Watu wengi wanaingia kwenye shida nyingi bila kujua chanzo.
Wakati Yakobo amemkimbia Esau alifika nchi ya Luzu na usiku huo akalala hapo akaota ndoto malaika wanapanda na kushuka katika eneo hilo alipo amka asubuhi akaogopa sana na akajua eneo hilo kuna uwepo wa Mungu akasema Mungu ukinibariki huko niendako nami nitarudi hapa na kuweka madhabahu.
Yawezekana umejenga nyumba lakini umeshindwa kukaa,umeanzisha biashara kwa mtaji mkubwa sana lakini imekua tofauti na matarajio yako hivyo ujue eneo hilo kuna uwepo wa kipepo ni ngumu kufanikiwa mpaka maombi maalum ya kukomboa ardhi hiyo au toka umehamia eneo fulani hupati mafanikio hapo tambua eneo hilo linahitaji ukombozi wa Damu ya Yesu.
Toka uhamie kwenye nyumba yako mpya ni maruwe ruwe tu na ndoto za ajabu unaota,unahitaji maombi.Yakobo alipo ota alikua amelala porini kabisa hakuna hata nyumba lakini hapo palikua ni sehemu ambako Mungu yuko hata wewe umejenga au umeanzisha biashara sehemu fulani au umenunua kiwanja nje ya mji jua hapo kuna madhabahu ipo kama sio ya Mungu basi ya shetani kuna watu wamekimbia nyumba zao au kuna eneo unaweza kwenda kununua lakini eneo hilo kila anayejaribu kujenga hapo anakufa kila akinyanyua nyumba kufikia sehemu fulani anakufa ujue hapo ni lango la shetani huwezi kuishi mpaka msaada wa Mungu.Kuna kitu tunajifunza pale Mungu alipo wakumbusha wana Israel kwenye safari yao ya nchi yaahadi,kwani mwanadamu ana asili ya kusahau aliwavusha bahari ya shamu kwa kuigawa katikati,walitembea jangwani mda miaka arobaini (40 ) bila viatu wala nguo zao kuchakaa(Kumb 8:3-4),tendo ilo lilikuwa si la kibinadamu na lilikuwa lakushangaza ni jambo gani wewe ulishawahi kushindwa .
Mungu alikuwezesha,wakati wa shida yako,iwe ugonjwa au uchumi kuyumba au ajali, hebu kumbuka ili upate nguvu ya kumwamini Mungu tena na nguvu zake,Daudi aliweza kumkabili Goliath vile alivyo kuwa akikumbuka alivyowaua dubu na simba waliokuwa wanashambulia kondoo wa baba yake akuutazama uwezo wa Goliathi ila alitembea na nguvu ya Bwana iliyo muwezesha kuua dubu na simba uko nyuma,Neno hili liinue imani yako kwa kila unalo liona gumu mbele yako naituma nguvu ya Roho Mtakatifu ikaangushe kila kilichoinuka mbele yako kwa jina la Yesu (1 Samwl 17:34-36)
Wakati Yesu anasema anautangaza mwaka wa mateka na wafungwa kuachiwa huru hakuwa ana maanisha wafungwa wa Kamiti au Shimo la Tewa, hapana shetani amefunga fahamu za watu minyororo,unaweza kupata neema ya kuingia kanisani lakini huelewi neno la Mungu au unaweza kumuabudu Mungu lakini hujui ni Mungu gani unaemuabudu watu wametekwa na mambo ya kidunia kuna mambo wanayaamini sana kuliko hata Mungu,watu wanasumbuliwa na mapepo miaka mingi wana magonjwa ya miaka mingi wana ukomo wa maisha kwa miaka mingi shetani amewafanya watumwa amewafunga fahamu zao na maisha yao hata nikisema Yesu anaokoa hawaelewi hata kidogo.Lakini kwa neno hili la Leo Mungu akakupe kibali cha kulijua neno lake kila aliye mateka akawe huru kwa Jina la Yesu Kristo.
Mwanzoni wakati umempokea Yesu na ukawa unamuamini Mungu ulianza kuona mambo ni mepesi,magonjwa uliyokuwa nayo yalitoweka ulipo ombewa,mapepo yakakimbia ukabaki salama na ukafurahi kuwa ndani ya wokovu lakini kuna watu wako makanisani wakiendelea kumuomba Mungu zile shida zao zimerudia tena yale magonjwa yao hayapati nafuu mpaka umekata tamaa ya kuomba tena umeamua kutumia njia nyingine ili uweze kupona.
Nisikilize nikwambie Neno linasema Ufalme wa Mbinguni unafananishwa na mtu aliyelima shamba akapanda mbegu nzuri lakini usiku alipo lala adui akaja akapanda magugu kwenye shamba lake maana yake ni kwamba kuna wakati ulikua umeishika imani vizuri unaenenda yale yanayofaa lakini kuna mahali ulijisahau ukalala ndipo hapo shetani alipokuja kukupandia magonjwa tena ndio maana unaweza kujiuliza mbona naomba sana lakini hili tatizo mbona halainiishi kumbuka kuna sehemu ulilala kama mwanzo ulikua una omba sana baadae
ulipunguza ukizani shetani umesha muweza na hawezi kukufata tena.Kama mwanzo ulikua unafunga na kuomba ulipoona afadhali kidogo ukaacha kufunga huo ndio usingizi ulio lala umeanza kuwa na majukumu ya maisha, na mambo yako kisa umepata nafuu ya ugonjwa wako huo ndio usingizi ulilala umeanza kuwa hauendi kanisani huo ndio usingizi ulilala alafu unaanza kusema kisha unaanza kushutumu, haya makanisa hata ukiombewa tatizo linarudi tu hapana wewe ndio umelala usingizi unakuja kushituka magugu yamejaa shida zimejaa kwenye familia yako umaskini umekita mizizi,familia ni ugomvi ni kwa sababu ulianza alafu ukalala bila kuendelea.
Ni maombi yangu kwako leo Mungu ananiambia ni wengi ambao shetani amepanda magugu kwenye maisha yao na bila kujua wanamkufuru Mungu kwa kulalamika.Usilalamike jinsi wana waisraeli walivyo lalamika hata kusahau Mungu alitengeneza njia katika bahari ya shamu na akawavusha salama huku maadui wao wote wakaangamia. Mungu hakufurahia na hatua yao kutengeneza sanamu badala ya kumwabudu yeye.Tafuta ufalme wa Mungu na hayo mengine yote utazidishiwa.
Pokea mengi kutoka kwenye website yangu http://CantonaJoseph.wordpress.com
CantonaJosephMotivates. #Iposiku #Getlnspired #Itissettled

Discover more from cantonadigital
Subscribe to get the latest posts sent to your email.