Radio Fortune Africa
https://zeno.fm/radio/radio-fortune-africa
Bao la Asubui Na Cantona Joseph

Kuna wakati Mambo yatatokea na utajikuta umebakia peke yako.
Wakati huu hautawaona kwa karibu wale ambao ulijua utakuwa nao siku zote.
Wakati huu kila maumivu na changamoto unazopitia zitakuwa za kwako mwenyewe.
Hata ukitamani au kutafuta msaada kwa namna gani, hautaupata.
Ukijikuta kwenye hali ujue kuna mambo mawili:
Moja, Mungu anataka kukuonyesha kuwa anaweza kufanya bila wao.
Yaani, hataki mtu yeyote aje baadaye achukue sifa kwa kukusaidia.
Anajiandaa kukusaidia MUNGU mwenyewe.
Usiingie katika kuwalaumu au kunung’unika, uko kwenye mpango mkubwa wa Mungu.
Mbili, huwa anatumia majira hayo kukutenga na wengi…
…ili akuandae kwa ajili ya kesho yako kubwa.
Kuna mahali unaelekea na utakutana na nyakati kama hizi mara nyingi…
…Mungu anaamua kukujengea misuli mapema kwa kukuonyesha kuwa, huwa kuna majira kama haya.
Usipojifunza mapema na kujipa moyo, utaendelea kwenye hiyo hali kwa muda mrefu bila kutoka.
Katika nyakati kama hizi, inua macho na Imani yako kwa Mungu.
Amua kuwa hata kama kila mtu atakuwa mbali nawe, bado hautaacha kumwamini Mungu.
Nakuombea Mungu Akuvushe Salama.
Tafadhali ukimaliza kusoma nisaidie kushare.
Tufwatilie katika ukurasa wetu wa Facebook Page Radio Fortune Africa,like and Follow.
All Rights Reserved © Cantona Group Ltd||2024
Discover more from cantonadigital
Subscribe to get the latest posts sent to your email.