Radio Fortune Africa -Bao La Asubui
https://zeno.fm/radio/radio-fortune-africa
Na Cantona Joseph
NUSU YA MWAKA ILIYOBAKIA FANYA HAYA
Karibuni tena kwenye life wisdom series. Ni wengi sana tulioanza nao mwaka huu, lakini leo hawapo. Na hili ni jambo kubwa sana la kumshukuru Mungu. Moja ya kitu ambacho huwa kila mwaka kinatokea ni watu wengi sana ambao, huwa hawatimizi malengo yao, na wachache ambao wanatimiza kwa mafanikio makubwa.
Utafiti unaonyesha kama unataka kupata mafanikio kwenye nusu ya pili yam waka, kuna mambo mawili ya kuzingatia.
1. Jitahidi sana kutokuwa na malengo mengi kwa wakati mmoja
Tafiti zinaonyesha mtu anayekuwa na malengo zaidi ya matatu yenye ukubwa unaofanana, mali zake huwa zinatawanyika. Ni vizuri kuangalia ingawa una vitu vingi unataka kufanya, unatakiwa uchuje yale muhimu uende nayo.
Angalia mambo machache yanayoleta matokeo chanya. Ili ufanikiwe ili, ni lazima ugawe maisha yako kwenye mambo muhimu ya msingi. Angalia maeneo ya afya, mahusiano, fedha, kiroho. Ukisoma kitabu cha Timiza Malengo yako, utaona maelezo mazuri kuhusu breakthrough goal. Hili ni lengo mama, ambalo ukiweza kulitimiza, malengo mengine madogo madogo yatakuja.
2. Wengi wanashindwa sababu ya kuwa na malengo ambayo si halisi.
Watu wanakuwa too ambitious. Malengo makubwa ya kifedha, kibiashara, kiafya. Lakini kunakuwa hakuna uhalisia. Mfano mtu anasema kuanzia jan 1 atakimbia km 10 kwa siku. uhalisia unakuwa mgumu, maana huyo mtu ana miaka zaidi ya 10 hajawahi kukimbia hata km 1.
Unapotaka kufanikiwa kwenye maisha yako, epuka kufanya vitu ambavyo hauvipendi. Fanya vitu ambavyo viko ndani ya uwezo wako na unavyovipenda. Vitu vingi ambavyo umekuwa ukivilalamikia, umeacha kuvifanya. Ukitaka kuacha tabia mbaya, tafuta tabia nzuri, uibadilishe na ile tabia mbaya.
All Rights Reserved © Cantona Group Ltd||2024
Discover more from cantonadigital
Subscribe to get the latest posts sent to your email.