Siku yako ya mafanikio ipo karibu Sana usikate tamaa.

Kama hujawai kukutana na changamoto maishani mwako fahamu hujakamilika, changamoto hufanya mtu aendelee kukua na kufikia hazma aliyonayo.
Changamoto humjenga na kumwimarisha mtu.
Mtangulize na kumshukuru Mungu kwa Kila hatua unayopiga maishani mwako.
Mimi namshukuru Mungu kwa sababu ya mengi tena namsifu sababu ya vingi.
Kabla maharagwe hayajapikwa, huchambuliwa kwanza, ambapo yale maharage yaliyo mabovu hutupiliwa mbali ili yale mazuri yaweze kupikwa.

Hata hivyo, mvua inapokuja, yale maharage mabovu yaliyotupwa ardhini hugeuka kuwa mbegu, humea, ikakua na kuchanua kuwa maharage mazuri tena.Maisha yetu kipindi Fulani ni mfano was maharagwe.Wakati Fulani tumadharauliwa kutengwa na hata kuonewa.Wakati huo mshukuru Mungu.

Na yule aliyeyajaji kuwa ni mabaya na kuyatupa huenda yatakapokomaa akavuna na kuyala kwa afya.

Na maisha ndivyo yalivyo, unaweza ukatengwa, ukasemwa, ukadharauliwa na kuumizwa vibaya na wale uliowaamini. Lakini, Je, ni nani ajuaye njia za Mwenyezi Mungu?

Hao hao waliokuumiza itatokea siku watakutazama wakitegemea la kheri kutoka kwako. Huenda wakakupigia magoti kabisa wakihitaji walau neno lako moja tu wapone!

Usijipe laana, usihuzunike wala usilie pale Dunia inapokuegemea. Ni suala la muda tu kupata Mvua yako ya baraka! Siku yako ya kufanikiwa ipo karibu Sana usikate tamaa.Endelea kumtumainia Bwana Yesu.

cantonajoseph

#Iposiku #GetInspired #TwapigaHatuaPamoja #CantonaJoseph’sMotivates. #CantonaJoseph’World #CantonaJosephIntMinistry

Links:

YouTube: Official Cantona Joseph.

Youtube:CantonaJoseph Int Online Media.

Contacts: Facebook CantonaJoseph, Tweeter @cantonajoseph

Istagram:cantona.joseph.

Email: cantona.online254@gmail.com

©2019 FortuneBaraka Entertainments|All rights


Discover more from cantonadigital

Subscribe to get the latest posts sent to your email.

Leave a comment