Leo tunangazia mada muhimu Siri tatu muhimu,kuhusu fedha. Kumbuka mafanikio ni haki yako ya kuzaliwa.
Lakini hakuna atakaye kulazimisha wewe ufanikiwe.
Siri tatu muhimu ya fedha matajiri wanajua lakini maskini hawajui,hivi ni vitu vipi.
Vipo wazi lakini inakua siri maana wengi hawajui hilo.Nimeviweka katika vikundi vitatu.
Pata maarifa haya leo,fedha inazungumziwa na Kila mtu hata watoto wadogo,ukitaja fedha tu wanatabasamu.Hata mtu yule hajui kusoma na kuandika anazungumzia fedha na anajua kuhesabu. Fedha inamtazamo Fulani hasi.Zamani ulipokua unazungumzia fedha wengine utasikia wakisema fedha si nzuri ni chanzo cha majaribu mengi.Watu walikaa kimya hawakuzungumzia fedha hadharani.Hii ilikuja kuwa na madhara katika jamii.Maana watoto wengi walikosa elimu ya fedha.Ndio maana wengi wakipata fedha ndio majaribu yanakua mengi.Ndio wengi wanapitia maisha magumu na kukosa kuendelea kupanga maisha yao ya baadae. Ukijua vitu ukavitendea kazi fedha ni nzuri itakutumikia.
Fedha ni wazo:Mbona niseme hivi,Fedha si karatasi,fedha inaanza mawazoni wakati mwingine nasikia watu wakisema nikipata fedha nyingi ndiposa nitatekeleza hili na lile.Swali ni je mbona wezi wengi ni maskini anayeshinda bahati na sibu angali na madeni mengi.Hawana kitu cha kujivunia.Ndio amepata fedha haraka mawazoni Hana malengo hatimaye anarejelea umaskini. Tatizo si fedha ni mawazoni. Fedha ni mbegu,ukiwa na wazo au ukishindwa unatumika Kama daraja kuelekeza pesa kwa mwingine akatendee kazi hizo fedha. Wengi wana mawazo nitaenda kazini mwisho wa mwezi nitapata fedha nilipe madeni hadi mwisho wa mwezi nitalipa hili au Lile,nikikosa nitakopa,nitalipa.Hilo wazo halitakufanya uondoke katika utumwa wa kukosa.Ni vizuri unapokua na fedha panga kazi yako anza biashara fanya ukulima fedha ulizo nazo zikakutendea kazi.Ukiwa na wazo la kutofanya kitu utaishi Kama maskini.Hilo halina mjadala,unitaka ufanikiwe maishani ni kuomba Mungu akupe mawazo na kibali,Tia bidii ekeza ukipata mtaji au kusanya kichache ulicho nacho kikutendee haki.
Kuwa na mawazo endelevu.Unapolalamika Kila siku unachokipata ni kichache swali ni je ulipo kipata ulikitendea kazi.Hiyo ina maana hata ukipata kikubwa utatumia vibaya. Ushauri wangu badilisha mawazo yako kuhusu fedha,wacha kuona fedha Kama shetani,usione fedha ni kitu cha kupata unatumia pasipo kuekeza.Fedha inayopita mikononi mwako hata Kama ni kidogo isipite yote.Fikiria ekeza zilizosalia iwe ya matumizi na fungu la kumi.Biashara nyingi unaweza anza na fedha kidogo.

FortuneBaraka Photography 
FortuneBaraka Photography
Siri ya pili:Fedha inafuata thamani,hapa Kuna tofauti kubwa ya uelewa.Wakati unaanza kuelewa kwa kiwango cha kawaida pasipo kujituma inakua ni balaa katika biashara yako au kazi au taaluma uliyo ndani.Ni Bora uongeze thamani ili uwe bora.Fedha inafuata thamani,mzunguko mzima wa uchumi duniani unategemea thamani yake.Kitu cha thamani kina gharama.Ongeza thamani ya unachokifanya.Unapofanya kazi usijipendekeze kwa yeyote.Tia bidii boresha thamani yako.
Fedha ni mtumwa mzuri,unapotaka kitu unatumia mtu na unamlipa.Maskini ni mtumwa wa fedha ndio maana wakipata fedha wanachanganyikiwa hawezi akatulia,utashangaa ananunua hiki au kile.Ameenda mjini ananunua rundo la nguo. Mfuko umejaa bidha za matumizi,unaposema naye majibu hizi ni fedha za bahati nasibu nisipo nunua hiki au kile uenda kesho nikakosa pesa itakua imekwisha.Hapo kwangu ni utumwa wa fedha.Fedha inafaa ikufanyie kazi,tumia fedha kuekeza,zungumza na fedha itume ikatende kazi hiyo ni hatua ya imani.Sema wewe ni mtumwa wangu.Panga unachotaka kukitekeleza,nataka hii fedha izalishie zaidi,wacha iwe mbegu,ekeza.Umaskini ni wakati wewe unaifanyia kazi fedha na utajiri wakati fedha inakufanyia kazi.
Discover more from cantonadigital
Subscribe to get the latest posts sent to your email.