Maelekezo mapya Kenya  baada ya hakimu kupigwa risasi

Vurumai hiyo imetokea Juni 13, 2024, ambapo mmoja wa maafisa wa polisi mwandamizi ambae mke wake alifutiwa dhamana baada ya mshtakiwa kukiuka masharti ya dhamana alimpiga risasi hakimu.

Jaji mkuu Kenya Martha Koome atoa maelekezo mapoya baada ya hakimu kupigwa risasi / Picha kutoka  Martha Koome

Mahakama Kuu nchini Kenya, imelaani kitendo cha kushambuliwa kwa risasi kwa Hakimu wa Mahakama ya Makadara, iliyopo jijini Nairobi nchini Kenya. Katika taarifa ya vyombo vya habari iliyotolewa na Ofisi ya Mahakama Kuu nchini humo, imeonyesha kusikitishwa kwake na shambulizi hilo lilisababisha kujeruhiwa kwa Hakimu Monica Kivuti.

“Nimejulishwa kuhusu tukio la kushambuliwa kwa risasi katika Mahakama ya Makadara lililohusisha afisa polisi mwandamizi na kumsababishia majeruha Hakimu Monica Kivuti. Mahakama inalaamu tukio hili, na inataka vikosi vya usalama vya taifa kukabiliana na hali hii haraka iwezekanavyo,” Jaji mkuu Martha Koome amesema katika taarifa.

Vurumai hiyo imetokea Juni 13, 2024, ambapo mmoja wa maafisa wa polisi mwandamizi ambae mke wake alifutiwa dhamana baada ya mshtakiwa kukiuka masharti ya dhamana alimpiga risasi hakimu.

Baada ya uamuzi huo kutolewa, ndipo askari huyo alipomfyatulia risasi hakimu na kumjeruhi vibaya mguuni.Hata hivyo, afisa huyo alijibiwa kwa mashambulizi kutoka kwa maafisa wengine waliokuwa katika eneo hilo, na hatimae kukimbizwa hospitali kwa ajili ya matibabu.

Masharti mapya ya mahakamani

Jaji mkuu ametoa maelekezo mapya kwa ajili ya usalama mahakamani.

” Kitengo cha polisi cha mahakama pamoja na mkuu wa polisi nchini Kenya wameelekezwa kuongeza usalama katika viyuo vyote vya mahakama nchini kote. Pia wameambia kuhakikisha kuwa ni maafisa wa polisi ambao wamesajiliwa na mahakama tu ambao wanaruhusiwa kutoa usalama katiak vituo hivi,” Koome amesema.

Jaji mkuu pia ameongezea kuwa mahakama ya Makadara ambapo kisa cha hakimu kupigwa risasi kilitokea itafungwa hado tarehe 17 Juni 2024, na kesi zote ambazo zilifaa kusikizwa katika mahakama hiyo zitasikilizwa kupitia njia ya mitandaoni.

Kamati ya usalama ya mahakama itaangalia tena jinsi ya kuimarisha maswala ya kuboresha usalama katiak kila kituo cha mahakama nchini.

Maafisa wa usalama wa mahakama watapewa mafunzo spesheli.

Habari zinazohusiana

Katika Picha: Vijana waliochoshwa na vita DRC wapata faraja mchezo wa kuteleza

Katika Picha: Vijana waliochoshwa na vita DRC wapata faraja mchezo wa kuteleza

Huku kukiwa na operesheni za kijeshi zinazoendelea nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo za kung’oa makundi ya waasi, kijana mmoja anatoa suluhu la kipekee ili kupunguza msongo wa mawazo na kukabiliana na uhalifu mijini

Kenya yatangaza ubinafsishaji wa makampuni yake ya serikali

Kenya yatangaza ubinafsishaji wa makampuni yake ya serikali

Baraza la mawaziri la Kenya limeidhinisha mswada mpya wa Ubinafsishaji ambao utawezesha nchi kubinafsisha baadhi ya mashirika ya serikali.

Mke wa Rais wa Kenya kupanda miti milioni 500 Ndani ya miaka tisa.

Mke wa Rais wa Kenya kupanda miti milioni 500 Ndani ya miaka tisa.

Serikali ya Kenya kupitia mke wa Rais yajidhatiti kukabiliana na mabadiliko ya Tabia ya nchi kwa kupanda miti zaidi ya bilioni 15 kufikia mwaka 2032

Serikali za Kenya na Uganda zatangaza tahadhari katika mipaka yao.

Serikali za Kenya na Uganda zatangaza tahadhari katika mipaka yao.

Tahadhari na vizuizi vya wekwa katika mipaka ya kenya na Uganda siku chache tangu Tanzania ithibitishe kuwa na watu waliopata maambukizi ya virusi vya Marburg.

Makala yanayovuma katika kategoria hii

Bajeti ya Tanzania yaangazia zaidi uzalishaji wa ndani

Bajeti ya Tanzania yaangazia zaidi uzalishaji wa ndani

Sekta zilizonufaika kwa bajeti ni pamoja na viwanda vya maji, kilimo, madini na michezo hasa soka.

Bajeti ya Kenya iliangazia nini?

Bajeti ya Kenya iliangazia nini?

Kenya ilisoma bajeti yake ya mwaka 2024/2025 tarehe 13 Juni 2024 na kuangazia Kilimo, Biashara Ndogo, Biashara Ndogo na za Kati (MSME), Nyumba na Makazi, Huduma ya Afya na Barabara kuu ya Dijiti na tasnia ya ubunifu.

OUR PRODUCTS:

Cantona Digital

Queens Safaris

SkizaRecords

FBE Records

FBE Photography

FBE Brands& Events Management Ltd

Let’s do Business/Let’s Build Brands.

Building Brands for Generations.

All Rights|Reserved|Cantona Group Ltd|©2024


Discover more from cantonadigital

Subscribe to get the latest posts sent to your email.

Leave a comment