Ni bora kupendana mnapokubaliana kuishi pamoja katika ndoa.Mda mlio nao ni mchache sana.

Wanandoa msipoteze mda mliopewa na Mungu kuishi pamoja kunyanyasana nakugombana.Leo hebu tusome

AYUBU14 :1-2
Mwanadamu aliye zaliwa na mwanamke siku zake za kuishi si nyingi, naye hujaa taabu, yeye huchanua kama vile ua, kisha hukatwa, hukimbia kama kivuli, wala hakai kamwe.
Mpende uliye naye na muonyeshe mapenzi ya kweli, kwani kuna siku ataondoka na utatafuta wa kumuonyesha mapenzi ya kweli hutampata.
Si kila mtu anafaa kuwa mke au kuwa mume. Wewe uliye na mke au mume wako hivi sasa, huwezi kuelewe kwa haraka; ila mjane aliyepoteza mume au mjane aliyepoteza mke anaelewa nyakati anazopitia. Anatamani amuamshe mwenzake amuonyeshe upendo, ila ndiyo haiwezekani tena.
Kuna Siri kubwa mbele za Mungu ya kuishi wawili, na ndio sehemu ya kumalizia maisha yako ukiwa duniani; maana ulisha zaliwa, ukakua ukatengana na wazazi. Sasa penye maisha ya mwisho kabla ya kuitwa na Mungu ni NDOA. Ndiyo maana andiko linasema:
WAEFESO 5 :31-33
Kwa sababu hiyo mtu atamwacha baba yake na mama yake, ataambatana na mkewe, na hao wawili watakuwa mwili mmoja. Siri hiyo ni kubwa ila mimi nanena habari ya kristo na kanisa. Lakini kila mtu ampende mke wake kama nafsi yake mwenyewe, wala mke asikose kumstahi mumewe.
Watu wengi wanachezea upendo wanaopewa leo na wake zao, au waume zao, kwa kuwa wanadhani hautakoma; siku ukikoma utajutaa… Kuna siku utatamani kumwambia mume wako au mke wako kuwa unampenda, lakini hatakuwepo!
Mpambe mwenzio kwa maua kwa sasa akiwa hai,akiona kwa macho yake kwamba maua yako ni upendo.Usisubiri kupamba kaburi lake kwa maua,haitasaidia tena. Kwa Nini unatumia mda wako mwingi kutengeneza ugomvi,chuki na manyanyaso kwa mkeo au mumeo?
Mrudie mkeo au mumeo mlioachana;na mlio ndani ya ndoa rudisheni amani.Mungu anasema na nyie wanandoa kupitia ujumbe huu.

#Iposiku #TwapigaHatuaPamoja. #CantonaJosephMotivates. #CantonaJoseph’sWorld. #CantonaJosephIntMinistries. #Getinspired.

All rights reserved ©2019


Discover more from cantonadigital

Subscribe to get the latest posts sent to your email.

Leave a comment