Radio Fortune Africa
https://zeno.fm/radio/radio-fortune-africa

RADIO FORTUNE AFRICA
- HABARI KUU
- KIPENGA CHA MICHEZO
- MAKALA MAALUM
- AFYA NA JAMII
- UKWELI NA BURUDANI
- VIDEO KALI
- VIPINDI VYA RADIO
Tetesi za soka Ulaya Jumamosi 27.07.2024

27 Julai 2024, 07:50 EAT
Imeboreshwa Kipenga Cha Michezo
Miamba ya soka la England klabu ya Manchester City inapanga kumfanya kiungo wa klabu ya Bayern Munich na timu ya taifa ya Ujerumani Jamal Musiala, 21, kuwa mrithi wa kiungo mchezeshaji wao Kevin de Bruyne, 33. (CaughtOffside)
Barcelona wamefikia makubaliano ya kumsajili winga wa klabu ya Athletic Bilbao na timu ya taifa ya Uhispania Nico Williams, 22, kwa mkataba wa miaka mitano, ambao pia utakuwa na kipengele cha nyongeza ya mwaka mmoja. (Nicolo Schira)
Tottenham ipo mbele ya Liverpool na Arsenal katika kinyang’anyiro cha kumsajili winga wa klabu ya Juventus na timu ya taifa ya Italia Federico Chiesa, 26. (Football Transfers)Soma zaidi:
- ‘Mashabiki wa Arsenal walinihukumu kwa bei, sio uwezo wangu wa mpira’ – Nicholas Pepe26 Julai 2024
- Tetesi za soka Ulaya Ijumaa 26.07.202426 Julai 2024

Klabu ya Arsenal inataka kulipwa dau la walau euro milioni 50 (pauni 42m) ili kumuuza mshambuliaji wao raia wa Uingereza Eddie Nketiah, 25, ambaye mpaka sasa ameivutia klabu ya Ufaransa ya Marseille. (La Provence – in French)
Kipenga Cha Michezo -Tetesi za Soka Ulaya
Newcastle United wana imani kuwa winga wao Anthony Gordon atasalia kwenye klabu hiyo licha ya kufuatiliwa na Liverpool. (Team Talk)
West Ham wanajipanga kuongeza dau ili kumnasa mshambuliaji Jhon Duran, 20, kutoka Colombia ambaye klabu yake ya sasa Aston Villa inataka pauni milioni 40 ili kumuachia. (Standard)

Manchester United wamerejea katika mbio za kutaka kumsajili beki wa Bayern Munich na timu ya taifa ya Morocco Noussair Mazraoui, 26, baada ya mipango yake ya kuhamia West Ham kushindikana. (Sky Germany)
Mazraoui anatazamiwa kutaka kuhakikishiwa kuwa atapata muda wa kutosha wa kucheza kabla ya kukubali kujiunga na United. (Manchester Evening News)
Tottenham wapo kwenye mazungumzo na klabu ya Girona ili kuwauzia mshambuliaji wao raia wa Uhispania Bryan Gil, 23, ambaye tayari ameshaafikiana na Girona kuhusu maslahi yake binafsi. (Fabrizio Romano)

Manchester United wamefanya mazungumzo kuhusu uwezekano wa kubadilishana beki wao Aaron Wan-Bissaka, 26, na Denzel Dumfries, 28, kutoka Inter Milan. (Telegraph – subscription required)
Chelsea wanajiandaa kuwaruhusu wachezaji 12 kuondoka katika klabu hiyo kwenye dirisha hili la usajili baada ya mkataba wa beki wao raia wa Ufaransa Malang Sarr, 25, kuvunjwa ili kumuwezesha kujiunga na klabu ya RC Lens. (Sun)

Los Angeles FC wamepiga hatua katika mazungumzo yao kutaka kumsajili mshambuliaji wa klabu ya Atletico Madrid na timu ya taifa ya Ufaransa Antoine Griezmann, 33. (L’Equipe – in French)
Klabu hiyo inayocheza ligi ya Marekani (MLS) pia wapo karibu kumsajili kwa mkopo kiungo raia wa Uingereza Lewis O’Brien, 25, kutoka katika klabu ya Nottingham Forest. (Football Insider)
AfrikaLeoWikendi #AfrikaMwishoJuma
KipengaChaMichezo #KipengaChaAfrika
ParisOlympics2024
Baadhi ya wanariadha kutoka Afrika walishiriki katika sherehe za ufunguzi wa Michezo ya Olimpiki ya Paris 2024 walipovuka Mto Seine na boti wakiwa na bendera zao.
Kwa mara ya kwanza katika historia ya Michezo ya Olimpiki, ufunguzi rasmi wa mashindano haukufafanyika kwenye uwanja.
Jiji la Paris na hasa Mto Seine ulikuwa mandhari hai ya uzinduzi wa Michezo ya Olimpiki ya 2024.

















Mada zinazohusiana
Pia unaweza kusoma HABARI KUU
Sare za 9 za kuvutia zitakazovaliwa na wachezaji katika Olimpiki 202425 Julai 2024
Kutoka kukama maziwa ya ng’ombe hadi Man City – maisha ya Savinho24 Julai 2024
Kukimbia na ulemavu wa macho kumebadili maisha yangu baada ya kukanyaga bomu Afghanistan21 Julai 2024
Habari kuu DUNIANI
- Moja kwa moja,Sherehe ya ufunguzi ya mashindano ya Olimpiki 2024 yafanyika kwa mbwembwe mjini Paris
- ‘El Mayo’ Zambada na mtoto wa El Chapo: Je, ni walanguzi gani sugu wa dawa za kulevya wanaozuiliwa Marekani?26 Julai 2024
- Jinsi ya kuwashinda duma kukimbiaSaa 2 zilizopita
Gumzo mitandaoni Kote DuNIANI
Paris Olimpiki 2024: Wajue nyota wa kimataifa wa kuwatazama26 Julai 2024
Meli yenye bendera ya Tanzania yazama Taiwan
Kwa nini marafiki zako wanakufanya uishi maisha marefu zaidi25 Julai 2024
Vita vya Ukraine: Droni zafungua aina mpya ya vita vya baadaye25 Julai 2024
Maandamano Kenya: Waandamanaji wanakabiliwa na ukatili wa polisi23 Julai 2024
Je, kujiondoa kwa Biden kunamaanisha nini kwa Harris, Democrats na Trump?22 Julai 2024
Tanzania: Rais Samia awafukuza kazi Nape na Makamba22 Julai 2024
Trump na J.D Vance: Je ni kwanini nchi za Ulaya zinahofia kuingia mamlakani kwa wawili hawa?18 Julai 2024
Kwa nini Ruto hakuwa na chaguo bali kulivunja baraza la mawaziri?12 Julai 2024
Iliyosomwa zaidi KwiNgineKo
- 1Tetesi za soka Ulaya Jumamosi 27.07.2024
- 2Jinsi ya kuwashinda duma kukimbia
- 3Yafahamu mataifa 5 tajiri na masikini Barani Afrika 2024Imeboreshwa mwisho: 5 Machi 2024
- 4‘El Mayo’ Zambada na mtoto wa El Chapo: Je, ni walanguzi gani sugu wa dawa za kulevya wanaozuiliwa Marekani?
- Tetesi za Soka.
- Radio Fortune Africa
All Rights Reserved © Cantona Group Ltd||2024
Discover more from cantonadigital
Subscribe to get the latest posts sent to your email.