Usipuuzie Maumivu Yako, Madhara Yanayoletwa Na Maumivu Ya Moyo.
____1. Kutoamini watu wanaopaswa kuaminika.
Kuna watu kwa sababu walishawahi kuumizwa huko nyuma…
…imeua kabisa uwezo wao wa kuamini watu.
Wale ambao waliwahi kuumizwa kwenye mahusiano na wakasalitiwa…
Au walikuwa na ubia kwenye biashara na mtu kisha wakadhulumiwa…
…imekuwa ngumu kumwamini mtu ambaye hana tatizo lolote lile.
Madhara haya yamewaathiri sana kwa sababu…
…wamepoteza watu ambao wangeweza kuwa msaada kwa sababu hawaamini kila mtu.
Imekuwa haiwezekani kwa wao kufanya kitu kizuri na watu wapya wanaokuja kwenye maisha yao.
Hivyo kuna watu ambao wamefukuza watu muhimu kwenye maisha yao…
…kwa sababu wamejumlisha kila mtu kwenye mkumbo wa yule ambaye aliwasababishia maumivu.
Wengine wanaweza kuchukua watu wa Taifa fulani…
Kabila…
Jinsia…
Au Dini…
Kwa sababu tu kuna mtu mmoja kutoka kwenye hilo kundi aliwaumiza.
Hii inasababisha hata kama kuna mtu mzuri anakuja kwenye maisha yao…
…hawawezi kumpa nafasi na hawawezi kufaidika naye.
Je wewe ni mmoja wa watu wanaopitia changamoto ya Maumivu Ya Moyo?
Inawezekana ULIACHWA na unayempenda.
Au ULIKATALIWA na mzazi ukiwa mdogo.
Au Umezulumiwa na ambaye HUKUMTEGEMEA na una majukumu yanakuangalia.
Na mengine mengi.
POLE kwa hali unayopitia
All Rights Reserved|Cantona Group Ltd
Discover more from cantonadigital
Subscribe to get the latest posts sent to your email.