Kwa Nini Nchini Kenya, Tanzania na Uganda zasomba bajeti kwa wakati mmoja.

Habari

Biashara

Michezo

Maoni

Maisha

Video

Uchambuzi

Kwa nini nchi za Afrika Mashariki zinasoma Bajeti Kuu siku moja?

Kwa nini nchi za Afrika Mashariki zinasoma Bajeti Kuu siku moja?

Mwaka huu ni nchi kadhaa za Afrika Mashariki ikiwemo Tanzania, Kenya, Uganda na Sudan Kusini zitasoma bajeti kuu ya serikali zao kwa wakati mmoja.

Mwezi wa Juni kila mwaka unashuhudia kusomwa kwa bajeti za nchi kadhaa za Jumuiya ya Afrika Mashariki

Mwezi Juni kila mwaka unashuhudia kusomwa kwa bajeti kuu za nchi kadhaa za Jumuiya ya Afrika Mashariki yaani EAC kwa ajili ya mwaka mpya wa fedha.

Lakini utamaduni huu wa nchi kusoma bajeti kwa wakati mmoja ulianzia wapi na kwa nini?

Rwanda, Uganda, Kenya, na Tanzania zimekuwa zikifanya hivi kulingana na maelekezo ya mwaka 2010 ya Baraza la Mawaziri la EAC.

Wanafanya hivyo ili kuoainisha sera zao za kifedha ili kuendana na matakwa ya Umoja wa Forodha, Soko la Pamoja na hatimaye Sarafu moja.

Sababu nyengine ni kuepusha uwezekano wa nchi moja kujinufaisha kwa kushusha au kupandisha kodi kwa faida yake dhidi ya nchi nyingine.

Kwa mfano, Kenya ingesoma bajeti yake na kupanga bei ya mkate kuwa shilingi 60, Tanzania ingefuata mfano huo wiki au miezi kadhaa baadaye na kuweka bei yake kuwa shilingi 50 na wiki chache baadaye Rwanda pengine ingefuata mkondo huo na kupanga bei ya mkate huo huo kuwa shillingi 45 halafu Uganda nayo ikaweka shillingi 40.

Hii itakua na athari katika soko la kanda la Afrika mashariki.

Mwaka huu ni Tanzania, Kenya, Uganda na Sudan Kusini zitakazosoma bajeti zao kwa wakati mmoja.

Hii ni kutokana na kwamba, Rwanda imeshasoma bajeti yake mwezi wa 5 mwaka huu kwa sababu inaelekea kufanya mchaguzi mkuu mwezi Julai, 2024.

Kwa upande mwengine, Somalia na DRC hazitosoma bajeti zao siku hiyo hiyo, kwani bado hazijaainisha sera zao za kifedha na jumuiya ya EAC. Hata hivyo, bajeti za mwaka huu wa fedha kutoka nchi za Afrika Mashariki, zimejikita katika vipao mbele kadhaa, ikiwemo miradi ya kimkakati pamoja na uwekezaji katika miundombinu muhimu.

Wakati huo huo, wananchi wanategea macho kuona ni kwa kiasi gani bajeti ya mwaka huu itaathiri maisha yao ya kila siku, hasa ikizingatiwa kwamba, kumekuwa na mapendekezo ya kuongeza kodi katika bidhaa muhimu kama vile mafuta ya kupikia.

Bajeti Afrika Mashariki
Uchumi Afrika Mashariki
kenya
Uganda
Tanzania
Rwanda
Habari zinazohusiana

Vijana waliochoshwa na vita DRC wapata faraja mchezo wa kuteleza
Katika Picha: Vijana waliochoshwa na vita DRC wapata faraja mchezo wa kuteleza
Huku kukiwa na operesheni za kijeshi zinazoendelea nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo za kung’oa makundi ya waasi, kijana mmoja anatoa suluhu la kipekee ili kupunguza msongo wa mawazo na kukabiliana na uhalifu mijini
Kenya yatangaza ubinafsishaji wa makampuni yake ya serikali
Kenya yatangaza ubinafsishaji wa makampuni yake ya serikali
Baraza la mawaziri la Kenya limeidhinisha mswada mpya wa Ubinafsishaji ambao utawezesha nchi kubinafsisha baadhi ya mashirika ya serikali.
Mke wa Rais wa Kenya kupanda miti milioni 500 Ndani ya miaka tisa.
Mke wa Rais wa Kenya kupanda miti milioni 500 Ndani ya miaka tisa.
Serikali ya Kenya kupitia mke wa Rais yajidhatiti kukabiliana na mabadiliko ya Tabia ya nchi kwa kupanda miti zaidi ya bilioni 15 kufikia mwaka 2032
Hussein Mwinyi: Chakula kipo cha kutosha
Hussein Mwinyi: Chakula kipo cha kutosha
Wasiwasi juu ya gharama na upatikanaji wa chakula visiwani Zanzibar hasa katika msimu huu wa Ramadhani wazua hofu kwa raia.
Makala yanayovuma katika kategoria hii
Bajeti ya Uganda yalenga kuinua maisha ya mwananchi
Bajeti ya Uganda yalenga kuinua maisha ya mwananchi
Waziri wa Fedha wa Uganda alisema bajeti aliyosoma kwa kiasi kikubwa ni ya wananchi ambao bado wamekwama katika uchumi wa kujikimu.
Bajeti ya Tanzania yaangazia zaidi uzalishaji wa ndani
Bajeti ya Tanzania yaangazia zaidi uzalishaji wa ndani
Sekta zilizonufaika kwa bajeti ni pamoja na viwanda vya maji, kilimo, madini na michezo hasa soka.
Bajeti ya Kenya iliangazia nini?
Bajeti ya Kenya iliangazia nini?
Kenya ilisoma bajeti yake ya mwaka 2024/2025 tarehe 13 Juni 2024 na kuangazia Kilimo, Biashara Ndogo, Biashara Ndogo na za Kati (MSME), Nyumba na Makazi, Huduma ya Afya na Barabara kuu ya Dijiti na tasnia ya ubunifu.
EU yaingiza €56 Milioni za maombi ya viza yaliyokataliwa kutoka nchi za Afrika
EU yaingiza €56 Milioni za maombi ya viza yaliyokataliwa kutoka nchi za Afrika
Kihistoria, Waafrika wamekuwa wakiongoza katika kuwasilisha maomba ya viza ya Shengen. Licha ya kuwa na idadi kubwa ya maombi, lakini pia, maombi yao yanaongoza kukataliwa, huku Algeria ikiwa mstari wa mbele kunyimwa viza ya Shengen.
Nini kingine ungependa kujua

Vijana waliochoshwa na vita DRC wapata faraja mchezo wa kuteleza
Katika Picha: Vijana waliochoshwa na vita DRC wapata faraja mchezo wa kuteleza
Kenya yatangaza ubinafsishaji wa makampuni yake ya serikali
Kenya yatangaza ubinafsishaji wa makampuni yake ya serikali
Mke wa Rais wa Kenya kupanda miti milioni 500 Ndani ya miaka tisa.
Mke wa Rais wa Kenya kupanda miti milioni 500 Ndani ya miaka tisa.
Hussein Mwinyi: Chakula kipo cha kutosha
Hussein Mwinyi: Chakula kipo cha kutosha
Serikali za Kenya na Uganda zatangaza tahadhari katika mipaka yao.
Serikali za Kenya na Uganda zatangaza tahadhari katika mipaka yao.
Maarufu
Vijana waliochoshwa na vita DRC wapata faraja mchezo wa kuteleza
DRC: Jeshi la Kongo lataka ushirikiano wa raia ili kuwadhibiti wanamgambo
Ukame wapelekea changamoto ya kiafya nchini Somalia
Kenya yatangaza ubinafsishaji wa makampuni yake ya serikali
Raia wa Nigeria waanza mfungo wa Ramadhani huku kukiwa na uhaba wa noti za benki.

OUR PRODUCTS:
Cantona Digital
Queens Safaris
SkizaRecords
FBE Records
FBE Photography
FBE Brands& Events Management Ltd

Let’s do Business/Let’s Build Brands.

Build Brands for Generations.

All Rights|Reserved ©|Cantona Group Ltd

Discover more from cantonadigital

Subscribe to get the latest posts sent to your email.

Leave a comment