Afrika Leo Alfajiri -Radio Fortune Africa
Na Cantona Joseph

Kikosi cha kwanza cha polisi wa Kenya kiliwasili katika mji mkuu wa Haiti siku ya Jumanne kuanza misheni iliyokuwa ikisubiriwa kwa muda mrefu ya kulinda amani katika nchi ya Caribbean ambayo imekumbwa na ghasia za magenge, huku kukiwa na shaka kutokana na maandamano waliyoacha nyumbani.
“Hatimaye jeshi la kimataifa liko hapa kusaidia polisi wetu wa kitaifa,” Waziri Mkuu wa Haiti Garry Conille alisema katika mkutano na waandishi wa habari, akisema kazi ya kuchukua tena nchi itaanza “polepole, bila mapigano makubwa isipokuwa lazima.”
“Lakini sitaki mtu yeyote atilie shaka malengo yetu,” alisema. “Jimbo litapata tena mamlaka na kuthibitisha mamlaka yake ili Wahaiti wote waishi kwa amani katika nchi hii.”
Misheni hiyo iliombwa kwa mara ya kwanza na serikali ya awali ya Haiti mwaka wa 2022. Lakini uungwaji mkono ulidorora na mtangulizi wa Conille alilazimika kujiuzulu mapema Machi baada ya kusafiri hadi Nairobi kupata uungwaji mkono wa Kenya huku ghasia zikiongezeka huko Haiti.
Vita vya magenge hivi sasa vimewakosesha makazi zaidi ya watu nusu milioni na karibu milioni tano wanakabiliwa na uhaba mkubwa wa chakula.
Makundi yenye silaha, ambayo sasa yanadhibiti sehemu kubwa ya mji mkuu, yameunda muungano mpana huku yakitekeleza mauaji yaliyoenea, utekaji nyara na unyanyasaji wa kingono.
“Madhumuni ya pekee ya Kenya ni kutumika kama mawakala wa amani,” Waziri wa Mambo ya Nje wa Kenya Monica Juma aliuambia mkutano na waandishi wa habari, akisema polisi watatoa kipaumbele kwa kulinda raia, kufungua njia za usafirishaji wa watu, bidhaa na misaada ya kibinadamu, na kulinda taasisi za serikali.
wingu la shaka
Misheni hii imekumbwa na ati ati tangu mwanzo huku baadhi wakihoji uwezo wa polisi wa Kenya kudhibiti magenge hayo.
Pia kumetokea madai yasiyothibitishwa kuhusu malipo ya polisi hao ambao baadhi wanadaiwa kutopokea pesa kamili walizoahidiwa kabla ya kuanza safari yao.
Lakini hata polisi wa Kenya waliovalia sare waliposhuka kutoka kwa ndege ya shirika la ndege la Kenya Airways wakiwa na silaha mkononi katika mji mkuu wa Haiti Port-au-Prince, wenzao huko Nairobi walikuwa na changamoto kubwa kukabiliana na vijana wa Gen Z waliowashinda nguvu nakupeleka maandamano yao hadi majengo ya bunge.
Polisi hao walishutumiwa pia kutumia nguvu kupita kiasi huku zaidi ya watu watano wakifariki kutokana na majeraha ya risasi, jambo ambalo limeshutumiwa vikali na makundi ya haki za binadamu.

Katika hotuba ya dharura kwa taifa usiku wa Jumanne, Rais William Ruto aliahidi uchunguzi utafanywa juu ya ukiukaji wowote wa haki za waandamanaji huku akisisitiza kuwa, japo kuna uhuru wa kuandamana, polisi pia wana jukumu la kujilinda, na kulinda mali na amani ya wananchi.

Rais mstaafu wa Kenya Uhuru Kenyatta ameelezea kusikitishwa kwake na maafa ambayo yametokea nchini mwake leo wakati waandamanaji walipojitokeza kuupinga muswada wa fedha wa mwaka 2024 ambao ulipitishwa na bunge la taifa.
Kenyatta amesema ni haki ya kila Mkenya kuandamana kwa mujibu wa katiba ya nchi hiyo. Kiongozi huyo wa zamani ameongeza kuwa ni wajibu wa viongozi kusikiliza vilio vya wananchi.
Taarifa ya Kenyatta ameitoa muda mchache tu baada ya Rais William Ruto kulihutubia taifa na kutaja matukio ya leo ya waandamanaji kuwa uhaini.
Waziri mkuu wa zamani Nchini Kenya Raila Odinga.

KINARA wa Azimio la Umoja, Bw Raila Odinga ameelezea kusikitishwa kwake na visa vya mauaji ya vijana yanayotajwa kutekelezwa na maafisa wa polisi wakati wakikabiliana na waandamanaji mnamo Jumanne, Juni 25, 2024.
Maandamano yalishuhudiwa maeneo tofauti nchini kupinga kupitishwa kwa Mswada wa Fedha 2024, na idadi ya watu isiyojulikana wanahofiwa kuuawa kwa kupigwa risasi na polisi.
Baadhi walikumbana na mauti wakati wakijaribu kuingia Bunge la Kitaifa, eneo ambalo Jumanne lilikuwa chini ya ulinzi mkali Mswada tata wa Fedha ukijadiliwa na kufanyiwa marekebisho.
Bw Raila, kupitia taarifa rasmi kwa vyombo vya habari alisema ni jambo la kusikitisha kuona serikali inatumia asasi zake za kiusalama “kuangamiza watoto ambao waliandamana kwa amani kutekeleza haki yao Kikatiba”.
Kulingana na Waziri Mkuu huyo wa zamani ambaye miaka ya awali amekuwa akiongoza nchi kushiriki maandamano kushinikiza serikali kuangazia gharama ya juu ya maisha, Wakenya walitarajia serikali ya Kenya Kwanza ingewapa sikio vijana wanaoandamana.
“Ninasikitishwa na ukatili wa polisi kwa vijana waliokuwa wakiandamana kwa amani na kwa mujibu wa sheria… Ninasikitishwa na mauaji, kutiwa nguvuni, kuzuiliwa na msako unaoendeshwa na polisi kwa wavulana na wasichana wetu ambao tu wanataka kusikizwa kuhusu ushuru dhalimu, unaowanyang’anya maisha yao ya leo na ya siku za usoni,” akasema Bw Raila.
Kiongozi huyo wa chama cha ODM alisema malalamiko ya vijana yangesuluhishwa kwa njia ya amani, ila yaliyoonekana Jumanne hayajawahi kushuhudiwa tangu Kenya ipate uhuru wa kujitawala.
Mashirika ya kutetea haki za kibinadamu, ikiwemo Chama cha Wanasheria Nchini (LSK), yamekashifu vikali jinsi polisi wanakabiliana na waandamanaji.
Mswada wa Fedha 2024 ambao Jumanne mchana ulipitishwa na wabunge, sasa ukisubiri kutiwa saini na Rais Ruto kuwa sheria, unahofiwa huenda ukasababisha maisha kuwa magumu kutokana na ushuru wa ziada (VAT) unaopendekezwa kwa baadhi ya bidhaa na huduma.
Jeshi lamuriwa kuleta utulivu.

Waziri wa Ulinzi wa Kenya Adan Duale ameamuru jeshi la nchi hiyo kupelekwa mitaani na sehemu mbalimbali ya nchi kusaidia polisi kukabili dharura ya kiusalama ambayo imesababishwa na maandamano ya kupinga muswada wa fedha wa mwaka 2024 nchini humo.
Maandamano hayo yamesababisha maafa huku vyombo vya habari nchini humo vikiripoti vifo vya watu 10 na wengine zaidi ya 100 wakijeruhiwa.
Sehemu Bunge la Seneti ikichomwa.


SEHEMU ya Bunge la Seneti imeteketezwa Jumanne, Juni 25, 2024 na kundi la vijana kufuatia maandamano yanayoendelea maeneo tofauti nchini.
Maandamano hayo yanayoongozwa na vijana wa kizazi cha sasa, maarufu kama Gen Z, yameonekana kuchacha Nairobi, Bunge la Seneti la lile la Kitaifa yakivamiwa.
Sehemu ya lile la Seneti imechomwa licha ya maafisa wa polisi kushika doria katika malango yake.
Moshi unaonekana ukifuka, huku makundi ya vijana wenye hasira na ghadhabu wakikimbizana na polisi kujaribu kuingia mabunge hayo mawili.
Duru zinaarifu wabunge wamehepa, kwa minajili ya usalama wao.
Vijana wanaandamana kupinga Mswada wa Fedha 2024, ambao Jumanne mchana ulipitishwa na Bunge la Kitaifa.
Mswada huo, ambao sasa unatarajiwa kutiwa saini na Rais William Ruto kuwa sheria kuiwezesha serikali kukusanya ushuru mpya wa Sh347 bilioni kufadhili bajeti ya mwaka wa 2024/2025, ulipitishwa na wabunge 195 waliopiga kura ya NDIO kuunga mkono marekebisho, huku wabunge 106 wakirusha kura ya LA, kuupinga.
Wengi wa waandamanaji wakiwa Gen Z, wanaukataa kwa msingi kuwa utachangia gharama ya maisha kupanda mara dufu.
Idadi ya watu isiyojulikana wanaripotiwa kuuawa kwa kupigwa risasi na polisi.
Mashirika ya kutetea haki za kibinadamu, ikiwemo Chama cha Mawakili Nchini (LSK), yamekashifu vikali polisi kwa kutumia nguvu kupita kiasi kutuliza waandamanaji.
Jumapili, Juni 23, 2024, Rais Ruto aliahidi kufanya mazungumzo na vijana ili kuangazia malalamishi yao.


MAASKOFU wa Kanisa Katoliki Nchini wamemhimiza Rais William Ruto kutotia saini Mswada wa Fedha wa 2024 ili kutoa nafasi zaidi kwa ushirikishwaji wa maoni na mapendekezo kutoka kwa umma.
Wakiongozwa na mwenyekiti wa Baraza la Maaskofu hao (KCCB), Askofu Mkuu Maurice Muhatia, maaskofu hao Jumanne walisema maandamano ya Wakenya kupinga mswada huo yanaonyesha kuwa hawakubaliani na mapendekezo yake.
“Kufuatia fujo zilizoshuhudiwa jijini Nairobi na maeneo mengine nchini, Rais William Ruto hafai kutia saini mswada huu tata wa Fedha kuwa sheria. Serikali itoe muda zaidi kwa Wakenya kutoa maoni yao kwa mswada huo kwa lengo la kurejesha utulivu nchini,” akasema kwenye kikao na wanahabari katika afisi za KCCB mtaani Karen, Nairobi.
Askofu Muhatia alikashifu maafisa wa polisi na baadhi ya waandamanaji waliosababisha fujo zilizochangia maafa, majeruhi na uharibifu wa mali wakati wa maandamano hayo yaliyoshuhudiwa katika kaunti 27 nchini.
“Kwa mara nyingine tunaomba maafisa wa polisi kukoma kutumia nguvu kupita kiasi na hata kupiga risasi waandamanaji. Nao waandamanaji, wadumishe amani wanapotekeleza haki yao Kikatiba,” akaeleza.
Maaskofu hao pia waliwataka waumini wa Kanisa Katoliki kote nchini kuombea taifa la Kenya wakati wa kipindi cha siku tisa (90) cha Maombi ya Novena of the Sacret Heart of Jesus.
Awali, maandamano yalishamiri jijini katika barabara kadha za Nairobi wakati ambapo wabunge walikuwa wakishughulikia mswada huo kwa awamu ya tatu.
Hatimaye katika kura iliyopigwa wabunge 195 walifaulishw kupitishwa kwa Mswada huo huku wenzao 106 wakipinga.
Hatua hiyo ilikasirisha zaidi waandamanaji, wengi wao wakiwa vijana barobaro maarufu kama Gen-Z, kiasi cha kuvamia majengo ya bunge na kuharibu mali.
Polisi walijibu kwa kutumia risasi dhidi ya waandamanaji hao na kuua idadi ya watu isiyojulikana.
MaandamanoYaGenZ
TheHeartBeatofAfrica
bunge
Kenya Kwanza
Mswada wa Fedha 2024
Rais William Ruto.
All Rights Reserved © Cantona Group Ltd||2024
Discover more from cantonadigital
Subscribe to get the latest posts sent to your email.