kuna wakati unahitaji neno moja tu, kufanya mambo makubwa. Unahitaji kupewa moyo na mtu mmoja tu, kupata courage ya kufanya, kitu ambacho umekwama kufanya muda mrefu.
Inawezekana umezoea kufanya, kitu fulani kwa muda mrefu, anaweza kutokea mtu mmoja, akakwambia nguvu yako, iko sehemu fulani.
Tunawahitaji sana, hawa watu. Watu ambao watakwambia unaweza. Watu ambao watakwambia fanya hivi ili ukue. Watu wenye mawazo chanya. Watu ambao watakupa mbinu zaidi.
Kwenye kitabu cha The Meaning of Mariah Carey, Mariah Carey anasema rafiki yake, wakiwa wadogo kabisa alimwambia- akiimba ni kama mchanganyiko wa ala tofauti muziki. Anasema, ni moja kati ya watu waliomfanya aiendee fani ya muziki.
Kwenye kitabu cha Ikigai, Hector Garcia mmoja ya mwandishi, anasema aliwahi kuambiwa, kwamba ana uwezo wa kukusanya habari mbali mbali na akaandika summary kwa weledi mkubwa. Na kuanzia hapo akaamini kuwa anaweza kuwa mwandishi.
Kwa maneno yake mwenyewe anasema. _Sometimes people need someone in their lives to confirm to them that they are on the right path_.
Wewe huwa unakutana, na watu gani? Watu huwa wanakwambia nini,? Na wewe huwa unawaambia nini watu wanapotaka ushauri.?
OUR PRODUCTS:
Cantona Digital
Queens Safaris
SkizaRecords
FBE Records
FBE Photography
FBE Brands& Events Management Ltd
Let’s do Business/Let’s Build Brands.
Build Brands for Generations.
All Rights|Reserved ©|Cantona Group Ltd
Discover more from cantonadigital
Subscribe to get the latest posts sent to your email.