AFRIKA LEO JIONI-AGOSTI 2,2024

Radio Fortune Africa

https://zeno.fm/radio/radio-fortune-africa

Habari Na Cantona Joseph

KUONDOLEWA kwa mashtaka ya ufisadi dhidi ya aliyekuwa gavana wa Kakamega Wycliffe Oparanya kumezua mzozo mpya kati ya Mkurugenzi wa Mashtaka ya Umma Renson Ingonga na Tume ya Maadili na Kupambana na Ufisadi (EACC).

Ingawa tume ya kupambana na ufisadi ilishikilia kuwa kuna ushahidi wa kutosha kuendeleza mashtaka ya mgongano wa kimaslahi na ufujaji wa pesa dhidi ya Bw Oparanya, Bw Ingonga alikuwa na maoni kwamba ingekuwa vigumu kumpata na hatia katika kesi hiyo kwa kukosa ushahidi wa kutosha.

Tume ya EACC ilishikilia katika barua iliyomwandikia Bw Ingonga mnamo Julai 31 kwamba stakabadhi na ushahidi uliowasilishwa kwake unaonyesha kuwa pesa zinazodaiwa kutumwa kwa akaunti ya kibinafsi ya Bw Oparanya na kwa mawakili wake zilikuwa ni ufisadi kutoka kwa wanakandarasi waliopewa zabuni mbalimbali na serikali ya Kaunti ya Kakamega.

“Kulikuwa na kesi ya wazi ya ulanguzi wa fedha na mgongano wa maslahi ambayo washukiwa hawawezi kutoa utetezi wowote dhidi yao. Kwa hivyo, tume inaamini kwamba ushahidi uliopatikana na uliowasilishwa kwa afisi yako unatosha na unaweza kuthibitisha kesi bila shaka yoyote,” barua ya Twalib Mbarak, Afisa Mkuu mtendaji wa EACC ilisema.

Bw Oparanya alitakiwa kushtakiwa kwa makosa 11 yanayohusiana na ufisadi kutokana na zabuni zilizotolewa kwa kampuni mbalimbali akiwa mkuu wa kaunti ya Kakamega.

Alipaswa kushtakiwa kwa mgongano wa maslahi na kupokea faida, kwa kununua mali anayomiliki.

EACC ilisema uchunguzi ulibaini kuwa Bw Oparanya alidaiwa kupokea kimakosa Sh56.7 milioni kutoka kwa serikali ya kaunti ya Kakamega.

Awali Mkurugenzi wa Mashtaka ya Umma alikubaliana na mapendekezo ya EACC ya kumshtaki Bw Oparanya lakini akafanya mabadiliko mnamo Julai, kufuatia ombi la Bw Oparanya kupitia kwa mawakili wake.

Hali ilizidi kuwa mbaya baada ya EACC kuliandikia Bunge kuhusu hali ya kesi hiyo huku wakili wa Bw Oparanya akisema barua ilikuwa na nia mbaya.

Bw Oparanya ni miongoni mwa mawaziri wateule ambao wanapigwa msasa kuhusu ufaafu wao kuhudumu serikalini na maswali kuhusu ufisadi yanatarajiwa kuibuliwa atakapofika mbele ya kamati ya Bunge Jumapili.

Wakili wa Bw Oparanya Dkt Ken Nyaundi alisema kwamba walimwandikia DPP mnamo Julai 24, 2024 wakimuomba apitie uamuzi wa kumshtaki baada ya kupata ushahidi mpya, kuonyesha kwamba pesa zinazodaiwa kulipwa kwa akaunti ya Bw Oparanya zilikuwa za mkopo.

Dkt Nyandi alisema EACC ilipokea mawasiliano kutoka kwa DPP na uamuzi wa kutupilia mbali uamuzi wa kumfungulia mashtaka Bw Oparanya, EACC iliandikia Bunge ikipuuza mawasiliano muhimu ambayo yalitangulia barua yao.

“Hakuwezi kuwa na chuki kubwa zaidi kuliko hii,” Dkt Nyaundi alisema.

Aliongeza, “Tunaagizwa kuwajulisha kuwa hakuna upelelezi wala mashtaka yanayomkabili Bw Oparanya kustahili malalamishi dhidi yake.”

Inafaa kukumbuka kuwa kwa msingi wa barua ya DPP na baada ya kupokea barua hiyo hiyo, EACC inafaa kutambua kwamba madai yote ya makosa kutoka kwa Bw Oparanya yalikataliwa.

Kwa kukubaliana na Bw Oparanya, DPP alibainisha kuwa pesa hizo ni mkopo.

Mashtaka yaliyopendekezwa yalitokana na pesa alizolipwa na Mkurugenzi wa Sabema International Ltd na Sesela Resources Ltd, Joseph Obulunji Okutoyi kwa kampuni ya Marende & Nyaundi Company Advocates ili kumwezesha gavana huyo wa zamani kununua nyumba huko Karen.

Sesela Resources Ltd ilishirikiana na serikali ya kaunti ya Kakamega kwa ujenzi wa Barabara ya Tsalwa Junction-Ombwaro-Manyulia kwa gharama ya Sh216 milioni.

Baada ya kulipwa Sh35.8 milioni, mwanakandarasi alihamisha Sh10 milioni kwa mawakili wa Oparanya.

dpp
eacc
Msasa wa Mawaziri
oparanya
ruto
uteuzi

MBUNGE wa Nyeri Mjini Duncan Maina Mathenge ambaye mwezi mmoja uliopita,  alisimama kwa hoja bungeni akisema alikuwa akimpinga Naibu Rais, Rigathi Gachagua kwa niaba ya wabunge wenzake sita waliochaguliwa katika Kaunti ya Nyeri, amejipata akipiga abautani.

Mbunge huyo alianzisha moja ya mashambulizi makali dhidi ya Naibu Rais kufikia sasa wakati huu wa mazingira magumu ya kisiasa nchini.

“Hotuba yangu hapa pia inawakilisha hisia za Seneta (Kimani Wamatinga) na Mwakilishi wa Kike (Rahab Mukami). Kwa kweli tumeteswa na vitisho na usaliti. Na ni muhimu kama viongozi waliochaguliwa tupewe nafasi ya kutekeleza jukumu ambalo watu wa kawaida wa Nyeri walitupa walipotupigia kura. Haiwezekani kwamba watu wa Nyeri walitupigia kura ili tuweze kumfuata mtu binafsi kote, wakati mtu huyo anaenda kucheza, kunywa Muratina na kula nyama choma. Haiwezekani. Tunataka kuzungumza kutoka  hapa ndani ya bunge hili na kufahamisha nchi kwamba heshima ni pande mbili. Hauwezi kutudharau katika maeneo bunge mengine na kutarajia tudumishe heshima ambayo tumekupa kwa miaka miwili iliyopita. Heshima hailazimishwi,” alilipuka na ikabidi atulizwe na Spika Moses Wetang’ula.

Mnamo Julai 31, 2024, Bw Mathenge alikutana na Bw Gachagua wakati wa hafla ya mazishi  ya mwanachama wa Baraza la Agikuyu, Bw Charles Kariuki Kabui na akiwa mwenyeji, hangeweza kutoroka kukutana ana kwa ana na Bw Gachagua kabla ya kutangaza kuwa alijutia matamshi yake ya awali.

Alikuwa amepingwa na spika wa Nyeri, Bw James Gichuhi Mwangi aliyemtaka atangaze hadharani ni kwa nini anapigana na Naibu wa Rais na kama alikuwa mmoja wa wanaounda njama ya kumtimua  ‘mwana wetu kutoka Rware’( mamlakani)’.

Akijitenga na tetesi za kumtimua Bw Gachagua ofisini, Bw Mathenge alisema hajui ni wapi mikutano ya kupanga mpango huo inafanyika.

“Sitaki kuhusishwa na siasa za ulaghai, unafiki na uongo. Naibu wa Rais anajua kuhusu heshima yangu kubwa kwake. Anafahamu kazi nyingi ambazo tumetekeleza pamoja bungeni. Alinipa nafasi ya kuwa mwenyekiti katika jopokazi la bunge  kuhusu mageuzi  ya kahawa. Nimejitolea kuhakikisha  nitamtuza kwa kupitisha sheria za kusaidia wakulima wetu,” alijitetea.

Alisema: “Pia ningependa kunyenyekeza na kwa dhati  naomba msamaha kwa matamshi yangu ya awali. Kulikuwa na kisa cha hivi majuzi ambapo mnamo Mei 19, 2024 Mheshimiwa alikuwa katika hafla ya kanisa katika eneo la Endarasha huko Nyeri na sikufika. Haikuwa makusudi kwani nilikuwa na harambee iliyopangwa awali katika eneo bunge langu na nisingeweza kuwaacha wageni wangu.Kama nilikukosea Bw Naibu Rais kwa kutokuwepo, samahani tena kwa dhati. Iwapo nitakutana na mchakato wa kukutimua, nitasimama kama mtu aliyejiweka hatarini kukutetea. Siku zote nimekuwa nikisisitiza hadharani na faraghani kwamba Bw Gachagua ndiye mfalme wa Mlima Kenya.”

Bw Gachagua aliposimama kuongea, alisikitika kwamba,  “kuna watu wachache ambao wamepotoshwa na maadui wa Mlima Kenya na wanatekeleza mipango iliyofadhiliwa ya kugawanya eneo hilo la Mlimani.”

Habari za Kitaifa Zaidi Nchini Kenya

MBUNGE wa Kapseret, Oscar Sudi amezua mjadala kwenye mitandao tofauti ya kijamii, baada ya kuonyesha saa yake ya mkono yenye thamani ya Sh17 milioni.

Saa hiyo ya kifahari ya Ulysse Nardin Freak Phantom, imezua mjadala mtandaoni, huku wakosoaji wakimshutumu mbunge huyo wakisema hana huruma akitembea na saa kama hiyo ilhali Wakenya wanalala njaa.

Bw Sudi alifichua kuwa saa hiyo ilikuwa zawadi kutoka kwa waziri mkuu wa zamani wa nchi nyingine.

“Nilikuwa na saa kama hizi mbili lakini hata sijui gharama yake kamili,” Bw Sudi alimwambia Oga Obinna wakati wa mahojiano.

Katika mahojiano hayo hayo, Bw Sudi alizungumzia maisha ya kifahari ya aliyekuwa Waziri wa Uchukuzi, Bw Kipchumba Murkomen.

Alisema Bw Murkomen, ambaye amewahi kuwa mhadhiri, seneta, na sasa waziri, awali alitajwa kumiliki saa yenye thamani ya Sh900,000, ufichuzi uliozua mjadala kwenye mitandao ya kijamii.

“Murkomen amekuwa mhadhiri, seneta kwa mihula miwili, na waziri kwa miaka miwili, na alisema saa yake ina thamani ya Sh900,000. Kweli, Sh900,000 ni nini?” Bw Sudi alisema.

“Wakati mwingine Wakenya wanakosea. Saa kama hii haikutengenezewa miti au ng’ombe kuvaa; ilitengenezwa kwa ajili ya binadamu. Unataka nani avae saa kama hii? Tuache wivu,” akasema akitetea mtindo wake wa maisha.

Maoni ya Sudi yamezua hisia tofauti mtandaoni huku baadhi ya watu wakimtetea mbunge huyo wakisema kuwa utajiri wake na maisha yake ya kifahari yanatokana na bidii yake kwenye biashara.

  • WAZIRI mteule katika Wizara ya Kilimo na Mifugo Daktari Mwihia Karanja, alikana kufanya kazi kama msaidizi wa Waziri wa zamani Bw Mithika Linturi.Madai hayo yalisambaa kwenye mitandao ya kijamii Julai 19, 2024 punde tu alipotangazwa na Rais William Ruto kuchukua nafasi ya kuwa Waziri wa Kilimo.Akiwa mbele ya Kamati Maalum kwa mahojiano Ijumaa, Agosti 2, 2024, Bw Karanja, alieleza kushangazwa na madai hayo.Alisisistiza kibinafsi au kitaaluma hajawahi hata kukutana na waziri huyo wa zamani.Hii ni baada ya Kiongozi wa Wengi kwenye Bunge la Kitaifa na Mbunge wa Kikuyu Kimani Ichung’wah kumtaka kufafanua zaidi mahusiano yake na waziri wa zamani kwenye wizara hiyo.“Kuwa msaidizi wake, hilo lilinishangaza sana. Nikiwa mbele ya Kamati hii, sijawahi kukutana na waziri huyo na sijawahi kuwa msaidizi wake wa kibinafsi,” akasema Dkt Karanja.Kwenye mahojiano hayo, suala la ufisadi lilijitokeza huku Mbunge wa Suna Mashariki akimuonya huenda akafutwa kazi baada ya mwaka mmoja kutokana na ufisadi uliokithiri kwenye Wizara hiyo kutokana na wafanyabiashara wafisadi.Mbunge huyo alisema wafisadi hao wamezingira afisi za serikali na kutekeleza uhalifu bila kuchukuliwa hatua.Bw Junet alimuonya Daktari Karanja, iwapo hatakuwa mwangalifu na kukosa kuchukua hatua kwa wafisadi hao, basi huenda wembe uliompata Waziri wa zamani Mithika Linturi utamkata.Kwa upande wake Daktari Karanja alihakikishia mbunge huyo na Wakenya, iwapo ataidhinishwa na kamati hiyo kwenye wadhifa huo, basi atafanya kwa juhudi zake kuwaondoa wafanyabiashara hao.“Najua suala la wafanyabiashara wafisadi ni shida kubwa na kuna njia mbalimbali nitakazotumia. Iwapo nitaidhinishwa na kamati hii, basi nawapa notisi wafisadi hao. Notisi hiyo ni kuwafahamisha kuondoka kwenye biashara hiyo, kulingana na kanuni ambazo ninaziheshimu sana, sitakubali kuhujumiwa,” alisema waziri huyo mteule.

CHAMA cha United Democratic Alliance UDA kimemfuta kazi rasmi Katibu wake mkuu Cleophas Malala baada ya mkutano wa Baraza Kuu la Kitaifa la chama hicho uliofanyika Ijumaa.Kutokana na kufutwa kazi kwa Malala, Hassan Omar Hassan ameteuliwa kuwa Kaimu Katibu Mkuu.“Uteuzi wa Mheshimiwa Cleophas Malala kuwa Katibu Mkuu wa muda umebatilishwa. Mabadiliko haya yanaanza kutekelezwa mara moja,” ilisema sehemu ya taarifa ya UDA.Haya yamejiri siku mbili baada ya sarakasi kushuhudiwa katika makao makuu ya chama cha United Democratic Alliance (UDA) Jumanne, Julai 30, 2024 baada ya baadhi ya wanachama kutaka kumwondoa Malala afisini.Wakiongozwa na wakili Joe Khalende, kundi hilo lililojiita “Waanzilishi wa UDA” lilimsuta Malala likidai anadumaza maendeleo ya chama hicho na Serikali Jumuishi iliyoundwa na kiongozi wa chama, Rais William Ruto na kiongozi wa ODM, Raila Odinga.Khalende na wenzake pia walimshutumu Bw Malala kwa kushirikiana na viongozi wa Vuguvugu la TAWE linaloongozwa na Gavana wa Trans Nzoia George Natembeya, hivyo kukiuka Katiba na mwongozo wa UDA.Akiongea na wanahabari, wakili huyo alijitangaza kuwa kaimu mpya wa Katibu Mkuu wa UDA na kwamba Malala amepigwa marufuku kuendesha majukumu yote ya afisi hiyo.“Malala ametelekeza wajibu na majukumu yake kama Katibu Mkuu wa chama chetu cha UDA. Miongoni mwa majukumu hayo ni kuwa msemaji wa chama na kuitisha mikutano yote. Yeye ameungana na wapinzani wetu. Anaunga mkono vuguvugu la TAWE na ajenda ambazo zinakinzana kabisa na za chama chetu ambacho ndicho chama tawala nchini,” Bw Khalende alisema.

MAGARI BINAFSI NCHINI KENYA NA MALORI CHANZO CHA AJALI.

RIPOTI mpya ya Mamlaka ya Kitaifa ya Usalama Barabarani (NTSA) imetupilia mbali kasumba kuwa nyingi za ajali barabarani husababishwa na magari ya abiria.

Kwa mujibu wa ripoti ya hivi punde ya NTSA, idadi kubwa ya vifo barabarani husababishwa na magari ya kibinafsi na malori.

Hii ni tofauti sana na ripoti za hapo awali ambazo zimekuwa zikionyesha kuwa maafa mengi barabarani husababishwa na magari ya abiria.

Ripoti hiyo pia inaonyesha kuwa licha ya ukweli kwamba pikipiki zilisababisha vifo vingi barabarani mwaka uliopita hadi mwezi Juni 2023 (vifo 1,157), magari ya abiria yalifuatia kwa vifo 1,086 ilhali magari ya kibinafsi yalisababisha vifo 1,078.

Magari ya serikali yalisababisha vifo 57 huku ambulensi zikisababisha vifo viwili kisha mkokoteni kifo kimoja.

Gavana wa nyeri Mutahi Kahiga apasua mbarika.

GAVANA wa Nyeri Mutahi Kahiga amedai kwamba kujificha kwa Naibu Rais Rigathi Gachagua nyumbani kwake Mathira mnamo Mei kulichangiwa na ‘mateso ya kisiasa’ kutoka kwa mrengo wa Rais.

Bw Kahiga amefichua kwamba Bw Gachagua alikuwa akiandamwa na masaibu sawa na yaliyompata Rais William Ruto alivyonyanyaswa na uongozi wa Rais Uhuru Kenyatta alipokuwa Naibu Rais.

Asema ahadi ya Rais ya kumlinda naibu wake dhidi ya kile alichokiita ‘mateso ya kisiasa’  haijatimia na akaongeza kuwa hali hii “inatufanya tushangae ni nini kimemwingia Rais ambaye tulimpigia kura 2022.”

Gavana Kahiga asema Mlima Kenya kwa sasa unajifunza mengi kwa hatua ya  kumwamini Dkt Ruto bila makubaliano ya kimaandishi kabla ya uchaguzi na kuundwa kwa serikali ya Kenya Kwanza.

“Hatukumwendea Ruto kama timu, viongozi wetu wote wakuu katika serikali yake walimwendea kibinafsi. Hatujawahi kuwa na mshikamano katika serikali hii kama Mlima Kenya,” akasema.

“Nilikuwa nimempendekezea Bw Gachagua tushinikize makubaliano ya maandishi na rais au hata tukatize ndoa yetu. Hata hivyo, alipuuzilia mbali pendekezo hilo akisema kwamba aliamini kuwa mambo yangetengenea. Alishikilia kwamba tutasalia katika chama cha Rais cha UDA,” Bw Kahiga aongeza.

Hata hivyo, gavana huyo ameonya kuwa Mlima Kenya una chaguo mbadala akisema “tuna vyama vingi vya kisiasa vya eneo la Mlima Kenya.”

“Rais anajua jinsi alivyoondoka Jubilee mbambo yalipokuwa magumu,” Bw Kahiga amekariri, akirejelea jinsi Dkt Ruto  alivyounda chama cha UDA alipokuwa akijiandaa kuondoka katika chama tawala cha Jubilee kabla ya uchaguzi wa 2022.

Uungwaji mkubwa wa Gachagua Mlimani

Amedai kuwa Gachagua anaungwa mkono na magavana wote wa Mlima Kenya “na ninazungumza kama mwenyekiti wao katika kaunti zote 10.”

Gavana huyo alisema dhuluma za kisiasa  kutoka kwa washirika wa Rais  zilimwathiri Gachagua hadi akalazimika kujificha  ili apate muda wa kutafakari.

“Naibu Rais alitoweka ghafla na hakuna aliyejua alikokuwa. Ilikuwa hali ya kutisha kwani hata hakupokea simu. Binafsi niliongoza juhudi za kumtafuta kwani mambo yaliyokuwa yakimwandama yalikuwa hatari. Baadhi ya viongozi wetu wa serikali walikuwa wameanza kumdharau. Alikuwa akinyimwa usafiri wa ndege za kijeshi, kulikuwa na njama zilizomzunguka na kutoweka kwake kusingechukuliwa kwa urahisi,” alisema.

Mnamo Mei 21 Gachagua alijitokeza baada ya wiki moja ya kutoonekana hadharani na kutangaza kwamba alikuwa ameingia katika msitu wa Mlima Kenya kufunga na kusali.

Gavana wa Nyeri Mutahi Kahiga akihutubu mwezi uliopita katika hafya iliyowaleta pamoja wafanyakazi wa kaunti hiyo. Mutahi ni mwendani mkuu wa Naibu Rais. Picha|Joseph Kanyi

Jana, Bw Kahiga alisema alipompata nyumbani kwake Mathira, Naibu Rais alikuwa “katika hali ya kutafakari”.

Alidai kuwa kumpata Bw Gachagua hakukuwa rahisi “kwani ilinilazimu kupitia mtandao wa wasaidizi wake ambao ni pamoja na maafisa wa usalama na familia.”

Alipofika nyumbani kwa Gachagua, gavana asema, alipata “mtu aliyefadhaika, akiwa peke yake nyumbani na katika mazungumzo yetu yaliyofuata, nilitambua uzito wa hali aliyopitia.”

Bw Kahiga asema alizungumza na Rais kibinafsi kuhusu masuala hayo.

Alidai mateso hayo yameongezeka hadi kufikia hatua kwamba “Huduma ya Kitaifa ya Ujasusi (NIS) inaonekana wazi kuendeleza kisasi dhidi ya Naibu Rais.”

Alikiri kwamba kuna njama ya kumuondoa Gachagua mamlakani

Bw Kahiga alidai njama hizo zinasukwa kwa kisingizio kwamba alihusika na ghasia ambazo zimekumba mji wa Karatina kwa muda wa mwezi mmoja uliopita.

Bw Kahiga amemkosoa mbunge wa Laikipia Mashariki Mwangi Kiunjuri kuhusu matamshi yake kuhusu wanasiasa wanaofadhili waandamanaji.

“Ninataka Kiunjuri aeleze vifaa halisi vilivyosafirisha wahuni 25,000 hadi Nairobi kutoka Mlima Kenya na pia ataje jinsi idadi hiyo inaweza kusafirishwa na kwa malori mangapi,” alisema.

HABARI ZINAZOTOKEA MASHARIKI YA KATI

IKIWA umeshtuliwa na hatua ya Israeli kumuua kiongozi mkuu wa kisiasa wa kundi la Hamas, Ismail Haniyeh, basi jua kwamba huelewi kwamba taifa hilo la Kiyahudi linaongozwa na mtu wa aina gani!

Waziri Mkuu wa Israeli, Benjamin ‘Bibi’ Netanyahu, si kiongozi wa kawaida. Hana mfano wake duniani. Wala hajali maoni ya watu.

Na hatambui maelezo kwamba Haniyeh alikuwa kiongozi wa kisiasa, si kijeshi, wa Hamas. Kwa maoni ya ‘Bibi’, ukiua, au ukila njama kuua raia wa Israeli, kuzimu kunakuita! Ni siku yako tu ambayo haijatimia.

Si ajabu wanamgambo wa Hamas walipowashambulia raia wa Israeli, wakawaua baadhi yao na kuwateka nyara wengine mnamo Oktoba 7, 2023, ‘Bibi’ akiapa kulipiza kisasi alionya: “Haniyeh ni maiti anayetembea.”

SOMA PIA: Baada ya sarakasi za siasa za Kenya, uhondo sasa upo Amerika

‘Bibi’ binafsi amefaulu kukwamisha juhudi zozote za kutekelezwa kwa ‘suluhisho la mataifa mawili’ huru na yenye amani, Israeli na Palestina, ambalo limependekezwa na jamii ya kimataifa kwa muda mrefu.

La ziada ni kwamba, ndiye waziri mkuu aliyeongoza kwa muda mrefu zaidi tangu taifa la sasa la Israeli liundwe mnamo 1947.

Amedumu mamlakani kwa muda mrefu – ila kuna vipindi vichache ambavyo alishindwa chaguzi – kutokana na msimamo wake mkali dhidi ya maadui wa Israeli.

Kila wanapotaka kiongozi wa kuwapigania, asiyetaka amani kati yao na maadui zao, anayeasisi na kuhimiza kutwaliwa kwa ardhi ya Wapalestina na walowezi wa Kiyahudi, Waisraeli humchagua ‘Bibi’.

Baada ya nyakati tukizi mno ambapo ameshindwa chaguzi, ‘Bibi’ amefanya juu chini, wakati mwingine kuwatia woga Waisraeli, ili kuhakikisha aliyemshinda hadumu mamlakani. Na bahati ikisimama kila anapojaribisha.

Kwa raia wa Israel, ‘Bibi’ ni kiongozi shupavu aliye radhi kuwafuata na kuwaangamiza maadui wao kokote waliko bila kuogopa lawama zozote, ilhali kwa Wapalestina anawakilisha pepo wa mauti.

SOMA PIA: Hivi ndivyo Rais Ruto anavyopaswa kuongoza nchi

Mja mkaidi kama mkia wa mbuzi, ‘Bibi’ alionyesha ukaidi huo alipohutubia Bunge la Amerika wiki jana, nyakati nyingine akigonga meza kwa hasira, akaapa kuwaangamiza magaidi wote wanaoilenga Israeli, siku chache kabla ya Haniyeh kuuawa.

Akitoa hotuba hiyo, aliwapuuzilia mbali na kuwadhihaki mamia ya waandamaji waliokuwa wakifoka kauli-mbiu za matukano nje ya Bunge hilo, wakipinga harakati za kijeshi ambazo Israeli inaendeleza dhidi ya Wapalestina katika Ukanda wa Gaza.

Ilikuwa ajabu sana kumwona mwandamanaji aliyetokea kimasomaso, huku kajitanda bendera ya kundi la wapiganaji wa Hamas, ambalo lilikwisha kutajwa na Amerika kuwa kundi la kigaidi, nje ya majengo ya bunge nchini Amerika!

Hali ilivyo sasa kwenye eneo zima la Mashariki ya Kati ni kuwa Waisraeli wanashangilia kwamba adui yao mkuu ameondolewa duniani, nao raia wengi wa mataifa jirani ya Israel wanaamini mwakilishi wa pepo wa mauti amefanya mambo yake. Amewatenda.

Kutokana na tukio hilo la hivi majuzi, watu wengi kote duniani wanatumbua macho yao kwenye runinga, kusikiliza redio, kusoma magazeti na kuvinjari mtandaoni wakiwa na hamu ya kujua kuuawa kwa Haniyeh kutakuwa na athari gani kidiplomasia.

Haniyeh alikuwa kiungo muhimu wa harakati za amani

Ukizingatia kwamba marehemu alikuwa kiungo muhimu katika harakati za kuleta amani kati ya Israeli na Hamas – na kukomesha vita vinavyoendelea kati yao – sasa ni sahihi kusema kuwa mustakabali wa vita hivyo haujulikani.

Ni kupitia gazeti hili ambapo nilimfahamu ‘Bibi’ Netanyahu alipochaguliwa kwa mara ya kwanza mnamo mwaka 1996, yapata miaka 28 iliyopita.

Wakati huo nilikuwa mwanafunzi wa Kidato cha Pili, na nilikumbana na picha ya ‘Bibi’ nilipokuwa nikipekua kurasa za gazeti hili ofisini mwa mwalimu wangu wa Kiswahili.

Mwanzo nilichangamkia picha hiyo sana kwa kuwa, kupitia hadithi nilizotambiwa na mamangu, nilimjua kakake, Yoni Netanyahu, aliyeuawa nchini Uganda akiwa katika harakati za kuwaokoa mateka walioshikiliwa na wanamgambo wa Palestina mnamo mwaka 1976.

Saa chache kabla ya kuuawa, ndege alimosafiria Yoni na wanajeshi wengine bingwa wa Israel ziliongezewa mafuta nchini Kenya kabla ya kuvamia Uganda, kulemaza jeshi la wanahewa la jirani yetu huyo, na kuwaokoa mateka wote kasoro mmoja.

Mamia ya raia wa Iran walipojitokeza kuhudhuria maandamano kabla ya mazishi ya kiongozi wa kisiasa wa Hamas Ismail Haniyeh jijini Tehran, Iran Agosti Mosi, 2024. Picha|Reuters

Katika fikra zangu za kitoto, hasa baada ya mamangu kunieleza jinsi aliyekuwa dikteta wa Uganda, Iddi Amin Dada, alivyoshirikiana na magaidi hao kuwateka na kuwatesa Waisraeli, Yoni alikuwa shujaa.

Ukitilia maanani taswira ya Shujaa Yoni niliyojengewa akilini na mamangu, utaelewa kwa nini nilifurahi nilipojua ndugu yake, ‘Bibi’, alichaguliwa kuiongoza Israel.

Katika fikra zangu kama Mkenya mchanga wakati huo, nilifurahi sana kwamba raia wa Israel waliona umuhimu wa ‘kurudisha mkono’, yaani kulipa wema kwa wema.

Ni baada ya kukua ambapo nilielewa kwamba ‘Bibi’ haisaidii Israel, hakika anaikwaza zaidi, kwa kuhakikisha kwamba haiishi kwa amani na majirani zake.

SOMA PIA: Vijana kuandaa maandamano bila Raila kwafaa kumkosesha usingizi Ruto

Ushawishi wa ‘Bibi’ umeenea mbali na karibu. Amefaulu kuwagawa Waamerika kwa makundi mawili: viongozi wa chama cha Democrat wanaosisitiza kutekelezwa kwa ‘suluhisho la mataifa mawili’, na wale wa Republican wanaotambua Israel na kupuuzilia mbali Palestina.

Usione ajabu kwamba ‘Bibi’ ameagiza Haniyeh aangamizwe; aliwahi kuwaagiza majasusi wa Israel wanaoogopwa mno kote duniani, Mossad, wamuue aliyekuwa kiongozi mkuu wa Hamas, Khalid Mashal, miaka ya tisini.

Mashal, ambaye tayari alikuwa ameshambuliwa kwa sumu, aliokolewa dakika chache kabla ya kuondoka duniani pale aliyekuwa rais wa Amerika, Bill Clinton, alipomshinikiza ‘Bibi’ kughairi nia ya kumwangamiza.

Sawa na jinsi jaribio la kumuua Mashal lilivyozua mzozo mkubwa wa kidiplomasia kati ya Israel kwa upande mmoja, na Amerika na mataifa kadha ya Kiarabu kwa upande wa pili, mauaji ya Haniyeh yanatarajiwa kuvuruga mambo. Letu jicho!

Yafahamu mataifa 10 barani Afrika yenye uwezo mkubwa wa kijes

Wanajeshi walinda amani wakipiga doria Libya

Uwezo wa kijeshi ni muhimu katika taifa lolote endelevu linalotaka kulinda mipaka yake mbali na maslahi yake kwa jumla .

Mtandao wa Global Firepower kupitia utafiti wake umeorodhesha uwezo wa kila jeshi barani Afrika kulingana na idadi ya wanajeshi, uwezo wake wa angani, ardhini, fedha zinazotengwa kugharamia majeshi hayo, vifaa vya kijeshi, mali asli, uwezo wa majini na kadhalika.

Hapa chini ni orodha ya majeshi 10 yenye uwezo mkubwa barani Afrika.

1. Misri

Kwa jumla Misri ndilo taifa linaloongoza kijeshi barani Afrika kutokana na ukubwa wa jeshi lake. Taifa hilo limewekwa katika nambari ya 12 kote duniani kutokana na uwezo wake.

MATANGAZO

Jeshi hilo la Misri linamiliki: Jeshi la majini, Jeshi la angani.

Takriban wanajeshi 500,000 wanahudumu katika jeshi hilo, ikiwa ni idadi kubwa zaidi ya taifa lolote barani Afrika.

Mbali na idadi kubwa ya wanajeshi wake, taifa hilo pia lina magari 10,000 ya kijeshi , magari 60,000 ya kimkakati wa kivita, ndege 1092 za kijeshi na visima vingi vya mafuta .

Rais Abdul Fattah al-Sisi,
Maelezo ya picha,Rais Abdul Fattah al-Sisi,

Hatahivyo kitu kinacholifanya jeshi hilo kuwa la aian ya kipekee Afrika ni uwezo wake katika jeshi la wanamaji ambalo lina meli za kijeshi na manuwari zenye uwezo wa kinyuklia.

Jeshi hilo limekuwa madarakani tangu mapinduzi ya kijeshi yaliomuondoa madarakani rais aliyechaguliwa kidemokrasia Mohammed Morsi na kumuweka al. Sisi madarakani . katika kura ya maoni iliofanyika mwaka huu, mapendekezo ya mabadiliko yaliowasilishwa yalilipatia jeshi uwezo mkubwa , suala ambalo wanaharakati wanasema ilipelekea jeshi kuingilia masuala ya raia.

2. Algeria

Sawa na mataifa mengine ya Afrika Magharibi, Algeria imefanikiwa katika mpaka wake mkubwa wa maji unaoipatia fursa kubwa. Taifa hilo limefanukiwa kuweka uwezo wa kijeshi ardhini, angani pamoja na majini. Hatahivyo taifa hilo linaorodheshwa la 27 kote duniani. Algeria ina takriban wanajeshi 130,000 wanaohudumu katika jeshi lake na ina magari 2000 ya kivita.

Jeshi la Algeria

Taifa hilo hatahivyo linakumbwa na mzozo baada ya rais wake wa miaka mingi kujiuzulu, lakini jeshi limepata sauti huku ukosefu wa uthabiti na ghasia za wenyewe kwa wenyewe zikiendelea.

Mkuu wa jeshi ameonesha wasiwasi wake kuhusu mapendekezo ya kucheleweshwa kwa uchaguzi ambayo yanaweza kusababisha ghasia nchini humo.

Jeshi nchini Algeria ndilo linaloweza kukabiliana na nguvu ya kiislamu iliochukua uongozi wa taifa hilo tangu uhuru wake.

3. Afrika Kusini

Kwa kuwa taifa hilo halijakumbwa na mzozo wa kivita kwa muda mrefu sasa, Afrika kusini inatumia jeshi lake lililopiga hatua kiteknolojia kuweka amani na ushirikiano wa kimataifa. Ukosefu wa mizozo haujalizuia taifa hilo kulitengea jeshi lake $4.6b.

Wanajeshi wa Afrika Kusini
Maelezo ya picha,Wanajeshi wa Afrika Kusini

Ndege zake na vifaa vya majini zinamiliki teknolojia ya kisasa na ijapokuwa lina wanajeshi 100,000, lina uwezo mkubwa.

Mbali na kumiliki teknolojia ya hali ya angani na ardhini , jeshi la Afrika Kusini lina sifa kubwa.

4. Nigeria

Taifa hilo la Afrika magharibi limekuwa likikabiliana na wapiganaji wa Boko Haram siku nenda siku rudi kwa zaidi ya muongo mmoja sasa.

Licha ya ufanisi mkubwa kupatikana katika awamu ya kwanza ya rais Buhari, Jeshi limepata mapigo katika kipindi cha mwaka mmoja kwasababu limefunzwa kukabiliana na jeshi jingine badala ya vita vya gorilla vinavyotumiwa na adui.

Wanajeshi wa Nigeria
Maelezo ya picha,Wanajeshi wa Nigeria

Kama Algeria na Misri, Jeshi la taifa hilo lina uwezo wa kuendelea na vita kutokana na raslimali ya mafuta linayomiliki.

Nigeria ina zaidi ya magari 1800 ya kivita , vifaru 250 , magari mengine 6000 ya kimkakati wa kivita mbali na ndege 300 za kijeshi na meli 25 za jeshi la wanamaji.

Hatahivyo uwezo wa wanamaji wake upo chini ikilinganishwa na mataifa mengine ya Afrika yalio na mpaka wa majini.

5. Ethiopia

Ndilo taifa la pakee lisilo na mpaka wa majini kati ya mataifa matano bora yenye uwezo mkubwa wa kijeshi.

Taifa hilo limeelekeza raslimali yake kuu kujenga jeshi lake .

Mtandao wa GFP haufutilii mbali mataifa yasio na mpaka wa majini kwa kutokuwa na jeshi la wanamaji.

Waziri mkuu Abiy Ahmed amekuwa na uhusiano mzuri na jeshi lake tangu alipochukua madaraka huku wanajeshi wakionekana wakitembelea baadhi ya miradi ya waziri huyo na akiwaelezea maono yake kuhusu taifa hilo.

Taifa hilo kwa miaka kadhaa sasa limekumbwa na mzozo wa wenyewe kwa wenyewe , uwezo wa kuwa na jeshi thabiti umetajwa kuwa muhimu kutokana na tisho la wapiganaji wa Al-Shabab.

Taifa hilo kwa sasa lina wanajeshi 140,000 huku watu milioni 2 kila mwaka wakiafikia umri wa kujiunga na jeshi.

6. Angola

Jeshi la Angola lina vitengo vitatu: Jeshi la angani, ardhini na lile la wanamaji.

Mapema mwaka huu ajenda ya mabadiliko ya rais Lourenco ilipitishwa jeshini ambapo majenarali 88 wa jeshi waliwachishwa kazi.

Hatua hiyo inajiri baada ya kamanda wa jeshi kupoteza kazi yake alipotajwa na mwanasheria mkuu kuwa katika uchunguzi wa ufisadi.

Ndege ya kivita

Hifadhi ya mafuta ya taifa hilo imelifanya kuwa na uwezo wa kusimamia bajeti kubwa ya jeshi lake.

Taifa hilo lina wanajeshi 100,000 wanaosaidiwa na magari 585 ya kijeshi, vifaru 300 ,ndege za kijeshi 285 na meli 57 za wanamaji.

7. Morocco

Mapema mwaka huu, Mfalme Mohammed VI alitoa wito kwa serikali kusajili raia 10,000 wa Morocco kuhudumia jeshini kwa lazima kwa mwaka mmoja na idadi hiyo ilitarajiwa kuongezeka hadi 15,000 kufikia mwaka 2020.

Jeshi la Kifalme lina wafanyakazi 196,000.

Wanajeshi wa Morocco
Maelezo ya picha,Wanajeshi wa Morocco

Pia lina ndege 291, magari 2,720 ya kivita, vifaru 1,109 na manowari 121.

Jeshi hilo pia lilianza mazoezi ya kijeshi ambayo yalipewa jina na Marekani la “African Lion 2019” mnamo mwezi Machi ambayo ililenga kuifunza dhidi ya ugaidi na ghasia za itikadi kali.

Hatahivyo, licha ya bajeti yake kubwa, washirika wake wanaowafadhili kama vile Marekani wameripoti uwepo wa “ufisadi, urasimu usiofaa na kiwango duni cha elimu katika upandishaji wa vyeo jeshini.”

Upelekaji wa vikosi vyake Magharibi mwa Sahara bado ndio changamoto yake kubwa hadi hivi sasa.

8. Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo

Vita mashariki mwa DR Congo

Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo ni ya pili kwa idadi kubwa ya watu Afrika ambayo ni milioni 86 Umoja wa Mataifa bado una majeshi yake nchini humo kwasababu vikosi vyake haviwezi kukabiliana na operesheni za kuleta amani kikamilifu.

Mabadiliko ya kiusalama nchini humo yalianza 2003 baada ya kipindi cha vita vya wenyewe kwa wenyewe na bado inakabiliana na juhudi za washirika wake wa kijeshi wa nchi za nje katika taasisi ya taifa ya usalama.

Nchi hiyo ina wanajeshi 134, 000 ingawa licha ya idadi hiyo bado iko nyuma kwa misingi ya mafunzo ikilinganishwa na wanajeshi wa nchi zingine.

9.Tunisia

.

Jeshi la Tunisia lina maafisa 80,000 na linashirikisha: brigedi tatu zzilizopo katika eneo la Kairouan (3), Gabès (wa 1) na Béja (wa pili). Kila moja linamiliki mzinga mmoja wa aina ya M60 Patton). jeshi hilo lina vifaru 90 na vidogo 55. Kwa jumla taifa hilo lina ndege 155 za kusafirisha wanajeshi, ndege 10 za kivita na helikopta 101.

10. Sudan

Hakujakuwa na amani wala uthabiti katika eneo la Afrika Kaskazini tangu kung’olewa madarakani kwa Muammar Gaddafi.

libya imekuwa katika mapigano ya wenyewe kwa wenyewe tangu kuuwa kwa rais Muammar Gadaffi
Maelezo ya picha,libya imekuwa katika mapigano ya wenyewe kwa wenyewe tangu kuuwa kwa rais Muammar Gadaffi

Jeshi hilo lina vifaa imara na bila shaka ni kutokana na pesa ambazo chanzo chao ni uuzaji wa mafuta.

Nchi hiyo sasa hivi imegawanyika kati ya Tripoli na jenerali aliyeasi, Jenerali Haftar, ambye anaungwa mkono na nchi za magharibi zenye nguvu kama vile Marekani.

Serikali huko Tripoli inakabiliana na kuondoa wanajeshi waliovamia mji huo kwasababu haina kikosi thabiti.

Lakini licha ya hayo, nchi hiyo bado ina magari 2,500 ya kivita, vifaru 500, zana 600 za kivita na magari 6,500 ya usafirishaji wanajeshi

Wakati huohuo Global Firepower imeorodhesha Kenya katika nafasi 12 , Uganda katika nafasi 14 huku Tanzania ikiwa katika nafasi 23 barani Afrika.

Muhtasari

  • Waombolezaji wakusanyika wakati kiongozi wa Hamas Haniyeh anazikwa nchini Qatar
  • Paris Olimpiki 2024: Muogeleaji wa Slovakia azimia baada ya shindano
  • Vita vya Ukraine: Mashambulizi ya Urusi yakaribia kilele chake mashariki mwa Ukraine
  • Ismail Haniyeh: Mazishi ya kiongozi wa Hamas yafanyika leo Qatar
  • Kuuawa kwa kiongozi wa Hamas ‘haisaidii’ mazungumzo ya kusitisha mapigano, anasema Biden
  • Uingereza: Saba wasakwa na polisi baada ya hoteli ya wahamiaji kushambuliwa
  • Putin akutana na raia wa Urusi walioachiliwa huru baada ya kubadilishana wafungwa
  • Ubadilishanaji mwingine wa wafungwa ulioweka historia
  • Wamarekani walioachiliwa huru Urusi kwa mabadilishano ya wafungwa waungana na familia
  • Mashindano ya Olimpiki: Biles ashinda taji lingine na kufikisha jumla ya medali sita za dhahabu
  • Nigeria: Watu kadhaa wauawa kwa kupigwa risasi katika maandamano ya gharama ya maisha
  • Ushahidi mkubwa waonyesha upinzani ulishinda uchaguzi Venezuela – Blinken
  • Kiongozi wa Hezbollah asema mzozo na Israel upo katika ‘awamu mpya’ baada ya mauaji
  • Wafungwa 24 waachiliwa katika mabadilishano makubwa kati ya Urusi na nchi za Magharibi tangu Vita Baridi

Moja kwa moja

  1. Saa 1 iliyopita. Na mpaka hapo ndio tunafikia mwisho wa matangazo yetu ya mubashara kwa leo, tukutane tena hapo kesho majaaliwa.
  2. Saa 2 zilizopita. Wanigeria wakabiliwa na marufuku ya kutotoka nje ya saa 24 kufuatia maandamanofCHANZO CHA PICHA,AFP Maelezo ya picha,Waandamanaji wanapinga gharama ya juu ya maisha na kile wanachosema ni “utawala mbaya”Mamilioni ya wakaazi kaskazini mwa Nigeria wanakabiliwa na amri ya kutotoka nje ya saa 24 huku kukiwa na maandamano ya nchi nzima kupinga gharama kubwa ya maisha.Serikali katika majimbo ya Kano, Jigawa, Yobe na Katsina zimewaamuru wenyeji kutotoka nje ya nyumba zao – na kwa hivyo wasihudhurie maandamano – siku ya Ijumaa.Mamlaka zinasema amri ya kutotoka nje ni muhimu kwa sababu “vigogo” wameteka nyara maandamano ili kupora na kuharibu mali.Hali ya usalama imeimarishwa kote nchini huku waandamanaji na wanaharakati na waandamanaji wakipanga “siku tisa za hasira”.Katika siku ya kwanza, maandamano katika mji wa kaskazini wa Kano yalivutia umati mkubwa zaidi.Polisi walifyatua risasi na mabomu ya machozi – na kunyunyizia waandamanaji maji ya pilipili – kujaribu na kuwatawanya maelfu ya waandamanaji. Watu watatu waliuawa kwa kupigwa risasi na wengine wengi kujeruhiwa.Waporaji pia walivamia ghala karibu na nyumba ya gavana wa Kano na polisi wanasema tangu wakati huo watu 269 wamekamatwa na kupatikana kwa maboksi mengi ya mafuta ya karanga yenye ujazo wa lita 25 na vitu vingine vilivyochukuliwa.Kwa mujibu wa shirika la kutetea haki za binadamu la Amnesty International, waandamanaji 13 kote nchini Nigeria waliuawa na vikosi vya usalama katika siku ya kwanza ya maandamano hayo.
  3. Saa 2 zilizopita. Habari za hivi punde,Uganda yathibitisha wagonjwa wawili wa Homa ya Nyani.CHANZO CHA PICHA,REUTERS. Wizara ya afya nchini Uganda imethibitisha kugunduliwa kwa kesi mbili za maradhi ya Homa ya Nyani {Mpox} nchini humo.Kulingana na taarifa iliotumwa kwa vyombo vya habari na mkurugenzi wa habari katika wizara ya afya nchini humo, maradhi hayo yalibainika baada ya kuchukuliwa sampuli kutoka kwa wagonjwa wawili.Taarifa hiyo inasema wawili hao ni mwanamke mmoja wa miaka 37 kutoka baraza la manispaa ya mpondwe ambaye ameolewa na mwanamume raia wa DR Congo na mwanamke mwengine mwenye umri wa miaka 22 raia wa DR Congo kutoka kijiji cha Bunywisa II katika wilaya ya Kasese.Wote wawili walikuwa na upele katika ngozi zaona dalili zinazohusishwa na homa ya nyani .Taarifa hiyo inaongezea kwamba sampuli za wawili hao zilifanyiwa ukaguzi na Taasisi ya kupima virusi nchini Uganda UVRI tarehe 24 mwezi Julai 2024.Kesi za maradhi hayo ni miongoni mwa sita zilizogunduliwa katika mpaka wa Bwera wilayani Kasese.Matokeo ya ukaguzi huo yamebaini kwamba maambukizi hayo hayakufanyika nchini Uganda na kufikia sasa hakuna maambukizi yaliotokana na visa hivyo viwili.Tayari wizara ya Afya nchini Uganda imepeleka timu ya maafisa wa kukabiliana na dharura katika Wilaya ya Kasese ili kushirikiana na maafisa wa afya katika eneo hilo ili kudhibiti visa hivyo viwili.Kufikia sasa watu tisa wanaodaiwa kushikana kimwili na waathiriwa wanafuatiliwa kwa karibu.Uganda inaendelea kufuatialia kwa karibu mambukizi ya maradhi hayo nchini DR Congo ambapo imatengazwa kwamba karibu mikoa yote imeripoti visa vya maambukizi , huku mkoa wa hivi karibuni ukiwa ule wa Kivu Kaskazini hususan mjini Goma.
  4. Saa 3 zilizopita Waombolezaji wakusanyika wakati kiongozi wa Hamas Haniyeh anazikwa nchini QatargCHANZO CHA PICHA,KWA HISANIMaelezo ya picha,Shughuli ya mazishi tofauti ya mazishi ya kiongozi huyo wa kisiasa wa Hamas ilifanyika mjini Tehran siku ya AlhamisiShughuli ya mazishi ya mkuu wa Hamas Ismail Haniyeh, ambaye aliuawa nchini Iran siku ya Jumatano, inaendelea nchini Qatar.Swala ya mazishi ya Haniyeh itafanyika katika msikiti wa Imam Muhammed bin Abdul Wahhab – mkubwa zaidi nchini Qatar – kabla ya kuzikwa kwenye makaburi huko Lusail, mji ulio kaskazini mwa Doha.Watu mashuhuri katika harakati ya Hamas – akiwemo mtangulizi wake kama kiongozi, Khaled Meshaal – walisimama kwenye lami kwenye uwanja wa ndege wa Doha wakati ndege iliyokuwa imebeba jeneza la Haniyeh ikitua kutoka Iran Alhamisi alasiri.Haniyeh aliuawa alipokuwa katika ziara nchini Iran na washirika wake wameilaumu Israel, ingawa Israel haijadai kuhusika na kifo chake. Mauaji ya Haniyeh yametajwa kuwa ni kikwazo kwa usitishaji mapigano,katika vita vya Israel na Hamas.Hamas ilisema kuwa “viongozi wa Kiarabu na Kiislamu” na wale wanaohusika na makundi mengine ya Palestina watahudhuria, pamoja na wananchi.Uturuki na Pakistan zilitangaza siku ya maombolezo siku ya Ijumaa kwa heshima ya Haniyeh, wakati Hamas imetoa wito wa “maandamano ya hasira … kutoka kila msikiti” yafanyike baada ya sala ya Ijumaa kupinga mauaji ya Haniyeh.Katika hafla tofauti ya mazishi ya Haniyeh ambayo ilifanyika Tehran siku ya Alhamisi, Kiongozi Mkuu wa Iran, Ayatollah Ali Khamenei, aliongoza sala – akiwa ameapa hapo awali kwamba Israeli itapata “adhabu kali” kwa mauaji hayo.Unaweza pia kusoma:Kiongozi mkuu wa Hamas Ismail Haniyeh ameuawa nchini Iran – kundi hilo lasemaMfahamu kiongozi wa Hamas aliyewanyima usingizi IsraeliMkuu wa jeshi la Hamas aliuawa katika shambulizi la Julai, Israel yasema
  5. Saa 5 zilizopita Paris Olimpiki 2024: Muogeleaji wa Slovakia azimia baada ya shindanofCHANZO CHA PICHA,GETTY IMAGES Maelezo ya picha,Potocka alishikilia nafasi ya 15 kwenye Mashindano ya Dunia mapema mwaka huuMuogeleaji wa Slovakia Tamara Potocka anapokea matibabu baada ya kuzirai kufuatia misururu ya kuogelea mita 200 katika uwanja wa La Defense Arena kwenye Michezo ya Olimpiki ya Paris.Potocka, mwenye umri wa miaka 21, alianguka kando ya bwawa, ambapo alipokea huduma ya matibabu ya haraka ikiwa ni pamoja na kupewa oksijeni.Timu ya Slovakia iliiambia BBC Sport kuwa Potocka ni mgonjwa wa pumu na alikuwa na shambulio la pumu.Potocka ameweza kupata fahamu na aliweza kuwasiliana na madaktari. Amepelekwa hospitali kwa uangalizi zaidi wa matibabu.Unaweza pia kusoma:Jedwali la medali ya mashindano ya Olimpiki ya Paris 2024Paris Olimpiki 2024: Wajue nyota wa kimataifa wa kuwatazamaSare za 9 za kuvutia zitakazovaliwa na wachezaji katika Olimpiki 2024
  6. Saa 5 zilizopita Vita vya Ukraine: Mashambulizi ya Urusi yakaribia kilele chake mashariki mwa UkrainefCHANZO CHA PICHA,REUTERS Maelezo ya picha,Mwanajeshi wa Ukraine akiwa katika eneo la mapigano karibu na Chasovoy YarMashambulizi ya Urusi, ambayo yamekuwa yakiendelea kwa karibu miezi 10 na kuongezeka mwishoni mwa majira ya masika na kiangazi yanafikia kilele chake.Mwishoni mwa Julai, vikosi vya Urusi viliweza kuongeza kasi ya mashambulizi katika mwelekeo muhimu – kuelekea Pokrovsk. Ili kumzuia adui, na kuilazimisha Ukraine kuhamisha hifadhi na vifaa vifaa.Lakini hali hii inadhoofisha ulinzi katika maeneo mengine yaliyo hatarini – kwa hivyo, katika miezi miwili ya majira ya kiangazi, Warusi walipata mafanikio ya mbinu katika mwelekeo wa Toretsk, Chasovoy Yar, na walifanikiwa pia kusonga mbele karibu na Krasnohorivka na Vugledar.Katika Mkoa wa Kharkiv, wanajeshi wa Urusi waliviteka vikosi vya Ukraine karibu na Liptsi na Vovchansk, na pia wameshambulia katika maeneo ya Mto Oskil karibu na Kupyansk. Hapa kulikuwa na tisho la kukatwa kwa daraja la Ukraine lililopo kwenye ukingo wa mashariki.Jeshi la Urusi karibu lilikaribia maeneo muhimu ya kimkakati ya Jeshi la Ukraine mashariki mwa Ukraine.Lakini swali linabaki ni iwapo litakuwa na nguvu za kutosha hadi shambulio la mwisho?.Unaweza pia kusoma:YA MSINGI:Mzozo wa Ukraine: Kwanini Urusi inaivamia Ukraine na Putin anataka nini?UFAFANUZI:Mzozo wa Ukraine: Swift ni nini na kwa nini kuipiga marufuku Urusi ni muhimu sana?UCHAMBUZI:Mzozo wa Ukraine: Putin humsikiliza nani?KWENYE RAMANI:Uvamizi wa Ukraine: Shambulio la Urusi kwenye ramaniZELENSKY:Volodymyr Zelensky: Mfahamu rais wa Ukraine aliyeacha umaarufu wake wa TV na kuingia kwenye siasaPUTIN:Vladimir Putin: Rais wa Urusi aliyeagiza shambulio Ukraine
  7. Saa 6 zilizopita Ismail Haniyeh: Mazishi ya kiongozi wa Hamas yafanyika leo QatargCHANZO CHA PICHA,REUTERS Mazishi ya mwili wa Mkuu wa ofisi ya kisiasa ya Hamas, Ismail Haniyeh,yamefanyika nchini Qatar leo, Ijumaa, kufuatia mauaji yake mjini Tehran katika shambulio linalohusishwa na Israel, huku jeshi la Israel likitangaza, kwa upande wake, kuwa “shambulio pekee ambalo lilitekelezwa usiku huo huko Mashariki ya Kati ni lile lililomlenga Fouad Shukr katika kitongoji cha kusini cha Beirut.Siku ya Alhamisi mchana, jeneza la Haniyeh, ambaye aliuawa pamoja na mlindi wake wake wa kibinafsi, liliwasili Doha katika makazi yake katika mji mkuu wa Iran, Tehran.Kabla ya hapo, umati mkubwa wa watu ulishiriki katika hafla maarufu za mazishi yake Alhamisi asubuhi katika mji mkuu wa Iran, ambapo Kiongozi Mkuu wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran, Ayatullah Ali Khamenei, aliwaongoza waumini katika mazishi ya Haniyeh katika Chuo Kikuu cha Tehran, na waombolezaji walibeba picha za mkuu wa ofisi ya kisiasa ya Hamas na bendera za Palestina.Baada ya swala hiyo, mbele yakamanda wa pili wa vuguvugu la Hamas, Khalil Al-Hayya, jeneza lililokuwa limefungwa kwa bendera ya Palestina lilibebwa mabegani kabla ya kusafirishwa hadi katika makaburi ya Lusail nchini Qatar kwa ajili ya mazishi.Qatar yamekuwa makazi yake na wanachama wengine wa Ofisi ya kisiasa ya Hamas.Unaweza pia kusoma:Kiongozi mkuu wa Hamas Ismail Haniyeh ameuawa nchini Iran – kundi hilo lasemaMfahamu kiongozi wa Hamas aliyewanyima usingizi IsraeliMkuu wa jeshi la Hamas aliuawa katika shambulizi la Julai, Israel yasema
  8. Saa 7 zilizopita Kuuawa kwa kiongozi wa Hamas ‘haisaidii’ mazungumzo ya kusitisha mapigano, asema BidengCHANZO CHA PICHA,REUTERSMaelezo ya picha,Marekani imesema kuwa haikuhusika katika mauaji ya kiongozi wa kisiasa wa HamasRais wa Marekani Joe Biden amesema kuwa mauaji ya kiongozi wa Hamas Ismail Haniyeh “hayasaidii” mazungumzo kuhusu uwezekano wa kusitisha mapigano huko Gaza.Haniyeh aliuawa katika ziara yake katika mji mkuu wa Iran, Tehran siku ya Jumatano. Iran na washirika wake wameilaumu Israel, ingawa Israel bado haijatoa maoni yoyote kuhusu kifo chake.Haniyeh alikuwa afisa mkuu wa Hamas na alihusika sana katika mazungumzo ya kusitisha mapigano na kuwaachilia mateka kutoka kituo chake nchini Qatar.Bwana Biden alisema “ana hofu sana” kuhusu kuongezeka kwa mvutano katika Mashariki ya Kati. “Tuna msingi wa kusitisha mapigano. Yeye [Waziri Mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu] anapaswa kuendelea nao [Hamas] wanapaswa kuendelea nao sasa.”Israel na Hamas hivi majuzi walianza tena mazungumzo ya muda, yasiyo ya moja kwa moja ili kujaribu kufikia usitishaji wa vita huko Gaza, ingawa kumekuwa na maelezo yanayokinzana kuhusu mafanikio ya mazungumzo hayo.Mwishoni mwa mwezi Mei, Bw Biden alielezea kile alichosema kuwa ni masharti ya pendekezo la Israeli la kusitisha mapigano. Huu umekuwa msingi wa mazungumzo ya moja kwa moja kati ya Hamas na Israel tangu wakati huo, huku Qatar, Misri na Marekani zikiwa wapatanishi.Mapema wiki hii, Israel na Hamas zilishutumu kila mmoja kwa kukwamisha maendeleo ya mazungumzo.Hamas ilisema Israel imeanzisha masharti mapya, huku ofisi ya Bw Netanyahu ikisema Hamas imetaka kufanyika kwa mabadiliko 29 kwenye pendekezo hilo.Unaweza pia kusoma:Kiongozi mkuu wa Hamas Ismail Haniyeh ameuawa nchini Iran – kundi hilo lasemaMfahamu kiongozi wa Hamas aliyewanyima usingizi IsraeliMkuu wa jeshi la Hamas aliuawa katika shambulizi la Julai, Israel yasema
  9. Saa 7 zilizopita Uingereza: Saba wasakwa na polisi baada ya hoteli ya wahamiaji kushambuliwagCHANZO CHA PICHA,HAMPSHIRE CONSTABULARY
  10. Watu saba wanatafutwa na polisi baada ya vitu kurushwa nje ya hoteli inayohifadhi wahamiaji wakati wa maandamano yaliyofanyika katika eneo la Aldershot.Polisi wa Hampshire watu wachache kati ya watu 200 walioandamana nje ya Hoteli ya Kimataifa ya Potters walihusika katika tukio hiloJumatano jioni.Kikosi hicho kimetoa picha za watu wanane ambao kingependa kupata utambulisho wao.Maandamano hayo yanafuatia ghasia zilizotokea katika maeneo mbali mbali kote nchini baada ya wasichana watatu kuuawa katika mji wa Merseyside wa Southport siku ya Jumatatu.Bebe King, sita, Elsie Dot Stancombe, saba, na Alice Dasilva Aguiar mwenye umri wa miaka tisa waliuawa kwa kuchomwa kisu kwenye darasa la mada ya Taylor Swift.Axel Muganwa Rudakubana mwenye umri wa miaka 17, alifikishwa mahakamani akikabiliwa na mashtaka matatu ya mauaji ya watoto hao nakujaribu kuwauwa watu wengine 10, baada ya watoto wengine wanane na watu wazima wawili kujeruhiwa vib Putin akutana na raia wa Urusi walioachiliwa huru baada ya kubadilishana wafungwa
  11. Rais wa Urusi Vladimir Putin amekutana na wafungwa walioachiwa huru walipowasili Moscow, akisema watapewa tuzo za serikali.

KIPENGA CHA MICHEZO

West Ham wapo ukingoni kusaini mikataba miwili, timu inayoshiriki Ligi Kuu ya England imefikia makubaliano ya kumsajili Romelu Lukaku na Arsenal wakaribia kumnunua Mikel Merino.

Arsenal, Real Madrid na Atletico Madrid wote wanamtaka kiungo wa kati wa Ufaransa Adrien Rabiot, 29, ambaye ni mchezaji huru baada ya kuondoka Juventus. (Gazetta, kwa Kiitaliano)

West Ham wanakaribia kuwasajili mshambuliaji wa Borussia Dortmund na Ujerumani Niclas Fullkrug, 31, na fowadi wa Leeds wa Uholanzi Crysencio Summerville, 22. (Sky Sports).

Nottingham Forest hailengi kumnunua kiungo wa kati wa Uingereza Morgan Gibbs-White, 24, licha ya Newcastle, Arsenal, Aston Villa na Chelsea kutaka kumnunua. (HITC)

TH

West Ham wamekubali masharti ya kibinafsi ya kumsajili beki wa kulia Aaron Wan-Bissaka, 26, lakini bado hawajakubaliana ada na Manchester United, ambao wanataka £18m badala ya £10m iliyotolewa. (Sky Sports Ujerumani)

Fulham wapo kwenye mazungumzo ya hatua ya juu kumnunua beki wa kati wa Villarreal Mhispania Jorge Cuenca, 24, kwa £6.7m. (Standard)

Napoli wana ofa ya euro 12m (£10.2m) tayari kwa kiungo wa kati wa Brighton na Scotland Billy Gilmour mwenye umri wa miaka 23 na wanasubiri wachezaji kuondoka katika klabu hiyo kabla ya kuitoa. (Sky Sports Italia)

Roma wamekubali mkataba na Girona kumsajili mshambuliaji wa Ukraine Artem Dovbyk, 27, kwa £28.8m – huku AC Milan ikionyesha nia ya kumsajili fowadi wa Roma wa Uingereza Tammy Abraham, 26. (Repubblica, kwa Kiitaliano – usajili unahitajika

Unaweza pia kusoma

TH

Arsenal wanakaribia kufikia dili la £25m kumsajili kiungo wa kati wa Uhispania Mikel Merino, 28, kutoka Real Sociedad. (Mirror)

Stuttgart wataondoa nia yao ya kutaka kumnunua mshambuliaji wa Brighton na Ujerumani Deniz Undav, 28, na kuangalia walengwa wapya hivi karibuni ikiwa hawawezi kufikia makubaliano na Albion. (Kicker, kwa Kijerumani)

Newcastle wapo kwenye hatua ya juu ya mazungumzo na Sheffield United ili kumsajili mshambuliaji wa Blades wa Denmark William Osula, 20 kwa dau la awali la £10m. (Telegraph – usajili unahitajika)

Leipzig itakataa ombi la pili kutoka kwa Barcelona kumnunua kiungo wa kati wa Uhispania Dani Olmo, 26. (Sport, kwa Kihispania)

TH

Aston Villa wamefikia makubaliano na Chelsea kumnunua mshambuliaji wa Ubelgiji Romelu Lukaku, lakini mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 31 anataka kujiunga na Napoli ya Antonio Conte. (Il Mattino, kwa Kiitaliano – usajili unahitajika)

Bristol City, Stoke na Birmingham City wanavutiwa na mlinzi wa Burnley raia wa Ireland Luke McNally, 24. (Football Insider)

Stoke City inamtaka kiungo wa kati wa Blackburn Rovers Muingereza Lewis Travis, 26. (Teamtalk)

Kiungo wa kati wa Manchester City Muingereza Jacob Wright, 18, amekubali kuhamia Peterborough United kwa mkopo. (Football Insider)

MAKALA YA OLIMPIKI PARIS 2024

Mwanariadha Beatrice Chebet wa Kenya amefuzu Katika fainali ya mbio na mita 5000m wanawake baada ya kushinda mkumbo wa pili kwa 15:00.72. Mashindano yanayoendelea ya Olimpiki Jijini Paris Ufaransa

Morocco 4-0 USA

Timu ya Taifa ya Soka ya Morocco imeigandamiza Marekani na kufunzu katika awamu nusu fainali michuano inayoendelea ya Olimpiki Jijini Paris Ufaransa.

KipengaChaMichezo

AfrikaLeoJioni

olympicsparis2024

TheHeartBeatofAfrica

All Rights Reserved © Cantona Group Ltd||2024


Discover more from cantonadigital

Subscribe to get the latest posts sent to your email.

Leave a comment