Usiwe na Visingizio kwenye kila kitu.

Wewe Unatoa VISINGIZIO GANI?

Kuna mambo makubwa unaweza kuyafanya Kwenye maisha yako…

…Kama utaacha KUTOA VISINGIZIO.

Hivi unajua, visingizio kwenye maisha yako HAVITAISHA?

Yaani, Kwenye kila hatua ya maisha yako na kwenye kila unachofanya…

…UKITAFUTA visingizio utavipata.

Watu wanaofanikiwa sio kwamba hawana VISINGIZIO vya kuvitumia…

…bali wameamua kuwa HAKUNA KITAKACHOWAZUIA.

Naomba nikukumbushe, kuna VITU usipoamua kuvikabili leo…

…HAUTAVIKABILI TENA.

Mae West alisema…

“You Only Live Once, but if you do it right, once is enough”

{Unaishi Mara moja tu, Ila Kama ukitumia muda wako vizuri, hiyo Mara moja INATOSHA}.

Kumbuka unapoendelea kutoa VISINGIZIO, kuna wenzako WANAPIGA HATUA.

Wanajilazimisha KUFANYA katikati ya changamoto ambazo wewe zinakukwamisha.

Leo, weka visingizio pembeni na AMUA KUJITOA MZIMA MZIMA, liwale na liwe.

Kuna UKUBWA wako ambao hautaweza kuuona hadi UMEWEKA VISINGIZIO pembeni.

Kama umejifunza kitu comment “NITAJITOA MZIMA MZIMA, Liwalo Na Liwe”

© Cantona Group Ltd


Discover more from cantonadigital

Subscribe to get the latest posts sent to your email.

Leave a comment