Luka 1:41 “Ikawa Elisabeti aliposikia kule kuamkia kwake Mariamu, kitoto KICHANGA kikaruka NDANI ya tumbo lake Elisabeti akajazwa Roho Mtakatifu” BHN
Kulikuwa na muunganiko mkubwa sana wa HATIMA Kati ya ALICHOBEBA Mariam (Yesu) na alichobeba Elizabeth (Yohana Mbatizaji). Mara baada ya Mariam kuonana na Elizabeth, ndani yake AKAPATA “Signal” kuwa kuna kitu kinawaunganisha.
Moja ya ombi MUHIMU kwenye maisha, ni kukutana na watu wenye MUUNGANIKO na HATIMA Yetu
na kile tukichokibeba (NDOTO, MAONO. KIPAJI n.k) na Kisha KUWATAMBUA.
Kila MARIAM huwa ana ELIZABETH wake yuko mahali, mkipishana huwa inachelewesha kasi yako ya kufika unakokwenda.
Nakuombea Mungu AKUFUNGUE MACHO na AKUKUTANISHE na Elizabeth wako mapema bila Kuchelewa ili HATIMA yako ISICHELEWE. Na ukikutana nao upate “signal” za kukujulisha kuwa ndio wenyewe.
TheHeartBeatofAfrica
Discover more from cantonadigital
Subscribe to get the latest posts sent to your email.