[Soma Mpaka Mwisho] Kwenye kila MAJIRA ya maisha yako, kuna mtu anakuwa ameandaliwa kuwa MFARIJI WAKO (Comforter).
Mtu huyu anakuwa amepewa moyo wa kukuonea huruma ya kipekee…
…na huwa yuko tayari kutumia MUDA wake kukufariji.
Mara nyingi sana watu wa namna hii wanaweza kuonekana kuwa ni wa kawaida sana na pengine HAWANA PESA, CHEO au MALI.
Unachotakiwa kujua ni kuwa, watu wa namna hii, huwa hawajaletwa KUKUPA VITU…
…ila wameletwa KUKUPA FARAJA ambayo wenye mali, pesa na cheo hawawezi kukupa.
Watu hawa wanaweza wasiwe na wewe kila siku, inawezekana sio watu ambao unawapa kipaumbele…
..ila MUNGU amewapa NGUVU ya KUKUVUSHA kwenye MAGUMU YAKO.
Hawa ni wale ambao ukiongea nao, ukitumia muda nao au ukiwaona…
…au kuwasikiliza huwa unajihisi kama kuna MZIGO MKUBWA umeondolewa kwako.
Changamoto ya watu wengi, huwa watu hawa tunawasahau kabisa wakishatusaidia na huwa hatuwapi nafasi tena.
Hata kwa sasa kwenye maisha yako kuna mtu wa namna hii AMEANDALIWA na AMETUMWA kwako.
Usikimbilie kutafuta msaada kwa wenye pesa, mali na vyeo tu…
…muombe Mungu akufungue MACHO yako umuone mtu wa namna hii pia, unamuhitaji sana.
Kama umejifunza kitu kupitia ujumbe huu naomba chukua hatua mpigie simu, mtumie meseji na kumshukuru aina hii ya mtu…
…ambaye Mungu aliwahi kumtumia kukuvusha katika magumu.
Kama utafanya hivyo comment maneno “Nitamshukuru”
Unaweza kumtaja pia kwenye comment aone moyo wako wa shukrani.
All Rights Reserved|©Cantona Group Ltd
Discover more from cantonadigital
Subscribe to get the latest posts sent to your email.