Radio Fortune Africa
https://zeno.fm/radio/radio-fortune-africa
BAO LA ASUBUI – NA CANTONA JOSEPH

UMRI GANI UNAFAA KWA KIJANA KUOA?
Umri mzuri wa kuoa au kuolewa ni pale utakapokuwa umekomaa “matured”.
Katika hili kuna aina 5 za ukomavu
1. Kukomaa kimwili “phyisical maturity”; ndoa inahusisha tendo la ndoa. Muda muafaka wa kuoa au kuolewa ni pale ambapo umekomaa kimwili kumudu tendo la ndoa na pilikapilika nyingine za ndoa. Ndio maana sheria ya ndoa ya mwaka 1976 inasema umri wa kuoa au kuolewa kisheria ni miaka 18 kwenda juu.Na pia ukiwa ndani ya ndoa unaweza ukapata watoto. Kama mwili wako haujakomaa unaweza ukapata matatizo wakati wa kujifungua.
2. Kukomaa kiakili “intellectual maturity”; ndoa inaambatana na majukumu. Ukiwa na majukumu utatakiwa kufanya maamuzi “decisions”. Mfano maamuzi ya namna gani uishi na mwenzako. Namna gani muendeshe familia nk. Sasa kukomaa kiakili hakuna mahusiano na umri. Unaweza ukawa na miaka 40 lakini una akili za kitoto. Kwahiyo kukomaa kiakili ni kigezo kingine kuwa uko tayari kuoa au kuolewa
3. Kukomaa kihisia “emotional maturity”. Mapenzi yanatawaliwa na hisia. Kwahiyo wakati wa “dating” au uchumba hisia ni kali mno na unaweza usione mapungufu ya mwenzako “love is blind”. Mkiingia ndani ya nyumba mkakaa wote usiku na mchana unaanza kuona hili na lile.Inafika kipindi sasa inabidi uamue kupenda sio upende kwa hisia. “You choose to love” even when you don’t fall in love. Hii inahitaji kukomaa kihisia “emotional maturity”.
Friendship > Feelings > Love > Respect
4. Kukomaa Kiimani “spiritual maturity”; Mwanzilishi wa ndoa ni Mungu. Biblia inasema Mungu asipoilinda nyumba yeye ailindaye afanya kazi bure. Pamoja na kukomaa kimwili, kihisia na kiakili bado mlinzi wa ndoa yako ni Mungu. Kumbuka Biblia inasema kwamba mambo ya kiroho yanaenda kiroho. Maana yake ni kwamba usitegemee sana akili zako katika masuala ya ndoa. Lakini Mungu pia amekupa akili. Hivyo tumia akili yako vizuri.
5. Kukomaa kifedha “financial maturity”; kukomaa kifedha haina mahusiano na kuwa na kipato kikubwa au kuwa na kazi au biashara. Isipokuwa akili iliyopevuka kujua kuwa kufanya kazi au kutafuta fedha ni muhimu ukiwa na familia. Unaweza ukawa na fedha nyingi lakini huna “financial maturity” Mfano; Kama fedha yako haisaidii familia yako hauko tayari kwa ajili ya ndoa. Kwahiyo ukiwa na upeo kuwa ndoa inahitaji fedha na uko tayari kupambana kushinda huo mtihani ni wakati muafaka kwako kuoa au kuolewa
Iwapo yote hayo yamekamilika kipimo cha mwisho ni amani ya moyo. Bila amani ya moyo kwa yule unayemuoa au anayekuoa hata kama umekomaa kimwili, kihisia, kiakili, kiimani na kifedha ngoja kwanza. Utaambiwa hapana ukifikisha umri wa miaka 40 lazima uolewe kwa sababu hutoweza kuzaa. Hapana, kuzaa ni baraka za Mungu. Wapo walioolewa na miaka 18 leo wana miaka 60 hawana mtoto. Na wapo walioolewa na miaka 46 na wamezaa. Amani ya moyo ni muhimu sana kwa anayeoa na anayeolewa.
Salamu ziwafikie wakaazi wa Tanga Nchini Tanzania.Hili ndilo bao la asubui.
All Rights Reserved © Cantona Group Ltd||2024
Discover more from cantonadigital
Subscribe to get the latest posts sent to your email.