BABA katika Jina la Yesu Kristo wa Nazareth Tunalibariki na kuliinua Jina lako Mungu mwenye nguvu. Ukuu na uweza wote vi mabegani mwako. Pokea sifa Ee Mungu MKUU! Kwanza, twaomba uturehemu Baba. Sisi wanadamu tunatenda dhambi hivyo kupungukiwa na utukufu wako. Baba wa Rehema, tulipokosa popote leo tunaomba msamaha. Tusafi Baba yetu kwa damu ya Yesu Kristo, Bwana wetu. Asante kwa msamaha. Pili, tunakushukuru kwa kuwa nasi wakati wote leo. Umetusaidia Bwana. Tumeuona mkono wako ukishuka toka juu Mbinguni na kutuzingira pande zote. Hilo limetufanya tuwe salama hata sasa. Twashukuru MUNGU. Tatu, Tunaomba ulinzi wako Ee Mungu wa Majeshi. Watoto wako tunaomba tupumzike salama usiku huu. Tuamke asubuhi tukiwa wazima wa afya na wenye furaha pamoja na amani tele. Nne, tuomba Ee Mungu Mwezi huu wa Oktoba watoto wako tuthibitike katika haki. Tukawe mbali na kuonewa. Mapenzi yako tu yakathibitike kwetu. Ratiba zote njema tulizopanga tunapoelekea mwisho wa Mwaka, zikatimie. Roho Mtakatifu, Rafiki na mwombezi unapoingia Patakatifu pa Patakatifu pa Patakatifu kusema na Mungu Baba, ingia na mafaili ya hoja zetu zote zilizojaa mioyoni mwetu. Kila mtu akapokee muujiza kutoka kwa Bwana sawa sawa na uhitaji wake. Kwa Jina la Yesu Kristo Tumeomba na Kushukuru Amen! Usiku mwema Kanisa! Tulindwe na Damu ya Yesu Kristo! Tulale Salama!


Discover more from cantonadigital

Subscribe to get the latest posts sent to your email.

Leave a comment