Kushindwa kwako sio hauna nguvu la hasha, Ni kutokana kutokua ufahamu.

Radio Fortune Africa-Bao La Asubui

https://zeno.fm/radio/radio-fortune-africa

Na Cantona Joseph

Upo uhusiano mkubwa sana baina ya namna unavyofikiri na hali yako ya kimaisha au na jinsi unavyoishi.

Kushindwa kwako, hakutegemeani na nguvu yoyote uliyonayo isipokuwa ufahamu wako.

Kuanguka kwako hakutegemei maadui wengi ulionao, isipokuwa aina ya mtazamo ulionao.

Kurudi nyuma kwako hakutegemei historia yoyote uliyowahi kuwa nayo, isipokuwa namna unavyoendeleza mawazo yako ya kushindwa.

Naelewa kwamba panahitaji mjadala wa kina kuhusu kipi kinachomtawala mwenzie: mawazo yetu ndiyo yanayotuongoza ama ni sisi ndio tunayaongoza mawazo.

Hapo inapidi tushukie penye uelewa na namna mawazo yetu yanavyojengeka vichwani mwetu.

Kwa haraka haraka, nadhani, twawaza vile tulivyoviingiza ubongoni iwe kwa hiari yetu wenyewe ama pasipo hiari hiyo. Kwa maneno mengine sisi ndio watawala wa mawazo yetu.

Hiyo ni kusema kwamba unavyojiona, ndivyo ulivyo. Ukijidharau, hakuna mtu atakuja kukufanyia kazi ya kukuonyesha thamani uliyonayo.

Ukianza leo kujiona masikini, ni wazi kuwa akili yako itakubaliana nawe na kusema kweli, utakuwa umeukaribisha umasikini wako kwa mikono yako miwili.Unavyowaza ndivyo utakuja kuwa.

Ningependa kukuachia ujumbe huu Asubui ya leo;

Katika kila unalojaribu kulifanya, dhania kwamba haiwezekaniki jambo hilo likashindwa kwa namna yoyote.

Kwa sababu, haiwezekani ukashindwa katika jambo lolote, isipokuwa kama utakubali akilini mwako kwamba umeshindwa.

Achana na mawazo ya kushindwa shindwa. Achana na watu ambao hawaishiwi stori za ubaya ubaya. Amua kuyaelekeza mawazo yako kwenye mafanikio.

Kwa sababu mawazo yako ndiyo nguvu yako kuu uliyonayo! Itumie nguvu hiyo!

Jitamkie Asubui ya leo kwa imani “Nayaweza mambo yote katika yeye anitiae nguvu”

Watag marafiki zako wambie kwa imani,Lipo Tumaini hata kama wamejikatia tamaa wambie ” Unayaweza mambo yote katika yeye akutiae nguvu”
Salamu zangu ziwafikie wenyeji wa Karatu Arusha Nchini Tanzania.

All Rights Reserved © Cantona Group Ltd||2024


Discover more from cantonadigital

Subscribe to get the latest posts sent to your email.

Leave a comment