Unapohisi imekwisha.

“Hakuna ninachoweza Kufanya”

Kuna wakati utafika kwenye maisha yako, kila dalili inayokuzunguka itakuonesha kuwa HAKUNA UNACHOWEZA KUFANYA ili kubadilisha hali yako.

Watu wengi wakifika katika hali hii, huwa inakuwa chanzo cha KUKATA TAMAA na KUISHIA NJIANI.

Mwingine kwa sababu ya KUPOTEZA PESA kwa kupata HASARA au KUTAPELIWA, kwa sasa ameandamwa na madeni na hajui ATATOKAJE.

Kuna mwingine ambaye amepitia changamoto kwenye MAHUSIANO yake na HAONI kama ATAPATA FURAHA TENA. Kuna ile hali mtu amewekeza kwenye mahusiano na mtu kisha anakuja kufanyiwa “tukio” ambalo LINAMVURUGA na KUMPOTEZEA mwelekeo.

Wengi wakifika hatua hii wanasema “Hakuna ninachoweza Kufanya”. Kiuhalisia inaonekana hivyo, ila UKWELI ni kuwa UNACHO CHA KUFANYA.

Usihangaike na kile KILICHO NJE YA UWEZO WAKO. Pambana na kile kilicho NDANI YA UWEZO WAKO. Tafuta kitu kimoja unachoweza kufanya ili USIENDELEE kuwa CHINI.

Inawezekana ni MAAMUZI TU ya kuanza UPYA au KUSAMEHE, yakabadilisha kabisa HALI YAKO YAKO.

Kipo UNACHOWEZA KUFANYA

All Rights Reserved © Cantona Group Ltd||2024


Discover more from cantonadigital

Subscribe to get the latest posts sent to your email.

Leave a comment