Tenisi: Kenya yajikwaa kupandishwa daraja ya Billie Jean kwa kichapo cha Nigeria
Nairobi, Kenya – Nigeria iliishinda Kenya mechi 2-1 siku ya Alhamisi na kupata faida ya mapema katika mbio za kupandishwa daraja.
Kwa mwaka wa pili mfululizo, matumaini ya Kenya kupandishwa daraja kutoka kundi la tatu hadi la pili katika Kombe la Billie Jean King yalipata kipigo mikononi mwa Nigeria ambao waliwasababishia kichapo cha mechi 2-1 dhidi ya wenyeji wa michuano hiyo ya 2024 inayofanyika katika uwanja wa Nairobi Club jijini Nairobi nchini Kenya.
Kenya ilikuwa imepoteza mechi ya ufunguzi wakati Barakat Quadre Oyinlomo alitumia dakika 57 tu kumlaza Alicia Owegi kwa ushindi wa seti 2-0 za 6-0, 6-1. Ila baadaye bingwa wa Afrika Angella Okutoyi alirejesha usawa kwa nchi yake kwa kumchapa Adesuwa Osabuohien 6-3, 6-3 ili kuhakikisha usawa huo ungehitaji kuamuliwa katika mechi ya wachezaji wawili kila upande (doubles).
Nahodha wa timu ya Kenya, Francis Rogoi alichagua kuchezesha Okutoyi na pacha wake Roselida Asumwa kwa matumaini kwamba wawili hao wataibeba timu hiyo kwenye mechi muhimu huku Nigeria ikiendelea na ushirikiano wa Adesuwa na Barakat.

Baada ya kuanza vizuri katika dakika za ufunguzi leo, Kenya ilitengeneza nafasi ya kwanza ya kupata alama katika mechi ya tatu lakini Nigeria wakazima hatari hiyo haraka kwa kurejea mchezoni.
Ghafla bin vu, Kenya ilibadilisha mkondo wa kushambulia na kuanza kushambuliwa meza zikibadilika katika mchezo uliofuata huku Nigeria ikibadilisha pointi yake ya kwanza ya mapumziko katika seti na kuongoza 3-1.]
Hata hivyo, wenyeji, wakiungwa mkono na sehemu kubwa ya mashabiki, walirudi wakichaji mara moja huku wakifanikiwa kupata mapumziko ya alama.

Nigeria hata hivyo walifanikiwa kumenyana na Kenya kwa mara nyingine katika mchezo wa nane walipoongoza kwa alama 5-3 katika mara ya pili ya kubisha huu Asumwa akihangaika kwenye kupakua mipira ya kwanza.
Wenyeji hao wa Afrika Magharibi walifanikiwa kuchukua seti ya kwanza 6-3. Seti ya pili ilionyesha ushindani mkali huku Kenya ikiazimia kutopoteza bila ya kuonyesha makucha yake.
Walipata mwanzo mzuri walipoiyumbisha Nigeria katika mchezo wa pili lakini hawakuweza kuvumilia na hali hiyo ilitokea walipofanikiwa kupenya tena katika mchezo wa sita, na kulazimisha mechi hiyo kwa sare ya bila kufungana ambayo Nigeria ilishinda 7-5 na kuchukua hatua muhimu kwenye harakati ya kupandishwa daraja.
“Kujitayarisha vyema kisaikolojia kulichangia, tulipanga sehemu maalum ya kupiga mipira, namna ya kupakua na wachezaji kujiamini,” alifichua kocha wa Nigeria, Rotimi Akinloye.

“Imekuwa siku ngumu katika michezo kwetu. Tulitoka 0-1 kwenye mechi ya kwanza lakini tuliweza kurejea na kuwa 1-1. Mechi ya mwisho ambayo ilikuwa ya maamuzi ilikuwa na changamaoto kidogo na shinikizo na mipira michache ilitugharimu mechi ili tupate matokeo,” kocha wa Kenya Francis Rogoi alikadiria.
“Kucheza na wenyeji si rahisi, tulijua watakua na presha kwa hivyo tukajituma zaidi na mwishowe tumepata matokeo bora,” aliongeza kocha Akinloye.
Fuatilia habari zote za kimataifa kwa kupakua App ya RFI
“Inapendeza sana, tulikuja kushinda. Mwaka jana tulipoteza mechi kadhaa na tulijifunza, mwaka huu tunayafanyia kazi,” alisema kwa furaha Barakat Oyinlomo.
Hata hivyo, bado hatujapoteza matumaini, mwaka jana tuliifunga Morocco mechi ya kwanza lakini wao ndio waliofuzu. Kwa hivyo mchezo bado unaendelea na mechi za mchujo katika kundi lolote hutokea na tunataka kupata ahueni na kujiandaa vyema. Ikiwa tutaweza kufanya makubwa Jumamosi basi kila kitu kitakuwa sawa,” Rogoi alisema na matumaini makubwa.

Kenya itakuwa na siku ya mapumziko Ijumaa huku Nigeria ikichuana na Afrika Kusini.
“Afrika Kusini! Lazima tumakinike asilimia mia, nguvu zetu ziwe juu,” alisema Adesuwa.
Kenya itahitaji Afrika Kusini kuiadhibu Nigeria kwa kipigo kikubwa ili kupata nafasi yoyote ya kupandishwa daraja watakapochuana na Afrika Kusini siku ya Jumamosi.
Kusambaza :
Soma zaidi mada inayofanana:
Kuhusu mada hiyohiyo

BILIE JEAN KING CUP
Tenisi: Kenya yajikwaa kupandishwa daraja ya Billie Jean kwa kichapo cha Nigeria

Ujerumani: Terzic anaondoka kwenye wadhifa wake kama kocha wa Borussia Dortmund
Kenya: Lionesses kutafuta tiketi ya Olimpiki katika mashindano ya Repechage

BILIE JEAN KING CUP
Tenisi: Kenya, Afrika Kusini na Nigeria zafuzu mchujo wa Billie Jean King Cup

Ancelotti: Real Madrid haitashiriki michuano mipya ya klabu bingwa ya dunia

Tenisi: Jannik Sinner anakuwa mchezaji wa kwanza wa Italia nambari moja katika historia

Kenya, DRC kabaruani, Cameroon yafanya kweli mechi za kufuzu kombe la dunia la FIFA

Rwanda yapoteza ugenini, mechi za kufuzu fainali za kombe la dunia

Mechi za mataifa ya Afrika kufuzu kwa kombe la dunia zinaendelea

KENYA RAGA
Kenya 7s yatuzwa kibabe huku ikilenga maandalizi ya Olimpiki

Kandanda: Mshambulizi wa Ufaransa Kylian Mbappé hatimaye ajiunga na klabu ya Real Madrid

Ndtoungou Mpilé na David Pagou wakataa uteuzi wa Samuel Eto’o

Timu ya Al Ahly ya Misri yashinda tena Ligi ya
- Israeli
- EAC
- DRC
- Palestina
- Matangazo ya dunia
OUR PRODUCTS:
Cantona Digital
Queens Safaris
SkizaRecords
FBE Records
FBE Photography
FBE Brands& Events Management Ltd
Let’s do Business/Let’s Build Brands.
Build Brands for Generations.
All Rights|Reserved ©|Cantona Group Ltd
Discover more from cantonadigital
Subscribe to get the latest posts sent to your email.