Aina ya akina mama.

Watu ambao walikosa sana au walinyimwa kabisa mapenzi wakiwa watoto au ktk sehemu fulani kwenye makuzi yao wanaweza kuonyesha tabia zifuatazo wanapokuwa watu wazima.

1.MAMA ANAYE PENDA UMBEA.

Huyu ni mama ambaye anapenda udaku wa kila,wakati wote atajihusisha na mambo ya watu wengine ana hata utapata atapagawa na umbea wake na mwisho kuwasengenya hata watoto wake. Mama waina hii anawakera watoto ake sana,wanajiuliza atawacha tabia hii lini?

2. MAMA ALIYE NA MACHUNGU.

Mama wa aina huyu ana machungu,ana hasira sana.
Anaweza hafurahi alipo maishani,labda andiye mlezi wa pekee wa wanawe.
Na wanawe wanapotaka kujua aliko baba yao,kutaja tuu linamkera sana, uhusiano wake na baba watoto ni mbaya sana.
Labda alipitia machungu na mwanaume wake baba watoto wake
Pasipo kufahamu machungu hayo yana athiri sana mtoto wake anapokua..

3.MAMA ASIYEKUBALI MAJUKUMU YAKE.

Huyu ni ama ambaye hajajikubali kwamba ni mama wa mwana au wana,ayupo tayari kabisa kuwa mama.
Anachofurahia ni kuendeleza taaluma yake.
Ametekeleza mwana kwa wazazi wake vijijini.Anafurahi amaisha ya kuishi pasipo uwepo wa watoto wake.
Anapokumbushwa majukumu ya mama anakwazika sana.Mwana anapokua hamtambui kama mama yake.

4. MAMA MWANA.

Huyu ni mama ambaye angali ana tabia ya usichana,anajiona angali barubaru.
Anapenda kuparty,kunywa  sana vilabuni,anapenda kuchepuka.Anatoka na wanaume tofauti tofauti.
Ametelekeza mtoto,anaweza akaficha yupo na mtoto,maana marafiki watamkumbusha kuwa ana majukumu.

Mtoto anayepata makuzi haya ya mama  ni mwenye kuonyesha kiu kubwa sana ya kupendwa hata kwenye vitu vidogo ambavyo utadhani havihitaji yeye kutaka aonyeshwe mapenzi. Sababu hii huwafanya wapenzi wao (wasiojua background zao) kuwaona ni wadekaji sana au wako demanding sana. Hii inaweza kusumbua sana mahusiano yao mara kwa mara unless ampate mtu mwelewa anayeielewa background yake.

5. MAMA AMBAYE ANA MAKOVU.



Huyu ni mama asiye na furaha ana huzuni na anapowalea watoto wake,watoto wana litambu hilo machoni amejaa machozi.
Hayuko sawa,hili swala lina athiri ukuaji wa mtoto,fahamu katika ukuaji wa mtoto anahitaji mazingira salama yenye ucheshi na furaha ni majonzi.

6 MAMA AMBAYE HISIA ZIMEKUFA.

Huyu ni mama ambaye anajukumika kuwalea watoto wake,anawandalia chochote wanachohitaji.
Anafurahia kuwalea lakini ule ukaribu na wanawe haupo maana hana mvuto nao,Uhusiano wa mwana na mama haupo.
Watoto wake wanatamani mama wa marafiki wao na yeye yupo.

7. MAMA MSHERATI/MZINI.

Huyu ni mama ambaye anawabadilisha wanaume,anaingia katika mahusiano na kuyavunja,ana megana na wanaume tofauti,ni mjeuri sana na anatumia kuchipuka kutimiza malengo yake.Anaweza athiri mtoto kupenda tabia ya kuchepuka au mtoto kudharau mama yake kutokana na tabia hiyo.

8. MAMA ASIYE NA MAONO.

Huyu ni mama asiye na maono kwa wanawe,lake ni kuona maisha yanasonga tuu,pasipo  na maono kwa wanawe.Hatoi mwelekeo wa malengo makubwa kwa wanawe,mtoto anakua pasipo kufundishwa maamuzi makubwa anayotarajiwa kuyafanya na malengo maishani.
Mama huyu hawezi kuwatia moyo watoto wake.

9.MAMA ANAYEPENDA KUNG’ARA

Huyu ni mama mawazo yake yote yapo kwenye ulimwende wake kung’ara tuu makucha yake,kujirembesha,muonekano wake.Hana hata mda kuwaogesha wanawe,hana mda na watoto wake.

10. MAMA ANAYEYAUA MAONO.

Wapo mama wanaoyaua malengo ya watoto wao,badala ya kuyakuza maono hayo  wanayamaliza kabisa.Hawapendi kuona watoto wakiwa na malengo makubwa.Utashangaa anasifia watoto wa wengine,anaenda katika party ya mafanikio ya watoto wa marafiki wake huku anashindwa kulea maono ya watoto wake.

11. MAMA ASIYEJIPENDA.

Huyu ni mama ambaye ajiamini mwenyewe,hili litachangia sana ukuaji wa mtoto na hatimaye,mtoto atakosa kujiamini.Mtoto asipojifunza kujipenda atakua ni mtu ambaye hata katika kufanya maamuzi atakuta anasitasita kutokana na tatizo hili la makuzi.
Mtoto anakuwa mwoga sana wa kupendwa “repulsive”, anahofia na kuogopa anapoonyeshwa mapenzi, anajiona kama hastahili. Unaweza kumpa zawadi kubwa sababu ya upendo tu akaikataa kabisa, au ukianza kumwonyesha mahaba anakukimbia au kukukwepa. Wana very low self esteem maana hawaamini kama wao wanastahili kupendwa na yeyote.

12. MAMA ANAYEAMUA KILA JAMBO.MAMA DIKTETA

Huyu ni mama anayeamua jambo pasipo kushirikisha watoto kuona maoni yao.
Atamua watoto wataoa nani,wataolewa na nani.Mtoto anakua na matatizo ya mahusiano na kukosa mwelekeo wa kujisimamia.Mtoto hawezi kuamua jambo na likawa,lazima aegeme mama.

13. MAMA ANAYEKUZA VYEMA.

Huyu ni mama ambaye anastahili kulea watoto,ana bidii,ana malengo ana uhusiano na watoto wake.
Yupo karibu na watoto wanapomwitaji,anawapenda,ni msikivu na anawadhibu watoto kwa upendo.
Amewekeza kwa watoto wake anapowatia moyo kufikia malengo makubwa maishani.
Anamsifia mtoto wake kuongeza jitihada maishani.Anasimama na mtoto kutambua fursa na kuekeza.

Mtoto anakua maishani akifaulu kwamba ana muhimili mkuu ambaye ni mama.Huyu ni super mother.

Ndio maana huwa nina sisitiza sana, kwenye mahusiano tamani sana kuifahamu background ya mpenzi wako. Inamchango mkubwa sana kwenye tabia zake za kila siku

Cantona School of Thoughts
Tembea Youtube Subscribe Youtube channel yangu
CantonaCast Television
https://youtu.be/l-hQx4EfR_Y
Website: cantonadigital.wordpress.com
Email:cantona.online254@gmail.com
#MahusianoNaNdoa
#IpoSiku
#CantonaJoseph

All Rights Reserved © Cantona Group Ltd|2024


Discover more from cantonadigital

Subscribe to get the latest posts sent to your email.

Leave a comment