Dunia ina taaluma nyingi sana, ujuzi mwingi, vipaji vingi, wale wanaoheshimu hivyo huvitumia na kufanikiwa.
Yawezekana unawaza na unatamani uwe bora kuliko wengine unaofanya nao kazi ya aina moja, elimu moja, ujuzi mmoja na kipaji cha aina moja, lakini kila ukijaribu unajikuta kuna watu wanafanya vizuri zaidi na kufanya vizuri kwao kunakukatisha tamaa.
Jaribu siri hii itakusaidia, angalia katika unachokifanya ENEO GANI UKO VIZURI ZAIDI KISHA SHIKILIA HILO NA FANYA KWA NGUVU ZOTE, AKILI YOTE, NA MAARIFA YOTE TENA KWA BIDII SANA MPAKA UJIPAMBANUE WEWE NI BINGWA WA HILO ENEO. ukifanikiwa bila shaka kazi yako, huduma yako, kipaji chako, na taaluma yako itaonekana bora zaidi na utakuwa mfano wa kuigwa. Lakini ukitaka uonekana unayaweza yote huenda ukaishia kuwa mtu wa kawaida maana huwezi fanya kila kitu na ukapata ubora kwa kila kitu.
Mungu alipoumba ulimwengu alichagua watu wake na kuwapa urithi.Watu hao ndio hupigwa vita na njia yao yakufanikiwa kuwa ngumu sana .Watu hao ni wewe unae waza mambo makubwa lakini huoni ni wapi pakuanzia,ni wewe ambaye vita vyako haviishi una dhulumiwa unasingiziwa na kuonewa,ni wewe ambaye magonjwa yamekuandama kila siku hayaishi,ni wewe ambaye umekata tamaa ya kuishi na kuona kama huwezi tena kufanikiwa ukidhani umechelewa sana.
Sikiliza nikwambie shetani humlenga yule mwenye kitu yule ambaye Mungu ameweka jambo kubwa ndani yake hiyo misuko suko ni lengo la shetani ukate tamaa,kuna mtu mmoja anaitwa Nabothi alikua na shamba la mizabibu lakini ahabu mfalme alilitaka ili alime mboga lakini Nabothi akakataa akisema siwezi kukupa urithi wa baba zangu.
Ahabu akachukia mpaka akashindwa kula wala kupata usingizi,ndivyo ilivyo na kwako shetani amechukia sana kuona Mungu amekupa baraka kubwa kiasi hicho lakini kwakua huoni rohoni unajidharau na ndio maana unakata tamaa hiyo ni roho ameweka kwako ili ulicho nacho akiibe,natamka kuanzia sasa Roho hiyo iondoke na kukuacha huru ufikie malengo yako kwa Jina la Yesu.
Acha kuwa na mashaka na maombi yako.Dai urithi wako.Toka ulipo zaliwa Mungu alikuandalia maisha yenye baraka na mafanikio.Baraka zako zimefichwa gizani.Kuna mtu kazificha gizani na ndio maana neno linasema nitakupa hazina zilizofichwa gizani.Ukisimama kwa Mungu usiangalie umeshindwa mara ngapi,Tazama Ayubu wote walimkimbia akasema nimebakiza mmoja tu mtetezi wangu yu hai na ataniokoa.Mungu aliye hai akakupe hazina zako na kukutoa kwenye taabu na shida zako kwa Jina la Yesu.Endelea kumtegemea Mungu kwa lolote unalolifanya na hakika utafanikiwa.
Pokea mengi kutoka kwenye website yangu http://CantonaJoseph.wordpress.com
CantonaJosephMotivates. #Iposiku #Getlnspired #Itissettled

Discover more from cantonadigital
Subscribe to get the latest posts sent to your email.