Radio Fortune Africa -Na Cantona Joseph
https://zeno.fm/radio/radio-fortune-africa

Muhtasari
- Maduro aahidi kutoa data ya upigaji kura huku waangalizi wakisema uchaguzi wa Venezuela ‘si wa kidemokrasia’
- Chui ashambulia wanaume wawili katika kambi ya jeshi la wanahewa Afrika Kusini
- Hezbollah yathibitisha kamanda wake alifariki katika shambulizi la Israel
- Kijana, 17, ashtakiwa kwa mauaji ya wasichana watatu Uingereza
- Watatu wanaotuhumiwa kupanga njama ya 9/11 wafikia makubaliano ya kukiri mashtaka – Pentagon
Moja kwa moja HII Ni Idhaa Ya Kiswahili Ya Radio Fortune Africa
- Maduro aahidi kutoa data ya upigaji kura huku waangalizi wakisema uchaguzi wa Venezuela ‘si wa kidemokrasia’
CHANZO CHA PICHA,EPA - Rais wa Venezuela Nicolas Maduro amesisitiza kuwa chama chake kiko tayari kuwasilisha majumuisho yote ya kura kutokana na uchaguzi wenye utata nchini humo baada ya waangalizi wa uchaguzi kusema kuwa “hauwezi kuchukuliwa kuwa wa kidemokrasia”.Tamko la Baraza la Kitaifa la Uchaguzi (CNE) kwamba Bw Maduro alishinda limesababisha maandamano ya siku mbili, huku upinzani nchini humo ukisema kwamba hesabu za kura zinaonyesha mgombea wake, Edmundo González, alishinda kwa kura nyingi.Mashirika yasiyo ya kiserikali yanasema kumekuwa na vifo vya takriban watu 11 katika ghasia zinazohusiana na maandamano huku makumi ya wengine wakijeruhiwa.Akizungumza na wanahabari siku ya Jumatano, Bw Maduro alisema tena kwamba sababu ya serikali yake kutochapisha matokeo ya uchaguzi ni “udukuzi” kwenye tovuti ya baraza la uchaguzi.Pia alidai alikuwa na “uthibitisho” kuwa kiongozi wa upinzani Maria Corina Machado anahusika na “vurugu” zinazoshuhudiwa.Alidai kuwa waandamanaji walikuwa wanakiuka katiba na kuomba Mahakama ya Juu Zaidi kuchukua hatua, ambayo inaweza kusababisha kukamatwa kwa watu wengi wa upinzani au waandamanaji.Soma zaidi:Raia wa Venezuela wakabiliana na polisi baada ya matokeo ya uchaguzi yaliyokuwa na utataNicolás Maduro: Kiongozi ambaye ameapa kushinda uchaguzi ‘kwa njia yoyote ile’Maduro ashinda uchaguzi uliokumbwa na utata VenezuelaDroni za kujihami: Iran yaisaidia Venezuela kumiliki silaha hiCrowdStrike yashtakiwa na wanahisa wake kwa hitilifau ya kiufundi iliyotokea kote duniani
CHANZO CHA PICHA,REUTERS - Kampuni ya CrowdStrike imeshitakiwa na wanahisa baada ya sasisho bovu la programu ya kampuni hiyo ya usalama wa mtandao kuharibu zaidi ya kompyuta milioni nane na kusababisha usumbufu wa kiufundi kote duniani .Kesi hiyo inashutumu kampuni hiyo kwa kutoa taarifa “za uwongo na za kupotosha” kuhusu majaribio yake ya programu.Pia inasema bei ya hisa ya kampuni ilishuka kwa 32% katika siku 12 baada ya tukio, na kusababisha hasara ya thamani ya $25bn (£14.5bn).CrowdStrike inakanusha madai hayo na inasema itajitetea dhidi ya kesi iliyopendekezwa dhidi yake.Kesi iliyowasilishwa katika mahakama ya shirikisho ya Austin, Texas, inadai kuwa wasimamizi wa CrowdStrike walilaghai wawekezaji kwa kuwafanya waamini kuwa masasisho ya programu ya kampuni yalijaribiwa vya kutosha.Kesi hiyo inatafuta kiasi ambacho hakijabainishwa cha fidia kwa wawekezaji waliokuwa na hisa za CrowdStrike kati ya tarehe 29 Novemba na 29 Julai.Inamtaja afisa mkuu mtendaji George Kurtz, ambaye alisema katika mkutano mnamo 5 Machi kwamba programu ya kampuni hiyo “imeidhinishwa, imejaribiwa na kuthibitishwa.”CrowdStrike iliambia BBC News kwamba inapinga madai hayo.”Tunaamini kuwa kesi hii haina mashiko na tutatetea kampuni kwa nguvu,” msemaji alisema
- Chui ashambulia wanaume wawili katika kambi ya jeshi la wanahewa Afrika Kusini
CHANZO CHA PICHA,GETTY IMAGES - Chui amewashambulia wanaume wawili katika kambi ya jeshi la wanahewa la Afrika Kusini ambalo linapakana na mbuga maarufu duniani ya Kruger National Park.Mmoja wa waliovamiwa ambaye ni mwanajeshi, alikuwa ameenda kukimbia.Mwingine, raia anayefanya kazi kwenye kituo hicho, alikutana na chui huyo akiwa anatembea, msemaji wa jeshi la wanahewa alisema.Wawili hao walilazwa hospitalini wakiwa na mikwaruzo lakini hawakuwa na majeraha makubwa, Brig Jenerali Donavan Chetty aliambia BBC.Mmoja ameruhusiwa kwenda nyumbani na mwingine anatarajiwa kuondoka siku ya Alhamisi.Siku ya Jumatano, chui huyo alichukuliwa na kuhamishwa hadi kwenye hifadhi karibu kilomita 100 (maili 62) kutoka kambi ya jeshi la wanahewa la Hoedspruit, kufuatia mashambulizi ya wiki iliyopita.Jenerali Chetty alisema kukutana na chui ni jambo la kawaida, lakini huwa sio hatari kwa wale wanaoishi na kufanya kazi karibu na mbuga hiyo.Mbuga hiyo, ambayo ni kitovu cha utalii kwa kuwa na idadi kubwa ya wanyamapori, imezungushiwa uzio.Hata hivyo, Jenerali Chetty alisema ni vigumu kuzuia chui, ambao wanajulikana kuwa wepesi wa kuruka uzio.Chui ni wanyama ambao huwa na shughuli nyingi nyakati za usiku hasa kutafuta mawindo mbalimbali, wakiwemo nyumbu, swara na samaki, tovuti ya Mbuga ya Kitaifa ya Kruger inasema.Pia unaweza kusoma:Nini cha kufanya ikiwa utakutana na chui?Jinsi ya kuwashinda
- Hezbollah yathibitisha kamanda wake alifariki katika shambulizi la Israel
CHANZO CHA PICHA,HEZBOLLAH HANDOUTHezbollah imethibitisha kuwa mmoja wa makamanda wake wakuu wa kijeshi aliuawa katika shambulio la anga la Israel huko Beirut, mji mkuu wa Lebanon.Siku ya Jumatano jioni, kundi linaloungwa mkono na Iran lilisema mwili wa Fuad Shukr ulipatikana kwenye vifusi vya jengo ambalo lilishambuliwa siku ya Jumanne.Watu wengine wanne waliuawa katika shambulizi hilo, wakiwemo watoto wawili. Awali, jeshi la Israel lilisema Shukr alikuwa akilengwa “kuuawa na ujasusi” .Israel iliongeza kuwa shambulizi hilo lilikuwa jibu kwa shambulio la roketi ambalo liliua watu 12 katika Milima ya Golan inayokaliwa na Israel siku ya Jumamosi, ambayo Israel inasema kamanda huyo alisaidia katika masuala ya kupanga.Hezbollah imekanusha kuhusika na shambulizi hilo.Fuad Shukr, ambaye alikuwa na umri wa miaka sitini, anaaminika kuwa mshauri mkuu wa kijeshi wa kiongozi wa Hezbollah Hassan Nasrallah.Shambulizi hilo lililenga jengo moja huko Haret Hreik, sehemu ya kitongoji cha Dahiyeh cha Beirut.Ni eneo lenye watu wengi. Dahiyeh yenyewe imezungukwa na vituo vya ukaguzi vya Hezbollah.Watoto waliouawa katika shambulizi hilo la anga ni mvulana wa miaka 10 na dada yake mwenye umri wa miaka sita.Shukr atazikwa siku ya Alhamisi, taarifa hiyo ilisema.Soma zaidi:Israel imethibitisha kufanya shambulizi la kulipiza kisasi nchini LebanonHezbollah ni nini huko Lebanon na itaingia vitani na Israeli?Tunachojua kuhusu kijiji cha Syria kinachoweza ‘kuchochea vita kati ya Israel na Hezbollah’ - Kijana, 17, ashtakiwa kwa mauaji ya wasichana watatu Uingereza
CHANZO CHA PICHA,PICHA ZA FAMILIAKijana wa miaka 17 ameshtakiwa kwa mauaji ya wasichana watatu katika hafla ya kucheza densi huko Southport.Bebe King, 6, Elsie Dot Stancombe, 7, na Alice Dasilva Aguiar mwenye umri wa miaka tisa walifariki dunia baada ya kushambuliwa kwa kisu kwenye hafla iliyopewa jina Taylor Swift katika mji wa Merseyside siku ya Jumatatu.Kijana huyo, ambaye anatazamiwa kufikishwa katika mahakama ya jiji la Liverpool baadaye Alhamisi, pia ameshtakiwa kwa makosa 10 ya kujaribu kuua.Watoto wengine wanane na watu wazima wawili waliokuwa kwenye hafla hiyo walijeruhiwa, huku baadhi yao wakiaminika kuwa bado katika hali mbaya.Mshitakiwa ambaye jina lake haliwezi kutajwa kwa sababu ya umri wake pia amefunguliwa shtaka la kumiliki kifaa chenye makali.Polisi wa Merseyside walitangaza mashtaka hayo wakati wa mkutano na waandishi wa habari mara tu baada ya saa sita usiku.Soma zaidi:Shambulizi la kisu laua watoto wawili na tisa kujeruhiwa katika warsha yao ya kucheza - Watatu wanaotuhumiwa kupanga njama ya 9/11 wafikia makubaliano ya kukiri mashtaka – Pentagon
CHANZO CHA PICHA,GETTY IMAGES - Wanaume watatu kati ya wanaotuhumiwa kupanga mashambulizi ya kigaidi ya Septemba 11, 2001 wameingia katika makubaliano ya kabla ya kesi, Idara ya Ulinzi ya Marekani imesema.Khalid Sheikh Mohammad, Walid Muhammad Salih Mubarak Bin Attash, na Mustafa Ahmed Adam al-Hawsawi wamezuiliwa katika kambi ya Jeshi la Wanamaji la Marekani Guantanamo Bay, Cuba, kwa miaka mingi bila kufikishwa mahakamani.Kwa mujibu wa vyombo vya habari vya Marekani, watu hao watakiri kuwa na hatia kwa makubaliano kuwa upande wa mashtaka ukubali kutoomba hukumu ya kifo.Masharti ya makubaliano hayo bado hayajatolewa.Takriban watu 3,000 huko New York, Virginia na Pennsylvania waliuawa katika mashambulizi ya al-Qaeda, ambayo yalisababisha “Vita dhidi ya Ugaidi” na uvamizi wa Afghanistan na Iraq.Mpango huo ulitangazwa kwa mara ya kwanza katika barua iliyotumwa na waendesha mashtaka kwa familia ya waathiriwa, kulingana na The New York Times.Hili lilikuwa shambulio baya zaidi kwenye ardhi ya Marekani tangu shambulio la mwaka 1941 la Japani kwenye Bandari ya Pearl, Hawaii, ambapo watu 2,400 waliuawa.“Kwa makubaliano ya kuondolewa kwa adhabu ya kifo kama adhabu inayowezekana kutolewa, washtakiwa hawa watatu wamekubali kukiri makosa yote yaliyokuwa yakishitakiwa likiwemo la mauaji ya watu 2,976 waliotajwa kwenye hati ya mashtaka,” ilisema barua hiyo kutoka kwa mwendesha mashtaka mkuu, Admiral Aaron Rugh.Watu hao wametuhumiwa kwa msururu wa mashtaka, ikiwa ni pamoja na kushambulia raia, mauaji kinyume na sheria za vita, utekaji nyara na ugaidi.Wanatarajiwa kuwasilisha maombi yao rasmi mahakamani mapema wiki ijayo.
- Ni eneo lenye watu wengi. Dahiyeh yenyewe imezungukwa na vituo vya ukaguzi vya Hezbollah.Watoto waliouawa katika shambulizi hilo la anga ni mvulana wa miaka 10 na dada yake mwenye umri wa miaka sita.Shukr atazikwa siku ya Alhamisi, taarifa hiyo ilisema.Soma zaidi:Israel imethibitisha kufanya shambulizi la kulipiza kisasi nchini LebanonHezbollah ni nini huko Lebanon na itaingia vitani na Israeli?Tunachojua kuhusu kijiji cha Syria kinachoweza ‘kuchochea vita kati ya Israel na Hezbollah’
- Saa 2 zilizopitaKijana, 17, ashtakiwa kwa mauaji ya wasichana watatu Uingereza
CHANZO CHA PICHA,PICHA ZA FAMILIA - Kijana wa miaka 17 ameshtakiwa kwa mauaji ya wasichana watatu katika hafla ya kucheza densi huko Southport.Bebe King, 6, Elsie Dot Stancombe, 7, na Alice Dasilva Aguiar mwenye umri wa miaka tisa walifariki dunia baada ya kushambuliwa kwa kisu kwenye hafla iliyopewa jina Taylor Swift katika mji wa Merseyside siku ya Jumatatu.Kijana huyo, ambaye anatazamiwa kufikishwa katika mahakama ya jiji la Liverpool baadaye Alhamisi, pia ameshtakiwa kwa makosa 10 ya kujaribu kuua.Watoto wengine wanane na watu wazima wawili waliokuwa kwenye hafla hiyo walijeruhiwa, huku baadhi yao wakiaminika kuwa bado katika hali mbaya.Mshitakiwa ambaye jina lake haliwezi kutajwa kwa sababu ya umri wake pia amefunguliwa shtaka la kumiliki kifaa chenye makali.Polisi wa Merseyside walitangaza mashtaka hayo wakati wa mkutano na waandishi wa habari mara tu baada ya saa sita usiku.Soma zaidi:Shambulizi la kisu laua watoto wawili na tisa kujeruhiwa katika warsha yao ya kucheza densi
- Watatu wanaotuhumiwa kupanga njama ya 9/11 wafikia makubaliano ya kukiri mashtaka – Pentagon
CHANZO CHA PICHA,GETTY IMAGES - Wanaume watatu kati ya wanaotuhumiwa kupanga mashambulizi ya kigaidi ya Septemba 11, 2001 wameingia katika makubaliano ya kabla ya kesi, Idara ya Ulinzi ya Marekani imesema.Khalid Sheikh Mohammad, Walid Muhammad Salih Mubarak Bin Attash, na Mustafa Ahmed Adam al-Hawsawi wamezuiliwa katika kambi ya Jeshi la Wanamaji la Marekani Guantanamo Bay, Cuba, kwa miaka mingi bila kufikishwa mahakamani.Kwa mujibu wa vyombo vya habari vya Marekani, watu hao watakiri kuwa na hatia kwa makubaliano kuwa upande wa mashtaka ukubali kutoomba hukumu ya kifo.Masharti ya makubaliano hayo bado hayajatolewa.Takriban watu 3,000 huko New York, Virginia na Pennsylvania waliuawa katika mashambulizi ya al-Qaeda, ambayo yalisababisha “Vita dhidi ya Ugaidi” na uvamizi wa Afghanistan na Iraq.Mpango huo ulitangazwa kwa mara ya kwanza katika barua iliyotumwa na waendesha mashtaka kwa familia ya waathiriwa, kulingana na The New York Times.Hili lilikuwa shambulio baya zaidi kwenye ardhi ya Marekani tangu shambulio la mwaka 1941 la Japani kwenye Bandari ya Pearl, Hawaii, ambapo watu 2,400 waliuawa.“Kwa makubaliano ya kuondolewa kwa adhabu ya kifo kama adhabu inayowezekana kutolewa, washtakiwa hawa watatu wamekubali kukiri makosa yote yaliyokuwa yakishitakiwa likiwemo la mauaji ya watu 2,976 waliotajwa kwenye hati ya mashtaka,” ilisema barua hiyo kutoka kwa mwendesha mashtaka mkuu, Admiral Aaron Rugh.Watu hao wametuhumiwa kwa msururu wa mashtaka, ikiwa ni pamoja na kushambulia raia, mauaji kinyume na sheria za vita, utekaji nyara na ugaidi.Wanatarajiwa kuwasilisha maombi yao rasmi mahakamani mapema wiki ijayo, gazeti la Times liliripoti.Soma zaidi:Shambulio la Septemba 11:Fahamu sababu za kisayansi zilizosababisha kuanguka kwa ‘Twin Towers’Shambulio la Septemba 11: Yafahamu Matukio matano yaliyoitikisa MarekaniMashambulio ya Septemba 11: Hiki ndicho kilichotokea dakika baada ya nyingine siku hiyoShambulio la Septemba 11: Milima ya ajabu iliyomficha Osama Bin Laden dhidi ya Marekani na Soviet .
WIMBI LA SIASA ZA MAREKANI
Donald Trump ametilia shaka utambulisho wa rangi wa Kamala Harris wakati wa mahojiano makali kwenye kongamano la waandishi wa habari weusi.
Trump alidai kwa uongo kuwa makamu wa rais na mgombea mtarajiwa chama cha Democratic alikuwa ameshikilia utambulisho wake wa Mmarekani mwenye asili ya Kihindi hadi hivi majuzi ambapo, alidai, “kuwa mtu mweusi”.
“Sikujua kuwa alikuwa mweusi hadi miaka kadhaa iliyopita alipobadilika kuwa mweusi na sasa anataka kujulikana kama mtu mweusi,” alisema katika kongamano la Chama cha Kitaifa cha Wanahabari Weusi huko Chicago Jumatano.
“Kwa hiyo sijui – ni Mhindi? Au ni mweusi?”
Bi Harris alisema matamshi ya Trump ni “mtazamo ule ule wa zamani” wa “kugawanya watu … na kutowaheshimu”.
“Watu wa Marekani wanastahili kiongozi bora zaidi,” alisema hilo katika mkutano wa Sigma Gamma Rho huko Houston. “Tunastahili kiongozi ambaye anaelewa kuwa tofauti zetu hazitugawanyi – ni chanzo muhimu cha umoja wetu.”
Bi Harris ndiye makamu wa rais wa kwanza mweusi na mwenye asili ya Kihindi, akiwa na wazazi wazaliwa wa India na Jamaica. Alihudhuria Chuo Kikuu cha Howard, chuo kikuu cha watu weusi kihistoria, na kujiunga umoja wa wanawake weusi wa vyuo vikuu uitwao Alpha Kappa Alpha .
Alikuwa mwanachama wa muungano wa wabunge weusi (Congress Black Caucus) baada ya kuingia katika Seneti mnamo 2017.
Kauli hiyo ya Trump ilizua mabishano makali kati yake na mwandishi wa ABC News Rachel Scott, mmoja wa wasimamizi wa hafla hiyo ya Chicago.
“Ninaheshimu upande wowote,” Mrepublican huyo alisema akimaanisha utambulisho wa rangi ya Harris. “Lakini yeye hafanyi hivyo kwa sababu alikuwa Mhindi wakati wote na ghafla akageuka na kuwa mtu mweusi.”
Katibu wa waandishi wa habari wa Ikulu ya White House, Karine Jean-Pierre alisema hakuna mtu “aliye na haki yoyote ya kumwambia mtu yeye ni nani, jinsi anavyojitambulisha. Hiyo sio haki ya mtu yeyote.”
“Nani alimteua Donald Trump kuamua yupi ni mtu mweusi na asiyekuwa mweusi?” aliuliza Mwakilishi Ritchie Torres wa New York. Alimtaja Trump kama “Kumbusho la zamani la taasubi za kibaguzi”.
Mgombea huyo wa chama cha Republican na rais wa zamani ana historia ya kuwashambulia wapinzani wake kwa misingi ya rangi.
Alidai bila ya kuwa na ushahidi kwamba Barack Obama, rais wa kwanza mweusi wa nchi hiyo, hakuzaliwa Marekani.
Trump alimshambulia balozi wa zamani wa Umoja wa Mataifa na mpinzani wake mkuu wa chama cha Republican Nikki Haley kwa kudanganya kuwa hawezi kuwa rais kwa sababu wazazi wake hawakuwa raia wa Marekani alipozaliwa.
Bi Harris amekabiliwa na msururu wa mashambulizi tangu apendekezwe kuwa mgombea wa chama cha Democratic. Warepublican wamekosoa uamuzi huo, wakisema alichaguliwa tu kwa sababu ya rangi yake.
Tim Burchett, mbunge wa chama cha Republican kutoka Tennessee, alimwita “makamu wa rais wa DEI” – akiashiria programu za kuleta,usawa na ujumuishi.
Siku ya Jumatano, Scott alimtaka Trump kufafanua ikiwa anaamini Bi Harris alikuwa “mwandani wa DEI”. Alijibu: “Kwa kweli sijui, huenda akawa.”
Bi Harris ameelezea jinsi alivyojivunia asili yake ya Kihindi na kwamba mara nyingi alitembelea nchi hiyo.
Mama yake pia aliwakuza binti zake wawili katika utamaduni wa watu weusi wa Oakland, California – ambako alilelewa, alisema.

Trump alishambulia pia sifa za kufuzu za Bi Harris wakati wa majadiliano, akisema alifeli mtihani wake wa uanasheria mwanzoni katika taaluma yake ya uwakili. Kauli ambayo ilipokelewa na manung’uniko kutoka kwa umati uliohudhuria .
“Nawaambia ukweli tu. Hakufaulu mtihani wake wa uwakili na hakufikiria kuwa angefaulu na hakufikiria kuwa angeweza kufaulu na sijui nini kilitokea. Labda alipitishwa, “alisema.
Bi Harris alihitimu kutoka Chuo Kikuu cha California Hastings,Chuo cha Sheria mwaka 1989. The New York Times liliripoti kwamba alishindwa jaribio lake la kwanza na akafaulu katika la pili.
Mamlaka ya mahakama ya serikali ya jimbo la California inasema chini ya nusu ya wale wanaofanya mtihani huo hufaulu katika jaribio la kwanza.
Majadiliano ya Chicago yalianza na mabishano kati ya Scott na rais huyo wa zamani. Trump alimshutumu mwanahabari huyo kwa kutoa “kutambuliusha vibaya sana” alipoanza mazungumzo akiuliza juu ya ukosoaji wake wa zamani wa watu weusi.
Alimnukuu Trump akiyaita maswali ya waandishi wa habari weusi kuwa ”ya kijinga na ya kibaguzi” na kwamba ”alikula chakula cha jioni na mzungu mwenye ubabe katika makazi yake ya Mar a Lago”.
“Ninawapenda watu weusi wa nchi hii, nimefanya mengi kwa watu weusi wa nchi hii,” alijibu.
Rais huyo wa zamani alikosoa mazungumzo hayo saa chache baadaye kwenye mtandao wake wa kijamii. “Maswali yalikuwa ya kijeuri na mabaya, mara nyingi katika mfumo wa taarifa, lakini tuliiponda!” alisema.
Maelezo zaidi:
NCHINI KENYA

SERIKALI ya Rais William Ruto imepata pigo kuu la kihistoria baada ya mahakama ya rufaa kuharamisha Sheria ya Fedha ya 2023.
Sasa Ruto atatumia Sheria ya Fedha ya Serikali ya Rais mstaafu Uhuru Kenyatta kukusanya ushuru wa kufadhili huduma za serikali ya Kenya Kwanza.
Kufuatia kuharamishwa kwa sheria hii ya Fedha ya 2023, sheria ya makato ya nyumba (housing levy) ni haramu kwa vile yanatokana na sheria hii iliyopigwa kalamu.
Majaji Kathurima M’Minoti, Agnes Murgor na John Mativo waliharamisha sheria hii ya Fedha ya 2023 wakisema inakinzana na Katiba.
Uamuzi huu wa majaji hawa umeletea afueni Wakenya waliokandamizwa na kuongezwa kwa ushuru wa mafuta kutoka asilimi mia nane (8) hadi kumi sita (16).
Majaji hawa wa mahakama ya pili kwa ukuu nchini walisema utaratibu uliopelekea kupitishwa kwa Sheria ya Fedha 2023 ulikaidi Katiba, umepotoka na hauna mashiko kisheria.
“Baada ya kutathmini mawasilisho ya Seneta Okiya Omtatah na walalamishi wengine, tumefikia uamuzi kwamba kupitishwa na kutiwa sahihi kwa Sheria ya Fedha 2023 kulikiuka Vifungu vya Katiba 220 (1) (a) na 221 pamoja na sehemu nambari 37, 39A, na 40 vinavyotoa utaratibu na mwelekeo wa kuandaliwa kwa Sheria ya Fedha,” majaji hao walisema.
Kukaidiwa kwa utaratibu na mwongozo uliowekwa umetweza na kupotoka.
Hivyo basi majaji hao walisema Sheria ya Fedha 2023 inakiuka katiba na haina mashiko na kamwe na “imeharamishwa.”
Majaji Kathurima, Murgor na Mativo walisema kesi ya Bw Omtatah imethibitisha kwamba Sheria ya Fedha ya 2023 ni kinyume cha sheria na kamwe haipasi kutumika kuwatoza wananchi ushuru.
Sasa ni afueni kwa wananchi kwa kuwa Sheria ya Fedha ya 2024/2025 iliondolewa na Rais William Ruto kufuatia maandamano ya Gen Z na sasa ile ya 2023/2024 imeharamishwa pia.
Wananchi sasa watatozwa ushuru kulingana na sheria ya Rais Mstaafu Uhuru Kenyatta.
Kenya Kwanza
Okiya Omtatah
ruto
Sheria ya Fedha 2023
uhuru

UHASAMA wa kisiasa katika Kaunti ya Meru ulitokota zaidi Jumatano baada ya diwani kuwasilisha hoja ya tano ya kumtimua Gavana Kawira Mwangaza uongozini.
Hoja hiyo iliwasilishwa katika bunge la kaunti na diwani mteule Zipporah Kinya. Hii ilikuwa hoja ya tano baada ya ile ya nne kuwasilishwa mnamo Jumanne.
Aidha hoja ya Jumatano iliwasilishwa siku mbili baada ya Bi Mwangaza kupata afueni kufuatia mahakama kuamua mzozo kati yake na madiwani uwasilishwe kwa Baraza la Wazee wa Njuri Ncheke.
Bi Kinya, ambaye ni Naibu Kiongozi wa Wengi Bunge la Kaunti ndiye aliondoa hoja ya kumtimua Bi Mwangaza mnamo Jumanne katika kile kilichoonekana kukwepa mitego au vizingiti vya kisheria.
Katika hoja ya Jumatano, Bi Kinya alisema kuwa gavana huyo anastahili kuondolewa afisini kwa kukiuka katiba na pia matumizi mabaya ya afisi.
“Kuendelea kukaa kwake afisini kumetia doa utoaji wa huduma na kulemaza matarajio ya wakazi wa kaunti,” akasema Bi Kinya.
Baada ya kuwasilishwa kwa hoja hiyo, Bi Mwangaza aliandika kwenye ukurasa wake wa Facebook kuwa ana matumaini atatatamba kwa mara nyingine baada ya majaribio ya nyuma ya kumbandua kufeli.
“Hoja hiyo imekufa hata kabla haijajadiliwa,” akasema Bi Mwangaza.
Wakili wa Gavana Mwangaza, Bw Elias Mutuma alionya bunge la kaunti dhidi ya kuwasilisha mswada huo akisema ni kukiuka amri korti. Hata hivyo, wakili wa bunge la kaunti Ndegwa Njiru alisema hakukuwa na amri yoyote inayoizua kaunti kuwasilisha hoja mpya ya kumtimua gavana.
Katika hoja mpya baadhi ya masuala ambayo yalikuwa katika hoja ya mwanzo yameondolewa. Kati ya masuala hayo ni kutimuliwa kwa mshauri wa masuala ya kisheria wa gavana na pia kuajiriwa kwa mwanasheria mkuu wa kaunti bila idhini ya bunge la kaunti.
Diwani huyo amesema gavana alikiuka sheria kwa kubatilisha uteuzi wa Katibu wa Bodi ya Kaunti Virginia Kawira, kukataa kuwateua wanaoshikilia uenyekiti wa bodi mbalimbali na kukataa kutekeleza mapendekezo ya kaunti.
Makosa mengine ni kuwatimua wakuu wa bodi na kuhadaa umma kutokana na kudai kuwa madiwani walikuwa wamechangisha Sh86 milioni kwa familia ya bloga marehemu Bernard Muthiani maarufu kama Sniper.
Pia Bi Mwangaza amelaumiwa kwa kulipa bila kufuata sheria Sh74.3 milioni kama marupurupu kwa madaktari, kuwaajiri wafanyakazi 111 ambao wanahudumu kwenye afisi yake. Kuajiriwa kwa wafanyakazi hao kulichangia gharama ya kaunti kupanda kwa Sh500 milioni kisha Sh103 milioni kulipwa nje ya mfumo wa kawaida wa ulipaji mshahara.
Kama hayo hayatoshi gavana amelaumiwa kwa kulipa Afisa wa Mawasiliano Christus Manyara mshahara ilhali alikuwa ameshtakiwa kwa mauaji, kulipwa kwake kukienda kinyume na mwongozo wa ulipaji wa watumishi wa umma.
Mahakama ilikuwa imeamrisha mzozo kati ya gavana utatuliwe na Njuri Ncheke lakini baraza hilo la wazee likajiondoa. Kamati iliyoteuliwa na Rais William Ruto kusikiza pande zote mbili kisha kuwasilisha ripoti yake imesema kuwa ishaandaa ripoti yake na inasubiri tu miadi na rais ili kuiwasilisha
Kawira Mwangaza
MERU
njuri ncheke
Zipporah Kinya
NDOANDOANO-MARRIAGE MATHEMATICS

MAAFISA wa polisi katika mji wa Kapenguria wameanzisha msako kuhusu tukio ambalo mwanaume mmoja anadaiwa kumua mkewe kisha baadaye akajinyonga kwenye mzozo wa nyumbani.
Wakazi wa kijiji cha Cherelio, eneo la Murkwijit katika kaunti ya Pokot Magharibi waliamka kwa mshangao Jumanne asubuhi kwa tukio la kutisha ambapo mwanaume huyo alimuua mkewe kisha akajitoa uhai.
Benjamin Morogo Mutai, 53, alimkata koo mkewe, Teresa Chepkemoi, 47, kwenye mzozo mkubwa. Miili ya wawili hao ilipatikana na majirani ambao walishuku kulikuwa na shida kwenye boma hilo.
Naibu wa Kamanda wa kaunti ndogo ya Pokot Magharibi Richard Omanga alithibitisha mkasa huo akisema kuwa uchunguzi unaendelea kubaini chanzo cha tukio hilo.
“Ilifanyika kutokana na mzozo wa nyumbani ambao ulienea. Tunafanya uchunguzi kujua kilichofanyika,” alisema.
Bw Omanga alisema kuwa, “Mwanaume alimdunga kisu mkewe kwenye kifua kisha akaaga dunia. Baada ya kutekeleza tukio hilo alijinyongea ndani ya nyumba. Tunashtumu vikali tukio hilo,” alisema akiongeza kusema kuwa wawili hao wamekuwa na mzozo wa nyumbani kwa muda mrefu.
Wakazi wa eneo la Murkwijit wameachwa na mshangao na huzuni huku wengi wakitaka hamasisho kuhusu suala la kutatua mizozo ya nyumbani.
Mike Kiprop, mtu wa ukoo wa familia hiyo alisimulia tukio hilo:
“Tulifika kwa boma na kupata mwanamke bado anapumua nje ya nyumba. Alikuwa anavuja damu mwili wote. Inaonekana mwanaume alimvamia akiwa nje kisha akaingia kwa nyumba na kujinyonga.”
“Tulimpeleka mke kwa hospitali tukiwa na imani ya kupona lakini alifariki tukiwa njiani.”
Sammy Moran, jirani anasema kuwa familia hiyo imekuwa na mizozo ya mara kwa mara.
“Familia hiyo imekuwa na mizozo mingi ya nyumbani ambayo iliwapaleka kwenye kituo cha polisi kusuluhisha,” alisema.
Bw Moran alisema kuwa alikerwa na kushangazwa na tukio hilo.
“Siamini kilichotokea. Tulikuwa kwenye kituo cha polisi tukifikiria tumesuluhisha mizozo. Nilimpigia simu mwanaume ikiwa angerudi kwenye kituo cha polisi Jumanne kuendelea na mazungumzo lakini niliamkia masaibu,” anasema.
Alisema kuwa watu wa ukoo walikuwa wamezuiwa kuingilia mzozo huo ambao hasa ulihusu kuuza kwa maziwa na mahindi.
Miili ya Benjamin Morogo Mutai na Teresa Chepkemoi ilipelekwa katika hospitali ya rufaa ya kaunti ya Kapenguria kufanyiwa uchunguzi.
Wakazi wanataka hamasisho kuhusu masuala ya ndoa kufanyika na kutatua mizozo ya ndoa.
Bodaboda jijini Nairobi Nchini Kenya

SERIKALI ya Kaunti ya Nairobi imeweka mikakati ya kudhibiti sekta ya bodaboda ambayo ni jukwaa la kibiashara na ajira kwa wafanyakazi wengi.
Afisa Mkuu wa Masuala ya Usalama, Tony Kimani Jumatano alisema kuwa kuna mipango ambayo kaunti imekuwa ikiendelea nayo ya kupunguza idadi ya wahudumu wa bodaboda katikati mwa jiji.
Bw Kimani alisema kaunti ina wahudumu wa bodaboda 700 ambao wamesajiliwa na wamekuwa wakihudumu katikati mwa jiji kila siku. Alisema idadi hiyo ni ya juu zaidi na si rahisi kudhibiti.
Aidha, idadi hiyo inaweza kuwa ya juu zaidi kwa sababu kuna wahudumu wa bodaboda ambao wanafanya kazi katikati mwa jiji kinyume cha sheria.
Afisa huyo aliongeza kuwa, kuna hatua ambazo zinahitajika kuhakikisha idadi ya wahudumu wa bodaboda inapungua hadi 300, malengo ambayo wameweka japo si rahisi kufikiwa.
“Kama serikali ya kaunti lazima tupunguze idadi ya wahudumu wa bodaboda katikati mwa jiji. Najua hiki ni kibarua kigumu lakini tutapambana na kuafikia kile ambacho tunakilenga,” akasema Bw Kimani.
Jinsi ilivyo kwa sasa, kaunti haina sheria au mwongozo ambao unadhibiti au kusimamia sekta ya uchukuzi wa bodaboda nchini.
Kaunti hata hivyo, imekanusha kuwa inawatimua wahudumu wa bodaboda jijini kutokana na wimbi la maandamano ambalo limekuwa likishuhudiwa nchini.
Pia, kaunti imesema kuna maafisa maalum ambao watakuwa wakisimamia sekta ya bodaboda na wanastahili kuwanyaka wale ambao wanaendeleza shughuli zao kinyume cha sheria.
“Si afisa yeyote katika serikali ya kaunti hasa katika idara ya usalama ataruhusiwa kumnyaka mhudumu wa bodaboda katikati mwa jiji. Kuna maafisa ambao wametengewa majukumu hayo katika barabara mbalimbali,” akaongeza Bw Kimani.
Bw Sakaja alipoingia mamlakani mnamo 2022, aliwaruhusu wahudumu wa bodaboda wafanye kazi katikati mwa jiji.
MABADILIKO YA UONGOZI WA ODM BUNGENI

CHAMA cha ODM Jumatano kilitekeleza mabadiliko kwenye uongozi wake bungeni huko Kinara wake Raila Odinga akiwatunuku wandani wake kutoka Nyanza na Magharibi nyadhifa muhimu katika Bunge la Kitaifa.
Kufuatia kuteuliwa Kiongozi wa Wachache Opiyo Wandayi kama waziri mteule wa Kawi, nafasi yake bungeni jana ilipewa mbunge wa Suna Mashariki Junet Mohamed ambaye alikuwa kati ya wasimamizi wa kampeni za Bw Odinga mnamo 2022.
Kabla ya uteuzi huo, Bw Mohamed alikuwa akihudumu kama kiranja wa wachache.
Mabadiliko hayo yalitangazwa na Katibu Mkuu wa ODM Edwin Sifuna baada ya mkutano wa Baraza Kuu la Chama (NEC) ulioandaliwa jijini Nairobi. Nafasi ya Bw Mohamed nayo ilitunukuwa mbunge wa Suba Kaskazini Millie Odhiambo.
Katika kamati za bunge, Mbunge wa Saboti Caleb Amisi atakuwa mwenyekiti mpya wa kamati ya hadhi ya Uhasibu Bungeni. Bw Amisi amemrithi mbunge maalum John Mbadi ambaye ameteuliwa waziri wa fedha kwenye mabadiliko yaliyotangazwa na Rais William Ruto majuma mawili yaliyopita.
Kama sehemu ya kutunuku Kaunti ya Busia ambayo ni ngome yake ya kisiasa, Mbunge wa Funyula Oundo Mudenyo amepewa wadhifa wa Naibu Mwenyekiti wa Kamati ya Uwekezaji Bungeni (PIC).
Hata hivyo, ODM bado haijajaza nafasi mbili za naibu kiongozi wa chama na pia ile ya uenyekiti iliyokuwa ikishikiliwa na Bw Mbadi. Magavana wa zamani Hassan Joho (Mombasa) na Wycliffe Oparanya (Kakamega) ambao walikuwa wakihudumu kama naibu kiongozi wa ODM ni mawaziri wateule wa Madini na Vyama vya Ushirika na Biashara Ndogo Ndogo.
Ubabe wa kisiasa hasa umeanza kushuhudiwa katika wadhifa wa uenyekiti huku mbunge wa Homa Bay Mjini Opondo Kaluma akisema wadhifa huo uliokuwa ukishikiliwa na Bw Mbadi lazima usalie Kaunti ya Homa Bay.
Hata hivyo, uteuzi wa Bw Mbadi kama waziri kisha Bi Odhiambo kama kiranja wa wachache, wote kutoka Homa Bay sasa unadidimiza matumaini ya nafasi hiyo kusalia katika gatuzi hilo.
Mbunge wa Rarieda Otiende Amollo ambaye amekuwa akipigiwa upato kuwahi nyadhifa za Mwanasheria Mkuu au uenyekiti wa PAC, alitoka bure katika mabadiliko hayo.
Bw Amollo ambaye anatoka Kaunti ya Siaya sasa yupo pazuri kumrithi Bw Mbadi kama mwenyekiti wa ODM iwapo uongozi wa chama utaamua nafasi hiyo isalie Nyanza.
Tetesi za Soka Ulaya Alhamisi 01.08.2024

Saa 5 zilizopita
Joe Gomez bado anataka kuondoka Liverpool, Marseille wana bei ambayo wako tayari kulipa kumpata Eddie Nketiah, Palace wako tayari kumruhusu Jordan Ayew kuondoka.
Beki wa Liverpool na England Joe Gomez, 27, yuko tayari kuondoka msimu huu wa joto baada ya uhamisho wa kwenda Newcastle kugonga mwamba mwezi uliopita. (Mail)
Marseille wako tayari kulipa takriban euro milioni 17 kumpata mshambuliaji wa Arsenal Muingereza Eddie Nketiah, 25, huku mazungumzo yakitarajiwa kuendelea kati ya klabu hizo siku zijazo. (Telegraph)
Crystal Palace wameonyesha nia ya kumruhusu mshambuliaji Jordan Ayew mwenye umri wa miaka 32 kuondoka msimu huu wa joto, huku Leicester wakipania kumsajili mchezaji huyo wa kimataifa wa Ghana. (Standard)

Everton wanavutiwa na mshambuliaji wa Paraguay Ramon Sosa, 24, lakini wanakabiliwa na ushindani kutoka kwa Nottingham Forest katika jitihada zao za kumsajili kutoka CA Talleres. (Team talk)
Chelsea huenda wakalazimika kupunguza bei yao ikiwa wanataka kukubaliana na Atletico Madrid kuhusu mauzo ya kiungo wa kati wa Uingereza Conor Gallagher. Klabu hizo zimetofautiana kwa £20m katika tathmini zao. (Mail)
Leeds wametoa ofa ya pauni milioni 2.5 kwa winga wa Fenerbahce Muingereza Ryan Kent, 27. Jose Mourinho ana nia ya kumsajili mchezaji huyo wa zamani wa Rangers. (Haber Ekspres – kwa Kituruki)
Paris St-Germain wamekubali kumsajili kiungo wa kati wa Benfica na Ureno Joao Neves, 19, kwa euro nilioni 60, pamoja na nyongeza ya euro milioni 10, huku kiungo wa kati wa Ureno Renato Sanches, 26, akihamia njia upande mwingine kwa mkopo. (Fabrizio Romano)
Nottingham Forest inatazamiwa kumsajili winga wa Ureno mwenye umri wa miaka 24 Jota Silva kutoka Vitoria Guimaraes kwa euro milioni saba, katika mkataba ambao pia unajumuisha nyongeza ya hadi euro milioni tano. (Sky Sports)

Wolves na Fulham wamejiunga na kinyang’anyiro cha kumsajili beki wa Ufaransa mwenye umri wa miaka 21 Isaak Toure kutoka Lorient. (Football Insider)
Fulham wamekubali dili la kumsaini beki wa Uhispania Jorge Cuenca, 24, kutoka Villarreal. (Fabrizio Romano)
Coventry City wamejizatiti katika mpango wa Hull City wa pauni milioni 2.5 kumsaini mshambuliaji wa Ghana Brandon Thomas-Asante, 25, kutoka West Brom. (Telegraph)
All Rights Reserved © Cantona Group Ltd||2024
Discover more from cantonadigital
Subscribe to get the latest posts sent to your email.