Radio Fortune Africa -Na Cantona Joseph
https://zeno.fm/radio/radio-fortune-africa
HIMIZO LA KWANZA – 31 Julai 2019
Maisha yangu ya ujana ningali mwanafunzi katika shule ya upili,nilikuwa kiongozi,kiranja mkuu aliyesimamia jumba la maakuli [dinning hall captain] Mwenyekiti wa ushirika wa wanafunzi wakristo shuleni yaani [Christian Union] na mwenyekiti wa chama cha kiswahili na habari shuleni,nilisimamia haki,nilihubiria vijana wenzangu na iwapo nisingekua mwanahabari leo hii ningelikua Mwanajeshi anayehubiri injili,Mwalimu anayehubiri injili,Mwanasoka anayehubiri injili au Polisi anayehubiri injili.
Nilipenda taaluma nilizotaja hapo.Lakini Mungu akanipa jukwa la Mwanahabari ambaye analifahamu hilo na ndipo nimeitikia mwito kuimba nyimbo za injili na Mungu amenipa jukwa ninapo andaa vipindi na kutangaza mwito wangu,kushauri,himiza kutia moyo chini ya jua hamna lisilowezekana iwapo unamtumainia Mungu ,napenda kushauri familia umuhimu wa Mungu maishani mwao.
Shiriki nami vitani nikiwa hai,simama nami nikiwa hai,tembea nami wakati huu.Usiolewe mwisho wa safari.
Taifa la Israel liliwahi kupata shujaa anaitwa Samson ambaye alikuwa mnadhiri wa Mungu, na mwamuzi kwa miaka 20.
Maisha yake yalijaa skendo lakini alifanya ubabe kwa utawala wa kifilisti ambao uliwatawala Israel kwa miaka ya kutosha. Agano lake lilikuwa kutonyoa nywele na kwa kipindi ameishi maadamu nywele zipo kichwani hakuwahi ogopa adui yeyote, BAHATI MBAYA SANA WATU WAKE ISRAEL WALIFANYA MAKOSA AMBAYO HADI LEO WATU WA MUNGU WENGI HUFANYA VILEVILE KISHA HUGUNDUA MWISHONI NA KUJUTA.
Nitakupa mifano miwili
- Siku moja Samson aliwachokoza wafilisti, wakaamua kufanya vita ila Watu wake waliogopa vita wakaona ni heri wamsaliti shujaa wao kwa KUMFUNGA NA KUMPELEKA KWA ADUI KULIKO KUPIGANIA HAKI YAO ILIYOKALIWA NA ADUI YAO.
Nampenda Samson hakutaka ugomvi na watu wake alikubali kusalitiwa lakini akiwa anakabidhiwa alikata kamba akaokota mfupa wa Punda akapigana peke yake akaua maadui 1000. JAMBO LILILONIUMA WATU WAKE PAMOJA NA KUONA KAWAPIGA MAADUI HAWAKUJUA ULE NDIO ULIKUWA WAKATI WA KUUNGANA NAYE KUSHINDA VITA NA KUTANGAZA UHURU WAO, Ndio kwanza walijikausha kama hawaoni kitu. Soma Waamuzi sura yote ya 15
Mfano wa pili
Ni siku kafanya kosa na katobolewa macho, kisha kufungwa, LAKINI NYWELE ZAKE ZILIPOOTA ALILIPIZA KWA KUANGUSHA JENGO NA KUUA ADUI WENGI ZAIDI Kuliko aliowahi ua akiwa hai. KINACHOSIKITISHA ALIPOKUFA TU, NDIPO WATU WAKE ( ISRAEL) WAKAJITOKEZA KUCHUKUA MWILI KWA MBWEMBWE KWENDA KUMZIKA. Soma Waamuzi tena sura yote ya 16
WALIKOSEA WAPI?
Walichofanya mwishoni alipokufa walipaswa wafanye mwanzoni akiwa hai, HILI NDILO KOSA LINALOGHARIMU NDOA, FAMILIA, TAASISII, JAMII, NA NCHI NYINGI. Mtu maadamu akiwa hai ,watu hawamtambui anapofanya vizuri,hapongezwi anaposhinda vita,wazazi wengi wametekelezwa na watoto wao,hawanunuliwi mavazi hawapatiwi chakula,hata malipo ya hospitali hawapati kutoka kwa watoto wao,hawatembelewi wameachwa vijijini,wakati ukija unasikia mzazi,,,,,mzazi swala ambalo nimeshuhudia.Nipende nikiwa hai,ungana nami wakati nikiwa hai kwenye vita.
Gharama ya kosa hili Mara zote huleta majuto na hapo ndipo neno NINGEJUA/TUNGEJUA husikika Sana. Hakuna faida ya KUMUENZI SHUJAA ALIYEKUFA KWA NYIMBO, MAANDIKO, MAOMBOLEZO, NA MBWEMBWE NYINGI ZA KUMBUKUMBU ZA MINARA, WAKATI ANGEENZIWA NA KUUNGWA MKONO AKIWA HAI YAWEZEKANA KABISA ANGESAIDIA KUKOMBOA KWA MUDA MFUPI TAIFA NA KULIFANYA LIDUMU LIKIFURAHIA FAIDA YA USHUJAA WAKE HATA KWA VIZAZI VYA BAADAYE.
Kwa taarifa yako Iliwagharimu Israel miaka mingi kuja kujitawala ilibidi aje atokee shujaa mwingine DAUDI kukomesha kabisa utawala wa unyonyaji na kugadamizwa na Wafilisti.
Naomba isiwe hivyo kwako, kwa ndoa yako, familia yako, taasisi yako, jamii yako, Taifa lak,biashara yako ndoto yako. Thamini kikiwa hai usijute kikifa.
CantonaJosephMotivates. #Iposiku #Getlnspired #Itissettled

Cantona akihubiria wanafunzi wenzake shuleni enzi ya ujana wake.TUMEUONA MKONO WAKO,UMETUTOA MBALI SANA BWANA.UNAWAINUA WATU KUTOKA CHINI.tumeuona kweli.

All Rights Reserved © The Cantona Group PLC||2019
Discover more from cantonadigital
Subscribe to get the latest posts sent to your email.