Tunza nafasi yako!!!

Utaitunzaje Nafasi Yako?

Kuna mbinu za kupata nafasi…

Na kuna mbinu za kuitunza nafasi.

Watu wengi sana walipoteza nafasi zao…

Ni kwa sababu waliendelea kutumia mbinu kupata badala ya mbinu za kutunza.

Si unajua kuna watu walipata nafasi kwa kutumia VITA?

Basi wakishaingia kwenye nafasi wanataka kuendeleza vita…

…badala ya kubadilisha mbinu.

Kuna mbinu 2 zimethibitika zitakusaidia kudumisha nafasi uliyopata:

Moja ni Mahusiano.

Yaani, hakikisha umeboresha mahusiano yako na watu.

Ikiwezekana, wale waliokuwa maadui wakati unatafuta nafasi.

Tafuta namna ya kuwapunguza, itakusaidia kudumu.

Usipigane vita pasipo na ulazima…

…kuna wakati diplomasia inalipa zaidi unapokuwa tayari kwenye KITI.

Mbili, pata MATOKEO.

Hakikisha VITENDO vinaongea zaidi kuliko MDOMO.

Usisahau kuwa vitendo vina sauti.

Fanya katika namna ambayo wale waliokuwa wanakupinga kwa kidhani HAUWEZI…

…wajibiwe na Matendo yako

Kumbuka kuna wengi wanaweza kuja UPANDE wako kama haya mawili utayafanya kwa ufanisi.

Kama umejifunza kitu comment maneno “NIMEJIFUNZA KITU”


Discover more from cantonadigital

Subscribe to get the latest posts sent to your email.

Leave a comment