
Rais wa Somalia Hassan Sheikh Mohamud (kushoto) akipongezwa na Rais Salva Kiir Mayardit wa Sudan ya Kusini mara baada ya Somalia kuidhinishwa kujiunga na Jumuiya ya Afrika Mashariki./Picha: Wengine
Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) Veronica Mueni Nduva amesisitiza nia ya Jamhuri ya Shirikisho la Somalia katika kudumisha mtangamano wa jumuiya hiyo.
Akizungumza katika kikao cha wiki moja kinachoangazia mtangano wa EAC mjini Nairobi nchini Kenya, Nduva aliweka msisitizo kwenye muktadha wa kihistoria wa nchi ya Somalia unaliweka taifa hilo kwenye safari ya kuelekea na kufikia mtangamano wa Jumuiya hiyo yenye nchi wanachama nane.
“Jamhuri ya Shirikisho la Somalia ilipata kuwa mwanachama kamili wa EAC Machi 2024, baada ya kuwasilisha rasmi hati yake ya kuridhia Mkataba wa Kujiunga na Jumuiya hii, mkutano wa leo unaashiria hatua muhimu katika safari hii, kuoanisha michakato ya kitaifa ya Somalia na mifumo ya kikanda ili kuhakikisha ushirikiano wa kina,” alisema.
Kulingana na Nduva, mchakato huo utahusisha shughuli zinazopaswa kufanywa kwa pamoja kati ya Somalia na Mashirika na taasisi za EAC.

“Mchakato huu unaelezea shughuli muhimu zilizoainishwa katika mipango ya kitaifa na yenye mwelekeo wa jamii. Hizi ni pamoja na kuoanisha mfumo wa kisheria wa Somalia na viwango vilivyowekwa vya kikanda na kuhakikisha ushiriki thabiti katika programu na shughuli za EAC,” aliongeza.
Kulingana na Nduva, hadi kukamilika kwake, mchakato huo utatumika kama nyenzo ya kimkakati ya kusawazisha programu na kukusanya rasilimali kwa ufanisi katika Jumuiya nzima.
Radio Fortune Africa
Habari zinazohusiana

Ukame wapelekea changamoto ya kiafya nchini Somalia

Hussein Mwinyi: Chakula kipo cha kutosha

Serikali za Kenya na Uganda zatangaza tahadhari katika mipaka yao.

Bandari kavu ya Tanzania kuanza kutoa huduma hivi karibuni
Makala yanayovuma katika kategoria hii

Kenya: Maandamano dhidi ya muswada tata wa fedha yaendelea

Nigeria: Mamilioni ya wasichana wapata chanjo dhidi ya saratani ya shingo ya kizazi
Maofisa wa nchi hiyo wamepongeza hatua dhidi ya virusi vinavyosababisha magonjwa ya zinaa (HPV).

Houthi: Tulitumia ‘silaha mpya’ kuzamisha meli ndani ya Bahari Nyekundu

‘Enzi mpya’: Ramaphosa wa Afrika Kusini aapishwa kwa muhula wa pili
Cyril Ramaphosa anasema muhula wake mpya kama mwanzo wa enzi mpya.
Nini kingine ungependa kujua?
Vile vile

Ukame wapelekea changamoto ya kiafya nchini Somalia

Hussein Mwinyi: Chakula kipo cha kutosha

Serikali za Kenya na Uganda zatangaza tahadhari katika mipaka yao.

Bandari kavu ya Tanzania kuanza kutoa huduma hivi karibuni

“Uturuki ni rafiki iwe mvua au Jua” ubalozi wa Tanzania, Uturuki
Maarufu
Katika Picha: Vijana waliochoshwa na vita DRC wapata faraja mchezo wa kuteleza
DRC: Jeshi la Kongo lataka ushirikiano wa raia ili kuwadhibiti wanamgambo
Ukame wapelekea changamoto ya kiafya nchini Somalia
Kenya yatangaza ubinafsishaji wa makampuni yake ya serikali
Raia wa Nigeria waanza mfungo wa Ramadhani huku kukiwa na uhaba wa noti za benki
Shirika
- Kuhusu Radio Fortune Africa
- Wasiliana Nasi
Majukumu ya Kisheria





Tovuti hii hutumia vidakuzi. Kwa kuendelea kuangalia tovuti hii, unakubaliana na utumizi wa vidakuzi.
All Rights Reserved © Cantona Group Ltd|2024
Discover more from cantonadigital
Subscribe to get the latest posts sent to your email.