Unashindwa kuongeza MAUZO yako? AINA 10 Za WATEJA Na Jinsi Ya KUWAHUDUMIA…
Leo tunaangalia aina moja wapo kati ya aina 10 za wateja na jinsi ya kuwahudumia.
1. Mteja Mwenye Mashaka (Suspicious Customer)
Mteja wa kundi hili huwa ni mtu wa kuonesha mashaka sana kwenye kila kitu unachomwambia.
Mara nyingi hii hutokea kama pesa aliyonayo ndio hiyo hiyo.
Na akikosea basi itakuwa amekosa kabisa alichokuwa anatarajia.
Ama pengine manunuzi ambayo anataka kuyafanya ni ya kitu cha kudumu…
…na hatakuwa na fursa ya kurekebisha ndani ya muda mfupi.
Kama mashaka yake yanatokana na hofu za namna hii…
…maana yake ni kuwa anakabiliwa na changamoto ya “Complex Buying Behavior”.
Hii hutokea pale ambapo mteja ananunua kitu kwa kutumia pesa nyingi.
Ama kitu ambacho akikosea ni gharama kubwa sana kuja kufanya marekebisho.
Ili kuhakikisha kuwa hafanyi kosa lolote katika manunuzi…
…mteja huyu huwa anajikita katika kuhakikisha anachokifikiria ndivyo kilivyo.
Kwa upande mwingine mashaka yake yanaweza kusababishwa na…
…kitu ambacho alishawahi kukutana nacho huko nyuma.
Inawezekana alishawahi kufanya maamuzi ya kununua kitu fulani…
…na baadaye akajikuta alichotarajia kupata hajaweza kukipata.
Na wakati huo ameshatumia gharama kubwa sana.
Kwa vyovyote vile kazi yako kubwa ya kwanza kwa mteja wa namna hii ni…
…kutafuta MZIZI wa mashaka yake unatokea wapi.
Ukishagundua mzizi wake ni rahisi kuanza kushughulika naye.
Kwa kumwondolea mashaka kuwa tatizo ambalo aliwahi kukutana nalo…
…hataweza kukutana nalo tena.
Natumai makala hii imekusaidia.
Kama imekusaidia na umeipenda na unataka ujifunze zaidi…
All Rights Reserved © Cantona Group Ltd||2024
Discover more from cantonadigital
Subscribe to get the latest posts sent to your email.