Mipango ya Mungu.

MUNGU alimuandaa Musa kwa miaka themanini, ili aweze kumtumia kwa muda wa miaka arobani. Miaka arobani ya kwanza alikuwa anapata elimu ya kimwili ndani nyumba ya Farao, yaani kuanzia chekechea mpaka chuo kikuu, kisha kupata elimu ya kijeshi hadi kufikia rank ya mwana wa binti farao. Katika wakati wote huo hakumjua Mungu Bali aliijua zaidi miungu ya ki Misri, hadi hapo BWANA alipomuondoa kwenye nyumba ya Farao na kumpeleka Midiani kwa Kuhani Yethro na kufundishwa elimu ya rohoni kwa muda wa miaka mingine arobaini. Hatua hii ya kutoka Misri hadi Midiani kwa Musa ilikuwa ni kama kupoteza muelekeo, huku ndoto zake zikiwa zimeshavurugika lakini katika hali hiyo bado ulikuwa ni mpango wa MUNGU wa kumuandaa kwa ajili ya kazi ya uongozi, ili awe kiongozi anayejua maisha yote ya shida na raha. Lakini pia Mungu alimuandaa Yesu kwa muda wa miaka thelasini ili aweze kuja kuifanya kazi kwa miaka mitatu tu. Usimdharau mtu yeyote wala usikate tamaa katika hali yeyote bali tambua kuwa ni Mungu anakuandaa….

FortuneBaraka Photography

Discover more from cantonadigital

Subscribe to get the latest posts sent to your email.

Leave a comment