Jiandae kwa kipindi Cha Matumaini-Hii Ni Idhaa Ya Kiswahili Radio Fortune Africa.

https://zeno.fm/radio/radio-fortune-africa

Maombolezo 3:31-33


Kwa kuwa Bwana hatamtupa mtu
Hata milele.Maana ajapomhuzunisha atamrehemu,Kwa kadiri ya wingi wa huruma zake.Maana moyo wake hapendi kuwatesa wanadamu.
Wala kuwahuzunisha.

Nimehimizwa moyoni sana kuandika ujumbe huu siku ya leo na ninajua ni kwa ajili yako wewe unaesoma wakati huu,ujumbe huu hujakutana nao kwa bahati mbaya kuna chakwako hapa

Nimehimizwa moyoni kukukumbusha kwamba, Wewe na Mungu mmetoka mbali sana, na kama angekuwa mtu wa kukutupa angeshakutupa siku nyingi,kama angekuwa mtu wa kukuacha angeshakuacha siku nyingi

Lakini hajawahi kukuacha,hajawahi kukutupa na hawezi kukutupa kamwe wala hawezi kukuacha kamwe,ajapo kuhuzunisha atakurehemu kwa kadri ya wingi wa rehema zake,maana moyo wake haupendi kuwatesa wanadamu

Nimetumwa kukumbusha kwamba,kuna kipindi ulipita katika bonde la uvuli wa mauti mahali ambapo woote uliowategemea walikutupa,wengine wakakuacha na kukucheka

Lakini huyu Mungu hakukuacha,ulipolia alilia na wewe,wakati wa huzuni alikuwa faraja yako,wakati wa upweke alikuwa rafiki yako wa karibu na alikukumbatia na kukwambia mwanangu usiogope nipo pamoja na wewe

Kwanini umekata tamaa tena? Kwanini unaona kama Mungu amekuacha tena, kwanini unahisi kama Mungu amekutupa,kwanini umeruhusu moyo wako kuinama?

Niko hapa kukutia moyo wanaweza kukuacha woote lakini sio Mungu, wanaweza kukukimbia woote lakini sio Mungu,wanaweza kukuchukia wote lakini sio Mungu

Yupo pamoja na wewe, anakupenda na anakuwazia mema, na yeye ni msaada wako wa karibu atakutetea, atakutia nguvu na atakutengeneza na kukusimamisha tena katika jina la Yesu

Kama umepokea Neno hili mshukuru Bwana kwa maneno haya Asante Yesu kwa Upendo wako kwangu, wewe na Yesu mnahistoria kubwa,mmetoka mbali hawezi kukuacha njiani atakusaidia na kukuvusha tu kwa jina la Yesu.

Tufwatilie na like Facebook Page.

Radio Fortune Africa.

All Rights Reserved © Cantona Group Ltd||2024


Discover more from cantonadigital

Subscribe to get the latest posts sent to your email.

Leave a comment