasovoy YarMashambulizi ya Urusi, ambayo yamekuwa yakiendelea kwa karibu miezi 10 na kuongezeka mwishoni mwa majira ya masika na kiangazi yanafikia kilele chake.Mwishoni mwa Julai, vikosi vya Urusi viliweza kuongeza kasi ya mashambulizi katika mwelekeo muhimu – kuelekea Pokrovsk. Ili kumzuia adui, na kuilazimisha Ukraine kuhamisha hifadhi na vifaa vifaa.Lakini hali hii inadhoofisha ulinzi katika maeneo mengine yaliyo hatarini – kwa hivyo, katika miezi miwili ya majira ya kiangazi, Warusi walipata mafanikio ya mbinu katika mwelekeo wa Toretsk, Chasovoy Yar, na walifanikiwa pia kusonga mbele karibu na Krasnohorivka na Vugledar.Katika Mkoa wa Kharkiv, wanajeshi wa Urusi waliviteka vikosi vya Ukraine karibu na Liptsi na Vovchansk, na pia wameshambulia katika maeneo ya Mto Oskil karibu na Kupyansk. Hapa kulikuwa na tisho la kukatwa kwa daraja la Ukraine lililopo kwenye ukingo wa mashariki.Jeshi la Urusi karibu lilikaribia maeneo muhimu ya kimkakati ya Jeshi la Ukraine mashariki mwa Ukraine.Lakini swali linabaki ni iwapo litakuwa na nguvu za kutosha hadi shambulio la mwisho?.Unaweza pia kusoma:YA MSINGI:Mzozo wa Ukraine: Kwanini Urusi inaivamia Ukraine na Putin anataka nini?UFAFANUZI:Mzozo wa Ukraine: Swift ni nini na kwa nini kuipiga marufuku Urusi ni muhimu sana?UCHAMBUZI:Mzozo wa Ukraine: Putin humsikiliza nani?KWENYE RAMANI:Uvamizi wa Ukraine: Shambulio la Urusi kwenye ramaniZELENSKY:Volodymyr Zelensky: Mfahamu rais wa Ukraine aliyeacha umaarufu wake wa TV na kuingia kwenye siasaPUTIN:Vladimir Putin: Rais wa Urusi aliyeagiza shambulio Ukraine
KIPENGA CHA MICHEZO
- Mashindano ya Olimpiki 2024: Joshua Cheptegei wa Uganda ajishindia medali ya dhahabu
Joshua Cheptegei wa Uganda ameshinda mbio za mita 10,000 kwa wanaume – medali ya kwanza kupatikana katika riadha na kuipatia Afrika dhahabu yake ya pili katika mashindano ya Olimpiki ya Paris, 2024.Cheptegei, mshikilizi wa rekodi ya dunia wa Uganda, alitoka mbio za kufa mtu katika raundi ya mwisho na kuweka rekodi mpya ya saa 26:43.14 akitia kibindoni medali ya dhahabu ya kwanza uwanjani Stade de France.Mwanariadha huyo mwenye umri wa miaka 27, na bingwa wa dunia mara tatu, alimaliza mbele ya Berihu Aregawi wa Ethiopia na mshindi wa medali ya shaba Grant Fisher, wa Marekani.Pia unaweza kusoma:Jedwali la medali ya mashindano ya Olimpiki ya Paris 2024




- Thierry Ndikumwenayo ambaye amezaliwa Burundi, ameiwakilisha Uhispania kwenye mbio za mita 10,000 Olimpiki, Paris, Ufaransa.
- Ndikumwenayo ambaye anashiriki michezo ya Olimpiki kwa mara yake ya kwanza, alimaliza katika nafasi ya 9 kwenye mbio za mita 10,000.
- Mwanariadha kutoka Uganda Joshua Cheptegei amemaliza wa kwanza na kushinda medali ya dhahabu katika mbio ya mita 10,000 upande wa wanaume.
- Aidha, ameweka rekodi mpya ya Olimpiki ya muda wa 26:43:14 katika mbio hizo huku pia akiibuka kuwa mwanariadha wa Uganda mwenye medali nyingi za Olimpiki baada ya ushindi katika mbio za Mita 5,000 na Mita 10,000, mashindano ya Tokyo 2020 na mbio za Mita 10,000 leo hii, Paris 2024.


- Malkia wa riadha kutoka Kenya, Faith Kipyegon, na Beatrice Chebet wamefuzu katika fainali za mbio za mita 5000 kwenye Olimpiki, nchini Ufaransa.
- Chebet ambaye alivunja rekodi ya dunia ya mita 10,000 kabla ya kushinda mbio za mita 5000 mjini Doha nchini Qatar, amefuzu pamoja na Faith Kipyegon, ambaye anashikilia rekodi ya dunia ya mbio za mita 1500, na mita 5000.
- Kwa sasa matumaini ya Wakenya yako kwa mabingwa hao wawili wanaotarajiwa kuwaletea dhahabu watakapoingia uwanjani tarehe 5 Agosti kwenye fainali za mita 5000.
- Kamala Harris achaguliwa rasmi kuwa mgombea wa chama cha Democratic
CHANZO CHA PICHA,GETTY IMAGES - Makamu wa Rais wa Marekani Kamala Harris amepita idadi inayohitajika kushinda uteuzi wa kugombea tiketi ya urais kupitia chama chama cha Democratic katika kura ya wajumbe wa chama.Akiongea kwa njia ya simu, Bi Harris alisema “naichukulia kwa heshima kubwa nafasi ya uwezekano wa kuwa mteule” kabla ya Kongamano la Kitaifa la chama cha Democratic litakalofanyika huko Chicago baadaye mwezi huu.Bi Harris ndiye mwanamke wa kwanza Mwafrika na mwanamke wa kwanza kutoka Asia Kusini kupeperusha bendera ya kuelekea Ikulu ya White House katika chama kikuu cha kisiasa cha Marekani.Ikiwa atamshinda Donald Trump, mgombea wa chama cha Republican katika uchaguzi wa mwezi Novemba, atakuwa rais wa kwanza mwanamke Marekani.Alichaguliwa bila kupingwa katika uchaguzi huo baada ya Rais Joe Biden kujiondoa mwezi uliopita na kumuunga mkono kuwania nafasi hiyo.Washindani wake kadhaa walifuata mkondo wake.Siku ya Ijumaa alasiri, Bi Harris akawa mgombea rasmi baada ya kupata uungwaji mkono kutoka kwa wajumbe 2,350, idadi inayohitajika kuteuliwa.Soma zaidi:‘Je, ni Mwafrika au Mhindi?’: Trump ahoji utambulisho wa rangi wa HarrisJe, Kamala Harris ana uwezo na sifa za kumshinda Trump?Njia tatu ambazo Trump anazitumia ‘kumzima’ Kamala Harris
- Kombe la Dunia 2034: Saudia yapanga kujenga uwanja wa mita 350 juu ya ardhi
CHANZO CHA PICHA,SAUDI 2034 - Maelezo ya picha,Taswira ya Uwanja wa Neom unaopendekezwaSaudi Arabia imewasilisha mipango ya kujenga viwanja 11 – ikiwa ni pamoja na uwanja mmoja wa mita 350 kutoka usawa wa ardhi, kama sehemu ya jitihada za nchi hiyo kuandaa Kombe la Dunia la 2034.Uwanja unaopendekezwa kujengwa katika eneo la Neom, jiji ambalo bado halijajengwa kaskazini-magharibi mwa nchi, utaweza kufikiwa tu kupitia lifti za mwendo wa kasi na magari yasiyo na dereva.Uwanja huo, ambao ni sehemu ya mradi wa nchi hiyo wa ‘The Line’ wa kuleta mseto wa uchumi wa ufalme huo mbali na mafuta, unatarajiwa kuandaa mechi ya robo fainali.Nia ya Saudi Arabia haijapata pingamizi na nchi hiyo ina muda hadi tarehe ya mwisho ya Oktoba kuwasilisha mipango yake.Kati ya viwanja 11 vipya, vinane vitakuwa katika mji mkuu Riyadh – ikiwa ni pamoja na Uwanja wa Kimataifa wa King Salman wenye uwezo wa kuwapokea watu 92,760, ambapo mechi za ufunguzi na fainali zitachezwa.
CHANZO CHA PICHA,SAUDI 2034 Maelezo ya picha,Uwanja wa Prince Mohammed bin Salman utajengwa juu ya mwamba, takriban mita 200 kutoka ardhini.Miji ya Jeddah, Al Khobar na Abha pia itapokea mechi za Kombe la Dunia 2034.Itakuwa mara ya kwanza kwa mashindano hayo yaliyopanuliwa kufanyika katika nchi moja tu ambapo timu 48 zitashiriki katika Kombe la Dunia la FIFA , kwa mara ya kwanza.Wenyeji wanatarajiwa kuthibitishwa rasmi na kongamano la Fifa tarehe 11 Disemba. - 1 Agosti
TETESI ZA SOKA ULAYA
Bayern Munich imekataa dau la Manchester United mara mbili kwa mlinzi wa kati wa Uholanzi Matthijs de Ligt, 24, na beki wa Morocco, Noussair Mazraoui, 26. (Telegraph – subscription required)
Newcastle wanapanga kuanzisha mazungumzo kuhusu mkataba mpya na winga wa Uingereza Anthony Gordon, 23, atakaporejea kutoka mapumzikoni baada ya mashindano ya Euro 2024. (Athletic – subscription required)

Fulham wanavutiwa na beki wa Aston Villa Mbrazil Diego Carlos, 31. (Mail)
West Ham wako katika mpango wa kumsajili kiungo wa Argentina Guido Rodriguez, 30, kama mchezaji huru baada ya kuondoka Real Betis. (Standard)
Pia unaweza kusoma:




All Rights Reserved © Cantona Group Ltd||2024
Discover more from cantonadigital
Subscribe to get the latest posts sent to your email.