Siku ya wauguzi duniani.

Mei 12, Dunia huadhimisha Siku ya wauguzi ambao Wana mchango mkubwa kwenye maisha ya watu.

Takwimu zilizotolewa Oktoba 13, Mwaka 2023 na Agnes Mtawa, Msajili wa Baraza la Wauguzi na Wakunga nchini zilionesha idadii ya wauguzi imefika 47,000 sawa na ongezeko la Kutoka 80% 2019 Hadi 95% Mwaka Jana.

Shirika la Afya ulimwenguni, (WHO) linaeleza, licha ya jukumu muhimu wanalofanya wauguzi katika huduma ya afya, kuna uhaba wa wafanyakazi hao ulimwenguni, uhaba ambao unatarajiwa kuongezeka kadiri idadi ya watu inavyoongezeka.

WHO inasema Wauguzi wana jukumu muhimu katika huduma za afya na mara nyingi ni mashujaa wasiojulikana katika vituo vya huduma za afya na huduma za dharura.

Mara nyingi wao ndio wa kwanza kugundua dharura za kiafya na hufanya kazi katika mstari wa mbele kuzuia magonjwa na utoaji wa huduma ya msingi ya afya, ikiwemo kukuza afya, kuzuia maginjwa, na kutibu.

IKumbukwe kuwa Siku ya wauguzi duniani, huadhimishwa kila tarehe 12 Mei ya kila mwaka, ikiwa ni siku ya kumbukumbu ya kuzaliwa kwa mwanzilishi wa taaluma hii ya uuguzi wa kisasa, Florence Nightingale ambaye angekuwa anatimiza miaka 204 mei 12, 2024.

Alikuwa muuguzi wa Uingereza na anayejulikana kama “mwanamke aliye na taa”. Anachukuliwa kama mwanzilishi wa uuguzi wa kisasa, kwani alikuwa wa kwanza kutumia njia ya kisayansi kupitia utumiaji wa takwimu. Alipendekeza pia shirika la hospitali za kambi.

TheHeartBeatofAfrica


Discover more from cantonadigital

Subscribe to get the latest posts sent to your email.

Leave a comment