Mswada Nchini Kenya waleta kimbiakimbia miji tofauti.

Na Cantona Joseph:Juni 20,2024

  • Afrika Leo Jioni
Kenya: Maandamano dhidi ya muswada tata wa fedha yaendelea

Kenya: Maandamano dhidi ya muswada tata wa fedha yaendelea

Waandamanaji mjini Nairobi wamesema wataelekea kwenye ukumbi wa Bunge la Taifa huku kukiwa na ulinzi mkali wa polisi.Maandamano hayo yalihamasishwa kupitia mitandao ya kijamii./Picha: AA

Waandamanaji nchini Kenya wameendeleza maandamano mengine siku ya Alhamisi kama ishara ya kupinga muswada wa fedha na ongezeko la kodi linalotishia kupanda kwa gharama za maisha nchini humo.

Serikali ya William Ruto ilikubali kufanya mabadiliko kwenye muswada huo siku ya Jumanne baada ya waandamanaji, wengi wakiwa ni vijana kukabiliana na polisi katika mji mkuu wa Nairobi.

Hata hivyo, serikali ya nchi hiyo bado itaendelea kutekeleza ongezeko la kodi ikisema hatua hiyo inalenga kutunisha hazina yake na kupunguza utegemezi wa ukopaji kutoka nje.

Waandamanaji hao wamenuia kuendelea na maandamano hayo nchi nzima, pamoja na maeneo ya Mombasa na Kisumu ambayo ni himaya za upinzani.

Barabara zafungwa

“Wanapaswa kukataa muswada ule sio kuuhariri,” Sarah Njoroge aliiambia AFP. “Wanadhani kuwa tutapaza sauti zetu kwenye mitandao ya kijamii tu na kuwa tutachoka.”

Mamlaka zilifunga barabara karibu na jengo la bunge mjini Nairobi, huku kukiwa na idadi kubwa ya walinda usalama, ambapo wabunge wanatarajiwa kuanza kujadili muswada huo siku ya Jumatano.

Waandamanaji mjini Nairobi wamesisitiza kuwa watatembea kuelekea kwenye eneo la bunge, ambalo ni lazima lipitishe toleo la mwisho la muswada huo kabla ya Juni 30.

Chanzo za bunge kiliiambia AFP kuwa kura kwa mapendekezo ya muswada huo inatarajiwa kupigwa Juni 27.

Upungufu

Kodi hizo zilitarajiwa kuongeza dola bilioni 2.7 ambayo ni sawa ya asilimia 1.9 ya pato la taifa, na kupunguza upungufu wa bajeti kutoka asilimia 5.7 mpaka 3.3 ya pato la taifa.

Siku ya Jumanne, ofisi ya Rais ilitangaza kuondoa baadhi ya kodi zilizopendekezwa kwenye manunuzi ya mikate, umiliki wa magari pamoja na huduma za miamala ya kifedha, jambo lililoibua onyo kutoka hazina kuhusu upungufu wa bilioni 200 kutokana na maamuzi hayo.

Kwa sasa, serikali ya Kenya imelenga ongezeko kwenye bei ya mafuta na kodi za mauzo ya nje kuziba ombwe linalotokana na mabadiliko, hatua ambayo wakosoaji wanasema itasababisha ugumu wa maisha zaidi huku nchi hiyo ikikumbana na viwango vikubwa vya mfumuko wa bei.

Dharau

Takribani watu 335 walikamatwa wakati wa maandamano hayo, kulingana na taasisi za haki za binadamu ikiwemo Tume ya Haki za Binadamu ya Kenya (KNCHR) na Amnesty Kenya.

“Tumebadili mbinu. Leo tutavaa mavazi tufauti ili kuepusha watu kukamatwa,” alisema mmoja wa waandamanaji.

Kenya ni mojawapo ya nchi zenye uchumi unaoendelea katika ukanda wa Afrika Mashariki. Hata hivyo, theluthi moja ya watu wake milioni 51.5 wanaishi katika umaskini.

Pata habari zaidi kupitia whatsapp channels

Radio Fortune Afrika

Habari zinazohusiana

Katika Picha: Vijana waliochoshwa na vita DRC wapata faraja mchezo wa kuteleza

Katika Picha: Vijana waliochoshwa na vita DRC wapata faraja mchezo wa kuteleza

Huku kukiwa na operesheni za kijeshi zinazoendelea nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo za kung’oa makundi ya waasi, kijana mmoja anatoa suluhu la kipekee ili kupunguza msongo wa mawazo na kukabiliana na uhalifu mijini

Kenya yatangaza ubinafsishaji wa makampuni yake ya serikali

Kenya yatangaza ubinafsishaji wa makampuni yake ya serikali

Baraza la mawaziri la Kenya limeidhinisha mswada mpya wa Ubinafsishaji ambao utawezesha nchi kubinafsisha baadhi ya mashirika ya serikali.

Mke wa Rais wa Kenya kupanda miti milioni 500 Ndani ya miaka tisa.

Mke wa Rais wa Kenya kupanda miti milioni 500 Ndani ya miaka tisa.

Serikali ya Kenya kupitia mke wa Rais yajidhatiti kukabiliana na mabadiliko ya Tabia ya nchi kwa kupanda miti zaidi ya bilioni 15 kufikia mwaka 2032

Serikali za Kenya na Uganda zatangaza tahadhari katika mipaka yao.

Serikali za Kenya na Uganda zatangaza tahadhari katika mipaka yao.

Tahadhari na vizuizi vya wekwa katika mipaka ya kenya na Uganda siku chache tangu Tanzania ithibitishe kuwa na watu waliopata maambukizi ya virusi vya Marburg.

Makala yanayovuma katika kategoria hii

Somalia iko tayari kudumisha mtangamano wa Afrika Mashariki

Somalia iko tayari kudumisha mtangamano wa Afrika Mashariki

Kulingana na Katibu Mkuu wa Afrika Mashariki, Somalia imeonesha nia thabiti ya kudumisha mtangamano huo.

Nigeria: Mamilioni ya wasichana wapata chanjo dhidi ya saratani ya shingo ya kizazi

Nigeria: Mamilioni ya wasichana wapata chanjo dhidi ya saratani ya shingo ya kizazi

Maofisa wa nchi hiyo wamepongeza hatua dhidi ya virusi vinavyosababisha magonjwa ya zinaa (HPV).

Houthi: Tulitumia 'silaha mpya' kuzamisha meli ndani ya Bahari Nyekundu

Houthi: Tulitumia ‘silaha mpya’ kuzamisha meli ndani ya Bahari Nyekundu

Mashambulizi ya Israeli katika eneo la Gaza yameingia siku ya 258 yakiwa yameua Wapalestina 37, 396, wengi wakiwa ni akina mama na watoto wadogo, na kujeruhi 85,523, huku zaidi ya watu 10,000 wakihofiwa kufukiwa na vifusi.

'Enzi mpya': Ramaphosa wa Afrika Kusini aapishwa kwa muhula wa pili

‘Enzi mpya’: Ramaphosa wa Afrika Kusini aapishwa kwa muhula wa pili

Cyril Ramaphosa anasema muhula wake mpya kama mwanzo wa enzi mpya.

Nini kingine ungependa kujua?

Vile vile

Katika Picha: Vijana waliochoshwa na vita DRC wapata faraja mchezo wa kuteleza

Katika Picha: Vijana waliochoshwa na vita DRC wapata faraja mchezo wa kuteleza

Kenya yatangaza ubinafsishaji wa makampuni yake ya serikali

Kenya yatangaza ubinafsishaji wa makampuni yake ya serikali

Mke wa Rais wa Kenya kupanda miti milioni 500 Ndani ya miaka tisa.

Mke wa Rais wa Kenya kupanda miti milioni 500 Ndani ya miaka tisa.

Serikali za Kenya na Uganda zatangaza tahadhari katika mipaka yao.

Serikali za Kenya na Uganda zatangaza tahadhari katika mipaka yao.

Kenya yatajwa kuwa nchi bora zaidi barani Afrika kwa watu kutoka nje kuishi

Kenya yatajwa kuwa nchi bora zaidi barani Afrika kwa watu kutoka nje kuishi

Maarufu

Katika Picha: Vijana waliochoshwa na vita DRC wapata faraja mchezo wa kuteleza

DRC: Jeshi la Kongo lataka ushirikiano wa raia ili kuwadhibiti wanamgambo

Ukame wapelekea changamoto ya kiafya nchini Somalia

Kenya yatangaza ubinafsishaji wa makampuni yake ya serikali

Raia wa Nigeria waanza mfungo wa Ramadhani huku kukiwa na uhaba wa

Shirika

Majukumu ya Kisheria

  • Pichani:Rais William Ruto wa Kenya

Tovuti hii hutumia vidakuzi. Kwa kuendelea kuangalia tovuti hii, unakubaliana na vidukizi

All Rights Reserved © Cantona Group Ltd|2024

Discover more from cantonadigital

Subscribe to get the latest posts sent to your email.

Leave a comment