Je! Unaamua kuwa kitabu cha kesho unayeilewa kesho au unataka uwafurahishe wasioiona kesho kwa kufuata mawazo yao badala ya yale Mungu kakupa kwa ajili yako na watu wake?
Unamuhitaji Mungu ili ufanikiwe katika utumishi wako, usije kujidanganya kuwa unajihitaji mwenyewe ili kufanikiwa, Maana huna nguvu za kujifanikisha.
Usichoke kujua na kusema si kwa nguvu zako umefika hapo, maana hukuwahi kupanga na kama ulipanga basi ilivyofanyika si kama ulivyopanga.
Kama unataka kuwa kitabu cha kusomwa hata na vizazi vijavyo, lazima uhakikishe unajisoma na kujielewa mwenyewe na mawazo yako na ujumbe wako. Lakini kama unataka kuwa kitabu cha kusomwa Leo na kusahauliwa basi endelea kutafuta kueleweka na watu wa Leo.
Kumbuka unaowasoma na kuwaelewa leo Jana na juzi hawakueleweka maana waliishi Jana wakiiwaza leo na wakaiandaa leo ili wewe wa leo usaidiwe na Jana yao. Sio vibaya kama utaeleweka leo,lakini lazima uanze kujielewa kabla hawajakuelewa wengine.
Kile ufanyacho ukiwa peke yako ndio matendo yako, kile usemacho kukiwa hakuna anayekusikia ndio maneno yako ya kweli, NA KILE UOMBACHO UKIWA PEKE YAKO NDIO UHALISIA WA MAISHA YAKO KWA MUNGU.
Kujitenga (solitary place) ni ibada pia lazima ufike mahali uheshimu kipindi cha kuwa peke yako kwa kila jambo, maana wakati wengine hawakusikii Mungu anakusikia, hawakuoni Mungu anakuona, hawakutafuti Mungu anakutafuta, hawakusemeshi Mungu anakusemesha, USIWE MJINGA KUKAA NA MAWAZO UWAPO PEKE YAKO NDIO MUDA MZURI SANA WA KUFANYA MAAMUZI NA MUNGU WAKO MAISHANI MWAKO.
#Iposiku #GetInspired #CantonaJosephMotivates #CantonaJosephWorld
All rights reserved ©2019

FortuneBaraka Photography
Discover more from cantonadigital
Subscribe to get the latest posts sent to your email.