Na Cantona Joseph
Wamekufukia Ili Usichipue Tena…
Kuna wakati watu wasiokupenda au maadui zako watafanya jambo la kukumaliza.
Ndio, yaani watakufukia ili Usichipue tena.
Wengine watafanya hivyo kwa KUKUZUSHIA mambo yatakayoharibu SIFA YAKO.
Wengine watafanya FITINA ili upoteze KUKUBALIWA mbele ya MKUU wako.
Wapo ambao hata watatumia MAMLAKA yao kukunyang’anya ULICHONACHO (Nafasi au Fursa fulani).
Nia yao kubwa ni kuhakikisha HAUINUKI TENA.
Usisahau MBEGU huwa pia INAZIKWA ila INACHIPUA.
Ukikutana na hali hii, UNACHOTAKIWA ni kutunza TUMAINI na IMANI YAKO.
UTACHIPUA TENA, walisahau kuwa wewe ni MBEGU.
Endelea Kuamini na Kutumaini, Siku yako ya KUCHIPUA haiko mbali.
Natumai makala hii imekusaidia.
Kama imekusaidia na umeipenda na unataka ujifunze zaidi…
All Rights Reserved © Cantona Group Ltd||2024
Discover more from cantonadigital
Subscribe to get the latest posts sent to your email.