Kitabu cha “Tuesday with Morrie: An Old Man, A Young Man and Life’s Greatest Lesson”…
…kimeeleza moja ya kanuni muhimu sana ya maisha ambayo kila mtu anatakiwa kuizingatia.
Kitabu hiki kimetoa stori ya kijana mmoja ambaye baada ya kumaliza masomo yake na kufanikiwa sana kimaisha…
…alikuja kukutana na mwalimu wake Professor Morrie ambaye alikuwa ni mzee sana wakati huo na anakaribia kufariki.
Kijana huyu aliamua kuwa kila Jumanne atakuwa anamtembelea professor Morrie ili kupata hekima za maisha kabla hajafariki.
Katika masomo yote aliyopewa anasema somo kubwa ni lile ambalo alimfundisha jinsi ya kuishi bila majuto.
(How to Avoid the Life of regrets) ambapo alimwambia sentensi hii…
…“Once you learn how to die, you learn how to live”
(Ukiwa karibu na kufa ndipo unapogundua mambo ya msingi ya kufanya ukiwa hai).
Somo kubwa hapa lilikuwa ni umuhimu wa kufurahia kila baraka ambayo Mungu amekupa kila siku ya maisha yako hata kama kuna baraka kubwa bado unaisubiri.
Kumbuka hakuna siku utafika utasema kila ninachohitaji ninacho.
MAISHA ni hatua ukipata unachokitamani leo utatamani kikubwa zaidi kesho.
Ndio maana hata mabilionea bado wanaamka alfajiri kutafuta pesa zaidi.
Si unakumbuka kuna vitu ulikuwa unaviota huko nyuma lakini leo unaviona vya kawaida?
Kuna kazi ulikuwa unaitamani sana lakini leo unatamani kuacha upate nyingine?
Kuna mtu ulikuwa unatamani sana kuwa naye lakini leo unamuona ni wa kawaida sana?
Usipojifunza kuappreciate kila ulichonacho kinapoteza thamani yake.
Jifunze kila siku KUMSHUKURU MUNGU kwa kile ULICHONACHO na KUJIZUIA KUNUNG’UNIKA kwa USICHONACHO.
Hesabu baraka zako, kuna kitu Mungu
amekubariki (Count Your Blessings one by one).
All Rights Reserved|©️ Cantona Group Ltd
Discover more from cantonadigital
Subscribe to get the latest posts sent to your email.