Simama kama Daudi na utalishinda hilo tatizo

Shetani anapenda sana kutumia picha kuwa dhoofisha watu,alimtumia Goliathi kuwaogopesha wana wa Israel anaweza kutumia tatizo ulilonalo ili kukutisha usimuamini Mungu anaweza,si kweli yet Mungu anauwezo,ni mkuu saana.Simama kama Daudi na utalishinda hilo tatizo kwa Jina la Bwana wa Majeshi.
Bwana Mungu akawaambia wana wa Israel nitayapiga na kuyatoa mataifa makubwa mbele zenu ili mkamiliki mali zao na nchi zao,Nami leo nakutabiria ushindi na unakwenda kumiliki.Kila adui zako wakapigwe na mkono wa Mungu.
Watu wa Mungu tunaitwa taifa moja tena teule unaposikia Israel ni wewe ambaye Mungu kakuchagua tofauti na wasio mjua Mungu wanaitwa mataifa kwakua kila mmoja ana abudu miungu anayo ijua yeye,ni kweli watu wote ni wa Mungu lakini wapo ambao Mungu kawachagua,hata kama mtu yuko Uropa au Asia kama ana muamini Mungu wa Isaka,Ibrahimu na Yakobo anajulikana kama Taifa la Mungu kwaio wew na yeye ni kitu kimoja Imani yenu ni moja na mnamuomba Mungu mmoja aliye umba vitu vyote.Nawasalimu kwa Jina la Yesu ee Israel Taifa la Mungu popote mlipo ndani na nje ya nchi hii Mungu aendelee kuwalinda nyie ni masalia ambayo mtachipua na kuitisha dunia Mungu atawapa nguvu hiyo

Kufanya kazi ngumu unayoipenda kunaifanya ionekane kazi rahisi sana japo kwa uhalisia ni ngumu. Lakini kufanya kazi rahisi usiyoipenda kunaifanya kazi hiyo kuwa ngumu sana ingawa kikawaida ni kazi rahisi. Ugumu au urahisi hauko kwenye kazi yenyewe bali uko moyoni. Rekebisha moyo wako uanze kupenda unachopaswa kufanya.
Kubali kufanya kile Mungu anataka ufanye na ukipende kwa moyo wako ili ukifanye sawasawa na ulivyo na kinavyotakiwa kuwa.Usiruhusu shetani achore picha yakulemaza mawazo yako hilo unalolifanya haliwezekani,yote yanawezekana ukijiamini.Chukua hatua leo.Tamka katika jina la yesu yanawezekana.Mwamini Mungu ufukara utakwisha,majuto yamekwisha unamiliki mambo makubwa.Wewe ni mteule,jeshi kubwa.

#Iposiku. #TwapigaHatuaPamoja. #CantonaJosephMotivates. #CantonaJoseph’sWorld #CantonaJosephIntMinistries

All rights reserved ©2019


Discover more from cantonadigital

Subscribe to get the latest posts sent to your email.

Leave a comment