WAKIAMBIWA HABARI ZA MUNGU NA NGUVU ZAKE, WATAMKIMBILIA WAPATE KUOKOLEWA
MAANA WALIPO NA WALIVYO, WAMEKANDAMIZWA BARA-BARA NA NGUVU ZA SHETANI
Fikiria watoto wa shule za msingi, sekondari,wanaanguka ghafla siku za kukaribia mtihani au hapa na pale katika majira fulani ya mwaka
Fikiria watoto wadogo shule ya msingi,baadhi wametekwa nyara na waganga, walozi,wachawi konki na konkodi.
Maana walishatolewa kafara kwa mizimu na kufundishwa, shirikishwa, husishwa na uchawi na tubibi twao wakiwa bado chalii kabisa
Fikiria kila ujauzito unatoka na wakizaliwa hawavuki miaka 5 wanakufa
Fikiria ukoo wao wote, wanawake hawaolewagi na ikitokea wameolewa, wanaachika,ndoa hazidumu.
Fikiria ukoo wao,wasichana wanazalishwa wakiwa shuleni, hakuna anayevuka kwenda chuo na chuo kikuu
Fikiria kuanzia babu na bibi ni wavuta bangi, tumbaku na ugolo mpaka baba na mama na watoto kwa kwenda mbele
Fikiria ukoo ambao wao kujiua na kuua ni kitu cha kawaida kama kusukuma bembeya na kubembea
Fikiria wanabeba mimba wakati wa kuzaa wanazaa mifuko ya rambo na kokwa za embe na maparachichi.
Fikiria mtu analewa mpaka kujikojolea, kulala mtaroni au wale wanaotumia madawa ya kulevya na kuanza kubembea njiani
SWALI: Watatokaje kwa hayo madubwasha wanadamu hao?
SWALI: Nani, atawaokoa jibu? ni Serikali, Jamii, mashirika yasiyo ya serikari ?
Imeandikwa:
Wakolosai. 1: 13 Naye alituokoa kutoka ufalme wa nguvu za giza,akatuhamisha na kutuingiza katika Ufalme wa mwana wa pendo lake
Ni Injili pekee-habari za wokovu wa Yesu Kristo ndiyo nguvu ya kuwang’oa kwa hayo
Kila mteule, popote mlipo, hubirini Injili hapana kabisa mchezo, hubiri Injili, na jina la Yesu lisifiwe kote.Simama katika pengo kuiombea jamii iliyotekwa nyara.

FortuneBataka Photography
Ungana nasi kufikisha injili mbali.
Discover more from cantonadigital
Subscribe to get the latest posts sent to your email.