Aina 3 Za Marafiki (Sicho Unachofikiria)
____1. Friendship Of Utility
Hawa ni watu ambao wako karibu yetu kwa sababu kuna vitu ambavyo sisi tunafaidika kutoka kwao…
…na wao wanafaidika kutoka kwetu.
Mara nyingi sana huwa ni watu tunaowapata katika mazingira ambayo na sisi huwa tunakuwepo kila siku.
Mfano wa aina hii ni wale tunaowapata tukiwa darasani pamoja…
Tukiwa ofisi moja…
Tukiwa eneo moja tunalofanya biashara n.k…
Hii ndio maana unaweza kuona mtu ni Rafiki yako sana mlipokuwa shule…
…au ulipokuwa ofisi fulani na mlikuwa mnafuatana kila mahali.
Lakini baada ya shule kuisha au kuhamia ofisi nyingine basi mtu huyo hata hamuwasiliani tena.
Sio kwa sababu mmegombana, bali ni kwa sababu kile kilichokuwa kinawaunganisha hakipo tena.
Hivyo unatakiwa kujua marafiki wa namna hii.
Na kujua mambo ambayo unatakiwa kuwashirikisha…
…na yale ambayo hautakiwi kuwashirikisha pia.
Ila pia itakusaidia kujua uwategemee kiasi gani katika mipango yako ya mbeleni pia.
©️ Cantona Group Ltd
All Rights Reserved 2024
Discover more from cantonadigital
Subscribe to get the latest posts sent to your email.