Walio katika mahusiano ya karibu wanajijengea hisia na nguvu fulani.

Walio katika mahusiano ya karibu wanajijengea hisia na nguvu fulani.
kwa sababu ya ukweli kwamba watu wanaokuwa katika mahusiano ya karibu wanajijengea hisia na nguvu fulani ambayo huwasaidia kusaidiana na kujaliana wakati wa shida.

Siyo tu kwamba watu walioko katika mahusiano ya aina hii wanaishi muda mrefu lakini pia ni kweli kwamba wanakuwa na furaha na wanaridhika na maisha kuliko wale wanaoshindwa kukaa katika mahusiano.

Suala la uaminifu katika mapenzi kwa karne hii limekuwa kikwazo kikubwa kwa watu wengi sana, wengi wemekuwa si waaminifu wakati mwingine kupelekea mahusiano hayo kufa.

Hivyo uaminifu ni muhimu sana katika mapenzi kwa kuwa katika mahusiano ya kimapenzi kuna faida nyingi kwa mwili na akili. Watu walio katika mahusiano bora ya mapenzi huishi maisha marefu na kufurahia afya njema kuliko wale wasiokuwa katika mahusiano ya aina hiyo.

UHUSIANO wa kimapenzi ni jambo gumu sana. Ugumu wake unatokana na ukweli kwamba, mwanaume aliyezaliwa na kulelewa katika mazingira tofauti, anakutana na mwanamke ambaye naye amezaliwa na kukulia katika mazingira mengine.

Wawili hawa wanaanza ukurasa mpya wa maisha, kila mmoja akiwa na historia tofauti kabisa ya huko alikotoka, unategemea itakuwa rahisi kwa wawili hawa kuishi bila misuguano?
Jibu ni HAPANA. Kwa lugha nyepesi, hakuna uhusiano wa kimapenzi ambao hauna changamoto na changamoto kubwa zaidi katika mapenzi ni usaliti.

Nimeshawahi kueleza huko nyuma na naendelea kueleza kwamba hakuna kitu kinachoumiza katika uhusiano wa kimapenzi, kama usaliti.
Ni ukweli kwamba licha ya usaliti kuwa jambo baya katika uhusiano, bado watu wanasalitiana kila kukicha.

Wanandoa wanasalitiana, wachumba wanasalitiana na hata wale ambao wapo kwenye hatua za awali kabisa kuelekea kwenye uchumba, nao wanasalitiana. Si ajabu hata wewe msomaji wangu, siku chache zilizopita umesaliti au umesalitiwa! Ni ukweli mchungu ambao ni lazima tujadiliane kuhusu namna ya kuukomesha.,.

Kama kuna kiumbe kinaishi kwa presha na msongo kwenye dunia ya leo basi ni hiki kiumbe kinaitwa MWANAUME!

Presha yenyewe inasababishwa na kujikaza bila kukubali kuwa kinahitaji msaada wa kiroho zaidi kuliko ushindi wa mwili. Kujikaza kwake kunakifanya kisiwe na mahali pa kusemea matatizo yake, kitafute mahali pa kulia pa siri ili kisionekane kinyonge, kinajihangaisha kudhibitisha kuwa mwanaume, kina nguvu mwisho kinajikuta hakina nguvu basi kinazidi kujipa presha, kinawaza sana namna gani kiwe na misuli ya mwili (sixpack) wakati rohoni kimekondeana sana, kinaogopa sana kuonekana dhaifu lakini hakiyaishi maisha ya kuwa na nguvu, NANI ATAKIOKOA KAMA SI MUNGU?Wanawake wanajieleza wakati wanapitia changamoto maishani,hata unapata analia,lakini wanaume hawajielezi hata kidogo.

Kizazi cha wanaume ili kipone kuna maeneo lazima kianze kupatikana kwa wingi, sehemu za ibada, sehemu za kazi, sehemu za semina, sehemu za maombi, na pia kipatikane nyumbani, ili kiweze kuwa na muda na Mungu, ndoa, familia, uchumi na heshima maana huko ndiko hivi vitu kinavyovitafuta sana vinapatikana.

Ila kikiendelea kupatikana bar, mpirani, hotelini, na vijiweni BASI BAADA YA MIAKA MICHACHE TUTEGEMEE MIAKA YAKE YA KUISHI KUZIDI KUPUNGUA KULIKO SASA.
HII NI NDOTO YA LEO NAAMINI WANAUME WENGI TUTAITAFAKARI.

Pokea mengi kutoka kwenye website yangu  hii link http://CantonaJoseph.wordpress.com
#CantonaJosephMotivates. #Iposiku #Getlnspired #Itissettled


Discover more from cantonadigital

Subscribe to get the latest posts sent to your email.

Leave a comment