Radio Fortune Africa
https://zeno.fm/radio/radio-fortune-africa

Na Cantona Joseph

Maafisa wa uokoaji nchini Taiwan wanatafuta meli ya mizigo iliyokuwa na wafanyakazi tisa ambayo imezama kwenye pwani yake ya kusini.
Meli hiyo yenye bendera ya Tanzania ilikuwa imetoka katika bandari ya kusini ya mji wa Kaohsiung wakati Taiwan ilipokumbwa na kimbunga Gaemi.
Dhoruba hiyo pia imesababisha mvua isiyoisha nchini Ufilipino, ambapo meli ya mafuta iliyokuwa imebeba takriban lita milioni 1.5 za mafuta ya viwandani imepinduka.
Wafanyakazi kumi na sita wa MT Terra Nova yenye bendera ya Ufilipino wameokolewa huku mmoja akiwa bado hajapatikana, Katibu wa Uchukuzi Jaime Bautista alisema.
Mshirikishe mwenzako, Meli yenye bendera ya Tanzania yazama Taiwan
Saa 1 iliyopitaPolisi arekodiwa video akimkanyaga kichwani mtu kwenye uwanja wa ndege.
Afisa huyo anaonekana kumpiga teke mara kwa mara mtu huyo, ambaye amelala kifudifudi
Afisa wa polisi amerekodiwa akimpiga akimkanyaga kumpiga kichwani mwanamume alikuwa amelala chini kwenye Uwanja wa Ndege wa Manchester nchini Uingereza.
Afisa huyo wa kiume aliyevalia sare anaonekana akiwa ameshikilia silaha aina ya Taser ( kifaa kinachotumika kujilinda bila kusabaisha madhara) juu ya mwanaume huyo, ambaye amelala kifudifudi, kabla ya kumpiga mara mbili huku maafisa wengine wakiwapigia kelele watazamaji , katika video iliyosambazwa sana mtandaoni.
Polisi wa Greater Manchester (GMP) walisema maafisa wa bunduki walishambuliwa walipokuwa wakijaribu kumkamata mtu kufuatia mapigano yaliyotokea kwenye uwanja wa ndege siku ya Jumanne.
Hasira kuhusu video hiyo imeendelea kuongezekana mamia ya watu waliandamana nje ya kituo cha polisi huko Rochdale, Greater Manchester Jumatano kulaani kitendo hicho.
Mshirikishe mwenzako, Polisi arekodiwa video akimkanyaga kichwani mtu kwenye uwanja wa ndege

Waziri mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu atetea vita vya Gaza huku waandamanaji wakiandamana nje ya bunge la Marekani.
Katika hotuba ya kihistoria aliyoitoka kwa Bunge la Congress Waziri Mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu aliwaambia wabunge wa Marekani kuwa “maadui zetu ni adui zenu” .
Hotuba hiyo ililenga kutapata uungaji mkonowa Marekanikatika vita vya Gaza, lakini iliambatana na maandamano yaliyofanyika ndani na nje ya jengo la bunge la Capitol Hill.
“Tunapopigana na Iran, tunapambana na adui mkali zaidi, muuaji wa Marekani,” Bw Netanyahu alisema.
“Pambano letu ni pambano lenu, na ushindi wetu utakuwa ushindi wenu,” aliongeza,Maelfu waandamana huku Netanyahu akihutubia bunge la Marekani
Kiongozi huyo wa Israel alipata mapokezi makubwa kutoka kwa wanasiasa wengi wao wakiwa wa chama cha Republican alipokuwa akitoa hotuba kwenye kikao cha pamoja cha Congress.
Lakini mgawanyiko wa kisiasa kuhusu vita huko Gaza ulisisitizwa na makumi ya wabunge wa Democratic wa Congress ambao hawakuhudhuria kwa makusudi huku maelfu ya waandamanaji wakiendamana mitaani nje.
Umati wa watu uliokusanyika kwenye jukwaa katika Capitol Hill ulibeba mabango yaliyoandikwa maandishi ya shutuma ikiwa ni pamoja na lile lililomtangaza kiongozi huyo wa Israel kuwa “mhalifu wa kivita anayetafutwa,” likilenga kukumbusha juu ya hati ya kukamatwa iliyotafutwa na mwendesha mashtaka wa Mahakama.
Maelezo ya picha,Maafisa wa polisi wakiwa wamesimama mbele ya Bunge la Congress huku waandamanaji wanaounga mkono Palestina wakipinga hotuba yake.
Kipindi Cha Matumaini..….
Jiandae Kipindi kipya Cha Matumaini katika Idhaa Ya Kiswahili Ya Radio Fortune Africa.

1Samweli 1:20
Ikawa, wakati ulipowadia, Hana akachukua mimba na kuzaa mtoto mwanamume; akamwita jina lake Samweli, akisema, Kwa kuwa nimemwomba kwa BWANA.
Mpendwa kuna ambo Mungu huwa anayafanya sawasawa au kuringana na aina ya majira, usiogope kuna mambo yape muda majira yake yatafika tuu.
Biblia inasema ikawa wakati ulipowadia Hana akachukua mimba na kuzaa mtoto mwanaume. Kwahiyo wakati wa Hana kuzaa ulikuwepo ila ulikuwa haujawadia
Wakati ulipowadia yeye aliyechekwa na Penina, yeye aliyetemewa mate na kusemwa kila aina ya maneno nyakati zilibadirisha kila kitu
Nimetumwa kukwambia maneno haya
Never judge someone based on Season, one season Hana alichekwa kwasababu hakuwa na mtoto, the next season aliheshimika kwasababu ya kuzaa mtoto aliyekuwa bora kuliko mtoto wa Penina
One season David was a Shepherd and the next season he was a king, My dear majira yanabadirika usikubali kamwe mtu akucheke kwasababu leo unachunga kondoo
It is about season’s leo nachunga kondoo but next season nitakuwa mfalme, leo sina mtoto na unanicheka kesho nitamzaa samweli my time is coming
Acha kulia ni kweli leo unachunga kondoo,ni kweli leo unadharauliwa, ni kweli leo unatemewa mate, ni kweli leo unachekwa na kina Penina usilie inuka jipige kifua sema my time is coming
Majira yako yamewadia inuka, usikubali kufia hapo kwasababu tu ya majira unayoyapitia leo nooooo, your season is coming ni swala la muda tu
Chukua dakika chache mchana huu comment “my time is coming”
Kisha watagi marafiki zako wambie “your time is coming” na usiache kushare ujumbe huu na kwa wengine Mungu atakubariki sana sana
Radio Fortune Africa
https://zeno.fm/radio/radio-fortune-africa

Bao La Asubui
Upo uhusiano mkubwa sana baina ya namna unavyofikiri na hali yako ya kimaisha au na jinsi unavyoishi.
Kushindwa kwako, hakutegemeani na nguvu yoyote ulivyonayo isipokuwa ufahamu wako.
Kuanguka kwako hakutegemei maadui wengi ulionao, isipokuwa aina ya mtazamo ulionao.
Kurudi nyuma kwako hakutegemei historia yoyote uliyowahi kuwa nayo, isipokuwa namna unavyoendekeza mawazo yako ya kushindwa.
Naelewa kwamba panahitaji mjadala wa kina kuhusu kipi kinachomtawala mwenzie: mawazo yetu ndiyo yanayotuongoza ama ni sisi ndio tunayaongoza mawazo.
Hapo inapidi tushukie penye uelewa na namna mawazo yetu yanavyojengeka vichwani mwetu.
Kwa haraka haraka, nadhani, twawaza vile tulivyoviingiza ubongoni iwe kwa hiari yetu wenyewe ama pasipo hiari hiyo. Kwa maneno mengine sisi ndio watawala wa mawazo yetu.
Hiyo ni kusema kwamba unavyojiona, ndivyo ulivyo. Ukijidharau, hakuna mtu atakuja kukufanyia kazi ya kukuonyesha thamani uliyonayo.
Ukianza leo kujiona masikini, ni wazi kuwa akili yako itakubaliana nawe na kusema kweli, utakuwa umeukaribisha umasikini wako kwa mikono yako miwili.
Ningependa kukuachia ujumbe huu mchana wa leo;
Katika kila unalojaribu kulifanya, dhania kwamba haiwezekaniki jambo hilo likashindwa kwa namna yoyote.
Kwa sababu, haiwezekani ukashindwa katika jambo lolote, isipokuwa kama utakubali akilini mwako kwamba umeshindwa.
Achana na mawazo ya kushindwa shindwa. Achana na watu ambao hawaishiwi stori za ubaya ubaya. Amua kuyaelekeza mawazo yako kwenye mafanikio.
Kwa sababu mawazo yako ndiyo nguvu yako kuu uliyonayo! Itumie nguvu hiyo!
Jitamkie mchana wa leo kwa imani “Nayaweza mambo yote katika yeye anitiae nguvu”
Watag marafiki zako wambie kwa imani hata kama wamejikatia tamaa wambie ” Unayaweza mambo yote katika yeye akutiae nguvu”
Salamu zangu ziwafikie wenyeji wa Karatu Arusha Nchini Tanzania.
All Rights Reserved © Cantona Group Ltd||2024
Discover more from cantonadigital
Subscribe to get the latest posts sent to your email.